Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-04 10:21:47    
Nishati safi yaboresha maisha ya wakulima wa sehemu ya magharibi ya China

cri

Jiko la Bw. Yang Changming ni zuri sana. Alitumia dakika 15 kupiga chakula kwa jiko la gesi ya kinyesi, lakini wali uliopikwa kwa chombo cha umeme cha kupikia wali(electric cooker) umepelekwa mezani.

Katika vijiji kadhaa vya sehemu ya magharibi ya China, maisha ya Bw. Yang ni mfano wa familia za wakulima zilizonufaika na nishati safi. Nishati mpya ikiwemo gesi ya kinyesi na umeme uliozalishwa kwa nguvu ya maji umekuwa nishati muhimu katika maisha ya wakulima wa sehemu ya magharibi ya China. Wakulima wa sehemu hiyo wameagana na maisha ya kuwasha moto kwa kuni.

Bw. Yang Changming mwenye umri wa miaka 57 mwaka huu anasema kuwa, zamani alikuwa anapika chakula kwa kuni, jiko lake lilikuwa linajaa moshi, watu hawakuweza kuvumilia. Lakini hivi sasa walitumia gesi ya kinyesi na umeme uliozalishwa kwa nguvu ya maji, si kama tu ni safi bali pia hauna madhara kwa afya, kupika chakula kumebadilishwa kuwa ni jambo rahisi.

Mradi wa kuanzisha vituo vidogo vya kuzalisha umeme kwa nguvu za maji unalenga kuhifadhi mazingira na kuboresha maisha ya wakulima, toka mwaka 2003 tangu mradi huo ulipoanza kutekelezwa katika vijiji vya China, wakulima laki tatu wamenufaika na mradi huo. Wakati huo huo, miradi ya ujenzi wa nishati za gesi ya kinyesi, upepo na nguvu ya jua ilifanyika katika sehemu ya magharini ya China.

Kukata miti ni sababu muhimu ya kutoweka kwa misitu, na kuyafanya mashamba kuwa jangwa, na kuleta mmomonyoko wa ardhi, hivyo kusababisha hali mbaya ya mazingira katika sehemu ya magharibi ya China ni mbaya.

Bw. Yang anaishi katika kijiji kimoja cha mkoa wa Guizhou ambacho kinazungukwa na milima, zamani wakulima walikuwa wanakata miti kila siku. Bw. Yang alisema kuwa, hivi sasa wakulima hawakati miti, gesi ya kinyesi na umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji unaweza kukidhi mahitaji ya maisha. Miti ilianza kukua kwa mara nyingine.

" kutumia gesi ya kinyesi kunaweza kuongeza mapato. Zamani tulikwenda nje kukata kuni, lakini hivi sasa tunatumia muda huo kufanya kazi ili kupata pesa zaidi." Bw. Yang alisema kuwa, zamani kila familia ilikuwa na mtu mmoja aliyeshughulikia kukata kuni, lakini hivi sasa hakuna miti karibu na nyumbani kwake, ni vigumu kupata kuni, walikuwa wanapaswa kwenda mbali kukata kuni."

Naibu waziri wa nishati ya maji Suo Lisheng alisema kuwa, kazi ya mwaka mmoja imeonesha kuwa, mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu za maji ni jambo lenye ubora mwingi. Mafanikio yamepatikana katika vituo vya majaribio. Hivi sasa mradi huo umenufaisha wakulima laki tatu, mkulima mmoja anabana matumizi ya yuan mia moja kwa utoaji wa nishati, hii ina maana kuwa, kila mwaka wakulima wanaweza kubana matumizi ya nishati kwa yuan milioni 30.

Hivi sasa, mradi huo unafanyika katika mikoa ya Sichuan, Yunan na Guizhou, hadi mwaka 2020 mradi huo wa kuzalisha umeme kwa nguvu za maji utakamilika kimasingi kote nchini China.

Idhaa ya kiswahili 2005-08-04