Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-09 21:09:18    
Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya CRI yataongezwa muda

cri

Kuanzia tarehe 1 Agosti mkurugenzi mkuu wa Shirika la utangazaji la Kenya KBC Bwana Wachira Waruru alifanya ziara hapa Beijing, China kwa wiki moja, ambapo alitembelea Kituo kuu cha televisheni cha China CCTV, Kampuni ya radio na televisheni ya China na Radio China kimataifa. Tarehe 4 asubuhi naibu mkuu wa Idara kuu ya radio, filamu na televisheni Bwana Dian Jin alikutana na Bwana Waruru, ambapo walizungumza kuhusu ushirikiano katika sekta za radio na televisheni.

 

Tarehe 4 alipotembelea Radio China kimataifa, manaibu wakurugenzi wakuu wa Radio China kimataifa Bwana Chen Minyi na Xia Juxuan walikutana naye, ambapo walibadilishana maoni kuhusu ushirikiano kati ya Radio China kimataifa na shirika la utangazaji la Kenya KBC, na wameahidi kupanua ushirikiano kati ya pande hizo mbili. Baadaye Naibu mkurugenzi mkuu wa Radio China kimataifa Bwana Xia Juxuan na Mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji la KBC walisaini makubaliano kuhusu kuongeza muda wa matangazo ya idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa kwa kupitia Radio KBC, kwamba kuanzia Tarehe 1, Septemba mwaka huu muda wa matangazo ya idhaa ya kiswahili na idhaa ya Kiingereza za Radio China kimataifa utakuwa wa saa moja.

Hii ni mara ya pili kwa Mkurugenzi mkuu wa KBC Bwana Wachira Waruru kufanya ziara nchini China, alisema amepata picha nzuri kuhusu Beijing, China. Alisema kuwa, mwaka 1988 aliwahi kuambatana na rais wa Kenya katika ziara yake nchini China, wakati ambapo alikuwa mwandishi wa habari. Hii ni mara yake ya pili kuja China, ameona mabadiliko makubwa yametokea nchini China, kiasi kwamba hawezi kuamini kuwa Beijing imekuwa na sura mpya namna hii.

Na kuhusu ushirikiano kati ya CRI na KBC, Bwana Waruru alifurahi akisema kuwa, Radio China kimataifa na shirika la utangazaji wa KBC zimepanua ushirikiano, safari hii matangazo ya idhaa ya kiswahili na idhaa ya Kiingereza ya Radio China kimataifa yameongezewa muda kuwa saa moja badala ya nusu saa, hili ni jambo la kufurahisha, kwani wanajua kuwa wasikilizaji wengi walikuwa na matarajio ya matangazo hayo kuongezewa muda.

Baada ya kuongezewa muda kwa matangazo ya idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa, vipindi vile vinavyopendwa zaidi na wasikilizaji wetu vitaongezewa muda, kama vile kipindi cha salamu zenu, na kipindi cha burudani za muziki na nyimbo. Bwana Waruru ametoa maoni yake juu ya vipindi vyetu akisema, anaona kuwa vipindi vya idhaa ya Kiswahili ya Radio China kimataifa vimepambwa vizuri, kuna habari nzuri za kimataifa, vipindi mbalimbali vinavyojulisha uchumi, utamaduni, historia na nyingine mbalimbali kuhusu China, baada ya kuongezewa muda kwa matangazo, vipindi mbalimbali vinaweza kuongezwa muda, kama kipindi cha salamu zenu, kikiongezwa muda, kitawafurahisha wasikilizaji wengi.

 

Wasikilizaji wapendwa, kuanzia Tarehe 1 Septemba muda wa matangazo yetu utaongezwa na kuwa saa moja, hali halisi kuhusu saa ya matangazo ya kila siku tutatangaza hivi karibuni, na mkiwa na maoni na mapendekezo juu ya vipindi vyetu tafadhali msisite kututumia barua ili mtusaidie kuboresha zaidi vipindi vyetu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-09