Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-04 17:49:41    
Mkoa unaojiendesha wa watibet

cri

Mkoa unaojiendesha wa Tibet ulianzishwa rasmi mwezi Septemba mwaka 1965, jambo hilo lilionesha kuwa, sehemu ya Tibet iliingia katika jamii ya ujamaa yenye usawa kutoka jamii ya mfumo wa utumwa wa ukabaila. Watu wa sehemu ya Tibet walianza kushughulikia wenyewe eneo lao lenye kilomita za mraba milioni 1.2 kutokana na haki waliyopewa na katiba ya China na mfumo wa kujiendesha wa sehemu ya kikabila, sehemu hiyo kabla ya kukombolewa ilikuwa inamilikiwa na makabaila, mahekalu na watawa wakubwa.

Mkurugenzi wa bunge la mkoa unaojiendesha wa Tibet Bwana Lie Que mwenye umri wa miaka 61 alishuhudia mambo hayo. Anasema:

"Nilizaliwa katika familia ya mkulima mtumwa katika wilaya ya Jiangzhi mkoani Tibet. Nilipokuwa mtoto nilishuhudia ubaya wa mfumo wa utumwa, na jinsi makabaila na watawa wakubwa walivyowakandamiza wakulima watumwa. Mwaka 1951, sehemu ya Tibet ilipata ukombozi kwa njia ya amani, na kuniwezesha kupata elimu ya kisasa. Nimewahi kuwa mwalimu, pia nimewahi kufanya kazi katika idara za wilaya, tarafa hadi mji wa Lahsa. Mwaka 2003, niliteuliwa kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya bunge la mkoa wa Tibet."

Mkoa unaojiendesha wa Tibet ni moja kati ya mikoa mitano inayojiendesha nchini China. Bw. Lie Que alisema kuwa, bunge la mkoa unaojiendesha wa Tibet si kama tu ni mamlaka ya mitaa ya kitaifa, bali pia ni chombo cha kisheria cha kutekeleza sera za kushughulikia mambo ya kikabila, ni uhakikisho muhimu kwa watu wa makabila mbalimbali wa mkoa wa Tibet kuendesha shughuli zao wenyewe. Anasema:

"Wajumbe wa kabila la watibet na makabila mengine madogomadogo wanachukua asilimia 70 ya wajumbe wote wa bunge hilo; kati ya wajumbe hao, si kama tu kuna wawakilishi wa wakulima, wafugaji na wafanyakazi, bali pia kuna wawakilishi wa idara za kidini. Nusu ya wajumbe hao wana diploma au shahada ya chuo kikuu, kiasi cha wataalamu, wasomi, na watu mashuhuri kinaongezeka hatua kwa hatua."

Bw. Lie Que alisema kuwa, kwa mujibu wa katiba ya China na sheria ya kujiendesha katika maeneo ya makabila madogo, bunge la mkoa unaojiendesha wa Tibet si kama tu limepewa madaraka yanayolingana na idara za ngazi yake, bali pia limepewa haki ya kushughulikia mambo ya siasa, uchumi, utamaduni na maendeleo ya jamii ya sehemu hiyo. Linaweza kutunga sheria kutokana na hali halisi ya Tibet. Anasema:

"Ilipofika mwezi Juni mwaka huu, bunge la mkoa wa Tibet kwa jumla lilitunga sheria 237, ambazo zinahusiana na sekta mbalimbali za siasa, uchumi, utamaduni na elimu, sheria hizo zimetoa mchango mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na jamii ya mkoa huo."

Bw. Lie Que alidokeza kuwa, tangu kufanyika kwa mkutano wa kwanza wa bunge la kwanza la mkoa wa Tibet mwaka 1965 hadi leo, bunge hilo limepokea maoni, miswada, na mapendekezo 7000 kutoka kwa wajumbe, ambayo yameonesha matakwa na mahitaji ya watu wa makabila mbalimbali mkoani humo.

Katika sehemu ya Tibet, ambapo watu wengi ni waumini wa dini ya kibudha ya kitibet, watu wa kabila la Watibet wanachukua asilimia kubwa ya idadi ya makarani wa idara za serikali ya mkoa. Watoto wanapewa elimu ya lazima ya miaka 9 , na mafunzo ya lugha ya kitibet yanatiliwa maanani sana. Taarifa za serikali na nyaraka za kisheria zote zinachapishwa kwa lugha mbili za Kichina na Kitibet. Vituo vya radio na televisheni vya mkoa huo vinatangaza vipindi kwa lugha ya Kitibet, watu wa kabila la Watibet na makabila mengine madogo wana usawa na wanaishi kwa masikilizano. Wakazi wa mkoa huo si kama tu wana haki ya kustawisha uchumi na jamii, bali pia wana haki ya kurithi na kuenzi utamaduni wa jadi na kuwa na uhuru wa kuamini dini.

Bwana Gesanyixi aliyefanya utafiti kuhusu utamaduni wa jadi wa Tibet na kazi ya uchapishaji, anasema:

"Katika miaka ya karibuni tulichapisha vitabu vingi kuhusu sekta mbalimbali za kabila la Watibet, kama vile historia, utibabu, unajimu hisabati, hali ya dini mbalimbali, fasihi na mashairi."

Katika miaka 40 iliyopita tangu mkoa unaojiendesha wa Tibet uanzishwe, mabadiliko makubwa yamepatikana. Katika miaka ya karibuni, mkoa wa Tibet ulidumisha ongezeko la kasi la kiuchumi, na utulivu wa kijamii, hali ya maisha ya watu inainuka siku hadi siku, mkoa wa Tibet uko katika kipindi kizuri kabisa cha maendeleo katika historia yake.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-04