Katika video iliyooneshwa tarehe 4 na kituo cha televisheni cha Al-Jazeera, kiongozi wa pili wa kundi la Al-Qaeda Ayman al-Zawahri alitishia kuwa, kundi hilo litaanzisha mashambulizi mengi zaidi dhidi ya Marekani na Uingereza.
Zawahri alisema kuwa, Bw. Tony Blair lazima awajibike na tukio la milipuko lililotokea huko London, sera yake huhusu Iraq inaweza kuleta mashambulzi mengi tu. Zawahri pia aliwalaani Rais George W. Bush na maofisa waandamizi wa Marekani kuficha ukweli kuhusu hali ya Iraq. Alisisitiza kuwa, Marekani haina njia nyingine nchini Iraq ila kuondoa jeshi lake kutoka nchini humo. Pia alionya nchi nyingine za magharibi zilizopeleka majeshi nchini Iraq kuwa, kama hazitaondoa majeshi yao, pia atazishambuliwa.
Siku hiyo Rais Bush alisema kuwa, Marekani haitatishika kutokana na tishio hilo na kuondoa jeshi lake nchini Iraq. Alisema, Iraq ni sehemu moja ya vita dhidi ya ugaidi, na jeshi la Marekani litaendelea kukaa nchini humo hadi litakapomaliza juhumu lake.
Wachambuzi wa kiarabu wanaona kuwa, kutokana na Zawahri kuwa ni kiongozi muhimu wa kundi la Al-Qaeda, tishio lake limeonesha kuwa, kundi la Al-Qaeda litachukua hatua mpya dhidi ya Marekani na Uingereza.
Kwanza, Zawahri amelaani sera za Marekani na Uingereza kuhusu Iraq, na kutaka jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani liondoke Iraq. Mwezi Januari na Mwezi Juni mwaka huu, Zawahri aliipinga Marekani kutekeleza mpango wa demokrasia huko Mashariki ya Kati, na kuzitaka nchi za magharibi ziiheshimu imani ya Kiislamu. Lakini mara hiyo alizingatia suala la Iraq, na kuyataka majeshi ya nchi za nje yaondoke Iraq, kutoiba maliasili ya mafuta ya Iraq, na kutounga mkono "mamlaka haramu" ya Iraq, na pia alitoa mwito akiyataka makundi madogo nchini Iraq yaanzishe mashambulizi mengi dhidi ya shabaha za Uingereza na Marekani.
Pili, kila Zawahri akionekana kwenye video, mashambulizi makubwa ya kigaidi yatatokea. Yeye hupasha habari kupitia rekodi na mkanda wa video. Hotuba zake zinachukuliwa kama ni uongozi wa wafuasi wa kundi la Al-Qaeda duniani, na wanaanzisha mashambulizi kwa mujibu wa hotuba hizo. Ingawa katika hotuba hiyo haikukiri kuwa kundi la Al-Qaeda linahusika na milipuko iliyozuka huko London na Sharm el-Sheikh, lakini ilitaka vijana wakerekewe wa dini duniani waanzishe mashambulizi mengi, ili kupinga muungano wa nchi za magharibi unaoongozwa na Marekani na Uingereza. Tarehe 7 mwezi Julai, milipuko iliyotokea huko London ilisababisha vifo vya watu 56. Jeshi la Marekani nchini Iraq hivi karibuni pia lilishambuliwa mara nyingi. Tarehe 3, askari 14 wa jeshi la Marekani waliuawa magharibi mwa Iraq, hadi hapo idadi ya askari wa Marekani waliokufa nchini Iraq imekuwa zaidi ya 1820. Takwimu mpya za maoni ya raia za Uingereza pia zimeonesha kuwa, theluthi mbili ya Waingereza wanaona kuwa, milipuko iliyozuka mjini London inahusiana na vita vya Iraq, na theluthi ya Waingereza wanaona kuwa ni Bw. Tony Blari lazima awajibike. Na matokeo ya uchunguzi uliofanyika mwishoni mwa mwezi Julai nchini Marekani pia yameonesha kuwa, karibu asilimia 70 ya Wamarekani wanaona kuwa, Marekani itakabiliwa na mashambulizi makubwa ndani ya miaka mitano ijayo.
Lakini wachambuzi wanaona kuwa, wakati Iraq haijamaliza kazi ya kutunga mswada wa katiba, kikosi cha usalama cha Iraq hakijamudu kazi ya kulinda usalama na kupambana na watu wenye silaha, msimamo wa Bush kuhusu kuondoa jeshi lake kutoka Iraq hautabadilisha. Na Marekani na Uingereza hazitajali matakwa ya kundi la Al-Qaeda kuhusu kuondoa jeshi la muungano liondoke kutoka Iraq. hivyo ushindani kati ya nchi za magharibi na kundi la Al-Qaeda utaendelea kwa muda mrefu.
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-05
|