Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-03 15:18:12    
Suala la nyuklia ya Iran lafuatiliwa tena

cri

Umoja wa Ulaya umejibu kwa hatua kali kitendo kilichofanywa na Iran tarehe mosi mwezi Agosti kuhusu kuanzisha upya kwa kazi za zana za kushughulikia mabadiliko ya uranium. Ujerumani imeainisha kuwa hii ni hatua ya makosa iliyopigwa na Iran. Ufaransa imeitaka Iran isizushe msukosuko wa kimataifa. Umoja wa Ulaya umesema kuwa kuanzisha upya kazi za zana za kushughulikia mabadiliko ya uranium kwa Iran kunaonesha kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili. Suala la nyuklia ya Iran lililotulia kwa miezi miwili limeanza kufuatiliwa tena.

Mwezi Novemba mwaka jana, Iran ilisimamisha kwa muda shughuli zote kuhusu uranium nzito na kuanzisha mazungumzo na Umoja wa Ulaya kuhusu suala la nyuklia ya Iran. Mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, Umoja wa Ulaya ilieleza kutoa mapendekezo kuhusu suala hilo katika miezi miwili ijayo. Lakini Iran ilitangaza tarehe mosi kuwa saa kumi na moja, alasiri ya siku hiyo ni kikomo cha mwisho kilichowekwa na Iran kwa Umoja wa Ulaya, kama matakwa ya Iran hayatatimizwa, Iran itaanzisha upya mara moja sehemu ya shughuli za mabadiliko ya uranium.

Kuhusu maendeleo mapya ya suala la nyuklia ya Iran, Chansela wa Ujerumani Bw. Gerhard Schroeder alieleza wasiwasi tarehe mbili na kuionya Iran isiendelee na mpango wake wa nyuklia.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bw. Douste Blazy alieleza tarehe 2 kuwa kama Iran itashikilia msimamo wake na kutokubali matakwa ya shirika la nishati ya atomiki la kimataifa, jumuiya ya kimataifa ingewasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama.

Magazeti ya Ulaya yameeleza kuwa msimamo mkali unaochukuliwa na Iran umeongeza wasiwasi wa Umoja wa Ulaya na umoja huo hauwezi kukubali Iran ianzishe hata kazi ndogo ya kusafisha uranium nzito, kwani jambo hilo linakwenda kinyume na lengo la mwisho lililowekwa na nchi za magharibi kwenye suala hilo, tena Marekani iliyoko katika kando nyingine ya bahari ya Atlantic pia haitakubali kufanya hivyo.

Marekani siku zote haiamini kuwa mazungumzo hayo yatapata maendeleo na kuona kuwa, hatimaye suala la nyuklia ya Iran itafikishwa kwenye baraza la usalama.

Kutokana na kitendo cha Iran kutangaza kuanzisha upya shughuli za zana za mabadiliko ya uranium, vyombo vya habari vya Ulaya vina maoni ya aina mbili. Maoni ya aina moja yanaona kuwa kitendo kilichofanywa na Iran miaka miwili iliyopita na hivi karibuni katika suala hilo kitainufaisha zaidi Iran. Maoni ya aina nyingine vinaona kuwa madhumuni ya kitendo hicho cha Iran ni kupima jibu la Umoja wa Ulaya. Lakini baadhi ya vyombo vya habari vinaona kuwa safari hii Iran imecheza mchezo huo kwa kupita kiasi na kusababisha ghadhabu kubwa kwa umoja huo. Kweli, madhumuni ya Iran kufanya hivyo ni mbinu yake ya kupambana na umoja huo katika mazungumzo, ili kujinufaisha. Kama Iran itavunja uhusiano na Umoja wa Ulaya, basi itaweka haki ya kudhibiti suala la nyuklia ya Iran kwa Marekani. Iran haitaki kuona hali hiyo. Kwa hiyo, iwapo Umoja wa Ulaya utarudi nyuma kidogo kwa Iran, Iran inaweza kurudisha uamuzi wake wa kuanzisha upya shughuli za mabadiliko ya uranium na kuendelea na mazungumzo na Umoja wa Ulaya.

Idhaa ya kiswahili 2005-08-03