Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-02 18:54:46    
Mfanyabiashara mkubwa wa biashara ya rejareja aliyeko nchini China

cri

Miaka zaidi ya 40 iliyopita, mmarekani mmoja anayeitwa Sam Walton alifungua duka moja la bidhaa za vyakula na matumizi ya nyumbani katika tarafa kwao lililojulikana kwa Wal-Mart. Baada ya kuendelezwa kwa miongo kadhaa, duka lake lile dogo sasa limekuwa kampuni ya kwanza kwa ukubwa duniani katika sekta ya uuzaji bidhaa kwa rejareja, ambayo pato lake kutokana na mauzo limezidi dola za kimarekani bilioni 280 kwa mwaka. Mwaka 1996 Wal-Mart iliingia nchini China. Baada ya miaka 9 kupita, Je sasa hivi Wal-Mart nchini imekuwaje?

Kwa kawaida bidhaa zinazouzwa katika maduka ya Wal-Mart zinafikia zaidi ya elfu 20, ambapo maduka ya wanachama yanauza bidhaa za kiwango cha juu zilizotoka sehemu mbalimbali duniani, wakati maduka yaliyofunguliwa kwenye makazi ya mijini yanauza vyakula na bidhaa ndogo ndogo za matumizi ya nyumbani. Lakini maduka yote ya Wal-Mart yamewawekea wateja mazingira bora ya kununua bidhaa.

Katika biashara ya rejareja, bei nafuu daima ni kitu muhimu sana kwa maendeleo ya duka. Tokea mwanzoni Wal-Mart iliahidi kuweka bei nafuu kila siku kwa wateja wake. Msimamizi mkuu anayeshughulikia mambo ya nje wa kampuni ya Wal-Mart Bw. Xu Jun alisema,

"Katika shughuli zetu za biashara tunajitahidi kuokoa matumizi ya fedha yakiwa ni pamoja na kupanga sehemu iliyo chini ya jengo kuwa ofisi yetu hapa mjini Beijing, ili kutumia fedha zilizookolewa katika shughuli za uendeshaji, kiofisi na utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu katika kupunguza bei za vitu kwa ajili ya manufaa ya wateja."

Kwa kampuni yoyote ya kimataifa kuwa na uwezo wa kuendana na hali tofauti ya kimasoko ya sehemu iliyopo, ni moja ya sifa inayopaswa kuwa nayo. Bw. Xu Jun alisema kuwa hivi sasa Wal-Mart ina maduka zaidi ya 5,000 katika nchi kumi duniani ambayo yanapokea wateja karibu milioni 140 kwa wiki. Wal-Mart inapofungua tawi katika nchi yoyote moja duniani inaweka mpango na kufanya usanifu kuambatana na hali ya kimasoko, mazingira ya utamaduni na desturi ya ununuzi ya watu wa huko ili kukidhi matakwa ya wateja.

Umaalumu mwingine wa tawi la Wal-Mart nchini China ni kutumia kwa wingi wafanyakazi wa China, habari zinasema kuwa hivi sasa wafanyakazi na wasimamizi wa maduka yote ya Wal-Mart nchini China pamoja na vituo vya usambazaji ni wachina. Naibu mkurugenzi mkuu wa Wal-Mart duniani Bw. Zhuang Mengzhe alisema,

"Idadi ya wafanyakazi wetu nchini China imefikia 25,000, tena viongozi wa maduka yote nchini China ni wachina. Miongoni mwa wafanyakazi wa Wal-Mart nchini China ni watano tu ambao wanatoka nchi za nje, wafanyakazi wa China katika Wal-Mart wanaweza kupewa mafunzo ya kazi na kupandishwa vyeo."

Mbali na kutumia wafanyakazi wa China, Wal-Mart inachukua hatua nyingine za kuikaribia China zaidi zikiwa ni pamoja na kuuza bidhaa nyingi zenye umaalumu wa kichina na kuweka zana nyingi za kuhifadhi vyakula vibichi ili kutosheleza mahitaji wa wateja wa China. Sababu nyingine muhimu kwa Wal-Mart kutumia fursa ya kwenda sehemu mbalimbali duniani kuuza bidhaa kwa rejareja, ni kuwa kampuni hiyo ina mfumo kamili wa usambazaji bidhaa na kupunguza gharama za matumizi ya kampuni. Hivi sasa Wal-Mart ina vituo viwili vya ununuzi na usambazaji bidhaa vya kisasa nchini China ambavyo viko katika miji ya Shenzhen na Tianjin. Naibu mkurugenzi mkuu wa Wal-Mart duniani Bw. Zhuang Mengzhe alisema kuwa, vituo vya kisasa vya ununuzi na usambazaji bidhaa si kama tu vinaweza kupunguza gharama ya matumizi ya kampuni ya Wal-Mart, bali pia vinaweza kusaidia kuongeza ufanisi wa uendeshaji kazi wa kampuni. Alisema,

"Sisi tunatoa teknolojia ya kisasa kwa wafanyabiashara wanaotuletea bidhaa, wanaweza kuona hali ya bidhaa zao zinavyouzwa katika maduka yetu katika mfumo wa mawasiliano ya kompyuta wa vituo vyetu vya usambazaji wa bidhaa, ili waweze kupanga uzalishaji wao kutokana na hali halisi ya uuzaji."

Hivi sasa ununuzi wa bidhaa za China wa kampuni ya Wal-Mart ni mwingi zaidi kuliko bidhaa inazonunua katika nchi za nje. Bw. Meng Zhuagnzhe alisema kuwa pamoja na maendeleo ya Wal-Mart nchini China, wafanyabiashara wengi zaidi wa China watashiriki katika mfumo wa ununuzi Wal-Mart duniani.

Mwaka 2004 Wal-Mart ilinunua bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 18, ambazo ziliuzwa katika matawi yake mbalimbali duniani, katika siku za baadaye Wal-Mart itanunua bidhaa nyingi zaidi za China, wateja wanatarajia bidhaa nzuri na za bei nafuu pamoja na huduma nzuri.

Tarehe 11 mwezi Septemba mwaka 2004 China ilitekeleza ahadi husika ilizotoa wakati wa kujiunga na WTO na kufungua mlango katika sekta ya uuzaji rejareja wa bidhaa. Msimamizi wa mambo ya nje wa kampuni ya Wal-Mart Bw. Xu Jun alisema kuwa, ufunguaji mlango umetoa nafasi kubwa ya maendeleo kwa Wal-Mart, Wal-Mart inafikiria kuwekeza katika miji ya ngazi ya pili na ya sehemu ya magharibi ya China.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-02