Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-04 18:53:16    
Mazungumzo kuhusu suala la nyukilia la penisula ya Korea yaingia wakati muhimu

cri
    Duru la nne la mazungumzo ya pande 6 limefanyika kwa siku kumi hadi tarehe 4 mwezi Agosti. Ingawa pande mbalimbali bado hazijafikia makubaliano kuhusu waraka wa pamoja, lakini zimeeleza kuwa zitajitahidi zaidi ili kuafikiana kwenye mswada wa nne wa waraka wa pamoja uliotolewa na China tarehe 2. Habari zinasema kuwa tarehe 4 asubuhi pande zote zinazoshiriki kwenye mazungumzo zilikubaliana kufanya majadiliano kuhusu waraka huo kwa mashauriano ya pande mbili. Kisha pande mbalimbali zitaamua kama uitishwe mkutano wa viongozi wa ujumbe wa nchi mbalimbali au mkutano wa wajumbe wote au la.

    Tarehe 3 asubuhi pande mbalimbali zilikuwa na mazungumzo ya pande mbili kwa muda mrefu kuhusu waraka huo, lakini hadi alasiri hazikuweza kufikia makubaliano kuhusu mambo yaliyomo kwenye waraka huo. Siku hiyo usiku China ikiwa ni mwenyeji wa mkutano huo iliendelea kuzihimiza kuwa na mazungumzo, China ilifanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na ujumbe wa Korea ya kaskazini na ujumbe wa Marekani na kuzisuluhisha kuhusu waraka huo wa pamoja. Lakini hadi usiku wa manane bado hakukuwa na habari yoyote ya kufurahisha. Kuhusu waraka huo wa pamoja, pande mbalimbali zilikuwa na matarajio makubwa, lakini mazungumzo kuhusu mswada wa waraka wa pamoja yamefanyika kwa siku nyingi, katika muda huo China imetoa miswada minne, lakini pande hizo hazikuweza kufikia makubaliano.

    Kiongozi wa ujumbe wa Marekani Bw. Christopher Hill tarehe 3 alisema kuwa mswada wa nne wa waraka wa pamoja ulibuniwa vizuri ukiwa na mambo mengi yenye manufaa na kusaidia kuafikiana hatimaye. Anaona kuwa huo ungekuwa mswada wa mwisho wa waraka wa pamoja, aliongeza kuwa tarehe 3 usiku ujumbe wa Marekani haukufanya majadiliano ya pande mbili na ujumbe wa Korea ya Kaskazini. Na tarehe 4 pia hayakupangwa mazungumzo ya pande mbili kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini. Kabla ya hapo Bw. Hill alisema kuwa serikali ya Marekani imekubali mswada wa nne wa waraka wa pamoja uliotolewa na China, na duru hilo la mazungumzo linakaribia mwisho.

    Kiongozi wa ujumbe wa Russia Bw. Alexander Alexeyev ambaye alirudi Russia kutokana na shughuli za haraka za nchini humo, tarehe 3 alisema kuwa mazungumzo yalipiga hatua za mbele lakini bado hayajapata mafanikio.

    Habari zinasema kuwa mswada wa 4 wa waraka wa pamoja umejumuisha misimamo na matakwa ya pande mbalimbali katika mazungumzo yaliyofanyika, tena umezingatia kadiri uwezavyo mambo yanayofuatiliwa na pande mbalimbali. Mswada wa 4 wa waraka huo unasisitiza kuwa pande zote zinatarajia kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na silaha za nyuklia, hivyo Korea ya Kaskazini itaacha majaribio ya nyuklia kiasi cha kuruhusu kukaguliwa, wakati pande zote nyingine zitatekeleza hatua zinazotarajiwa. Mswada huo pia umethibitisha kuwa "Azimio la kutokomeza silaha za nyuklia katika peninsula ya Korea" lililoanza kufanya kazi mwaka 1992 ni msingi wa utatuzi wa masuala husika. Kuhusu kufanya uhusiano nchi kuwa wa kawaida, ambayo ni moja ya masuala nyeti, mswada wa waraka umetumia maneno ya "kuhimiza kutengenea kwa uhusiano kati ya Marekani, Japan na Korea ya Kaskazini", na mpango kamili husika utashughulikiwa na nchi hizo tatu katika mazungumzo ya pande mbili katika siku za baadaye. Aidha, mswada huo haukutaja masuala ya "haki za binadamu" na "makombora" yaliyotolewa na Marekani pamoja na suala lililotolewa na Japan kuhusu utatuzi wa suala la "utekaji nyara" na "makombora", isipokuwa unatumia "suala la ubinadamu".

    Habari zinasema kuwa endapo pande zote zitaweza kuafikiana kuhusu mswada wa waraka wa pamoja, basi waraka huo wa pamoja utaweza kutolewa kama taarifa ya pamoja. Hiyo itakuwa ni taarifa ya kwanza ya pamoja kutolewa tangu kuanzishwa kwa mazungumzo ya pande 6. Lakini hali halisi ni kwamba Korea ya Kaskazini na Marekani haziaminiani na suala la nyuklia la peninsula ya Korea ni lenye utata mwingi, hivyo si jambo rahisi kwa pande hizo kufikia makubaliano kuhusu waraka huo wa pamoja.

Idhaa ya Kiswahili