Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-03 21:03:40    
Teknolojia ya kuunda meli nchini China

cri

Katika enzi ya Ming ambayo ilikuwepo mwazoni mwa karne ya 15, China ilikuwa na teknolojia ya juu kabisa ya kuunda meli na kuwa na msafara mkubwa kabisa wa merikebu duniani. Msafara huo uliokuwa na merikebu kubwa zaidi ya 260 uliongozwa na ofisa mmoja wa China Zheng He na kufanya safari 7 za mbali baharini, ambapo walieneza utamaduni na urafiki wa China kwenye nchi na sehemu zaidi ya 30 za Asia na Afrika, na kuonesha teknolojia ya juu ya kuunda merikebu na uwezo mkubwa wa kufanya safari za baharini kwa watu wa China.

Kabla ya kufanyika kwa safari za Zheng He baharini, teknolojia ya kuunda meli nchini China ili kuwa imefikia hatua ya juu. Kwa mfano katika enzi ya Song ya China miaka 400 kabla ya safari za Zheng He, China ilikuwa imeshaweza kuunda merikebu kubwa kwa ajili ya safari za baharini. Ilipofika zama alipoishi Zheng He, teknolojia ya kuunda merikebu ya China ilikuwa inachukua nafasi ya mbele duniani, merikebu yenye urefu zaidi ya mita 30 iliundwa katika wakati huo, hata mpaka sasa hakuna nchi zinazoweza kuzidi teknolojia hiyo kwa urefu na uwezo.

Lakini kaitka zama za karibuni, teknolojia ya China ya kuunda meli zimerudi nyuma. Kwa sababu meli zilizoundwa na China katika zama za kale zote zilikuwa zinaendeshwa kwa nguvu ya upepo, lakini nchi za magharibi zilivumbua na kutengeneza meli zilizokuwa zinatumia injini ya mvuke na injini ya mafuta. Kwa hivyo kabla ya miaka mia moja iliyopita, China ilianza kujifunza teknolojia ya kuunda meli kutoka kwa nchi za magharibi.

Kutokana na msingi huo, China iliendeleza shughuli za uundaji wa meli katika zama za karibu. Baada ya maendeleo ya karne moja, ilipofika mwanzoni mwa miaka ya 90 ya karne ya 20, teknolojia ya kuunda meli ya China ilipata maendeleo, lakini bado haikufika kiwango cha juu, na zilikuwa zinaweza tu kuunda meli zinazobeba kontena. Baada ya hapo, kutokana na serikali ya China kuweka mkazo sekta hiyo, teknolojia hizo zilianza kuendelea kwa kasi, hivi sasa zimefikia kiwango cha mbele duniani.

Shirika la kuunda meli la China CSSC (China State Shipbuilding Corp.) ni shirika kubwa linalowajibika na shughuli za uundaji wa meli kwenye sehemu ya kusini ya China. Ofisa wa idara ya mambo ya kimataifa ya shirika hilo Bi. Rao Huiqun alieleza:

"mbali na kuunda meli za kawaida, kama vile meli zinazobeba kontena na zinazosafirisha mafuta, shirika letu pia linaweza kuunda meli zenye teknolojia za juu na uwezo mkubwa zaidi, kama vile, meli kubwa za kusafirisha mizigo, meli za kijani zisizoharibu mazingira na meli za kasi zinazobeba abiria na mizigo kwa pamoja."

Mbali na kuunda meli za kawada, China pia inaweza kuunda meli maalum kutokana na mahitaji mbalimbali. Kama vile, meli moja ya pekee duniani ya kuweka chombo cha kuzalisha umeme kwa nguvu ya upepo baharini inaundwa na China kwa ajili ya Uingereza. Meli hiyo imesifiwa na Uingereza kuwa moja kati ya meli 10 zenye ubora wa juu duniani.

Meli hiyo ilisanifiwa na kuundwa na shirika jingine kubwa la kuunda meli la China CSIC (China Shipbuilding Industry Corp.). ofisa mkuu wa shirika hilo Bw. Huang Junmin alisema kuwa, sekta ya uundaji wa meli ni sekta inayotegemea teknolojia mbalimbali, na inapaswa kuendelea kuvumbua teknolojia mpya ili kuongeza uwezo wa ushindani kwenye soko la kimataifa. Alisema:

"shirika letu lina taasisi 28 za utafiti, ambazo ni tegemeo kubwa ya kitekonolojia ya shirika hilo. Hivi karibuni, shirika letu pia limeimarisha ushirikiano wa kiteknolojia na nchi za nje, vifaa vingi vyetu vinapatikana kwa kununua hataza za nje au kushirikiana na nchi za nje katika kuvisanifu. Hivyo, kiwango chetu cha kuunda meli kimeinuka kwa kiasi kikubwa."

Hivi sasa, meli zinazosafirisha liquefied gas ni meli zinazotumia teknolojia za juu kabisa duniani. Mashirika ya kuunda meli ya China yanaweza kuunda meli za aina hiyo, na kufanikiwa kuingia kwenye soko la kimataifa. Mhandisi mmoja wa shirika la uundaji wa meli la Ludong mjini Shanghai Bw. Hu Hongming alisema:

"meli hiyo inaundwa kwa kutumia teknolojia tofauti kuliko meli za kawaida, inaundwa katika mazingira safi yenye nyuzijoto 163 chini ya sifuri. Meli ya aina hiyo ni ya hali ya juu kabisa katika sekta ya uundani wa meli duniani, na tumeanza kuziunda kwa muda si mrefu."

Kuhusu kiwango cha teknolojia za kuunda meli za China, naibu mkurugenzi wa kamati ya viwanda vya sayansi na teknolojia za ulinzi ya China, ambayo ni idara kuu ya usimamizi wa sekta ya uundaji meli ya China, Bw. Zhang Guangqin alisema:

"hivi sasa, licha ya meli ya aina chache kama vile meli ya fahari ya utalii (yacht), China inaweza kuunda meli zinazolingana na kanuni za kimataifa na zinazosafiri kwenye eneo mbalimbali baharini."

Pamoja na maendeleo ya teknolojia za kuunda meli, sekta ya uundaji meli ya China inaendelea kwa kasi. Katika miaka 10 iliyopita, idadi ya meli zilizoundawa na China ilichukua nafasi ya tatu duniani baada ya Korea ya Kusini na Japan, na kuendelea kushika nafasi hiyo mpaka leo. Sekta ya uundaji wa meli ya China inayostawi inavutia wateja kutoka nchi mbalimbali duniani, meli zilizoundawa na China zimeuzwa katika nchi zaidi ya 60 duniani, zikiwemo Marekani, na baadhi ya nchi za Ulaya na Asia.

Kutokana maendeleo makubwa ya tekenolojia, sekta ya uundaji wa meli inaingia kwenye enzi mpya ya ustawi, na kutoa mchango kwa maendeleo ya sekta ya usafirishaji kwa meli duniani.

  

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-03