Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-03 21:27:47    
Mapishi ya kupika doufu pamoja na vitu vingi

cri

Mahitaji

Doufu gramu 250, karoti gramu 50, nyama ya ng'ombe gramu 100, uyoga gramu 100, haragwe gramu 50, mafuta gramu 250, mvinyo wa kupikia gramu 25, mchuzi wa soya gramu 50, chumvi gramu 2, sukari gramu 10, vitunguu maji gramu 10, tangawizi gramu 5, maji ya wanga gramu 10.

Njia

1. kata doufu iwe vipande vipande, ondoa gamba la karoti na uikate karoti na nyama ya ngom'be ziwe michamraba midogo midogo, na kuikata vitunguu maji na tangawizi kuwa vipande vipande vidogo.

2. mimina maji kwenye sufuria na kuyachemsha, tia vipande vya karoti na haragwe, zipakue na kuzikausha. Pasha moto tena, tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya doufu na kuvikaanga, vipakue.

3. pasha moto na tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe nyuzi ya asilimia 60, tia vipande vya nyama ya ng'ombe, vitunguu maji na tangawizi, korogokoroga, mimina maji kidogo, tia mvinyo wa kupikia, mchuzi wa soya, chumvi na sukari, baada ya maji kuchemsha, tia vipande vya doufu, karoti na haragwe, halafu mimina maji ya wanga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.