Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-10 14:36:28    
Nchi za Afrika zapoteza watu wengi wenye ujuzi

cri

Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na shirika la uhamiaji duniani zinaonesha kuwa, kila mwaka watu zaidi ya elfu 20 wenye ujuzi wa nchi za Afrika wanaondoka makwao, na kwenda kutafuta kazi kwenye nchi zilizoendelea za Ulaya na Marekani. Takwimu nyingine zilizotolewa na shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo duniani, ambalo makao makuu yake yako mjini Paris zinaonesha kuwa, watu zaidi ya milioni moja wenye shahada za vyuo vikuu kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanafanya kazi katika shirika hilo, na idadi hiyo inaongezeka siku hadi siku.

Takwimu zilizotolewa na shirika la afya duniani zinaonesha kuwa, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari, wakati huo huo asilimia 50 ya madaktari walioandaliwa na nchi hizo wamehamia nchi zilizoendelea, kiasi hicho kimefikia 68% nchini Zimbabwe.

Vyombo vya habari vya Cameroon hivi karibuni vilitoa habari kuwa, hivi sasa wachezaji 646 wa soka kutoka nchi 33 za Afrika wanachezea timu za mpira wa soka za Ulaya. Makadirio yaliyotolewa na idara husika yanaonesha kuwa, kutokana na wasomi wa Afrika kumiminikia nchi zilizoendelea, nchi mbalimbali za Afrika zinapaswa kuwaajiri wataalamu wa nchi za nje, mradi huo unazigharimu nchi za Afrika dola za kimarekani zaidi ya bilioni nne kwa mwaka.

Kuondoka kwa watu wengi wenye uwezo kumeathiri sana maendeleo ya uchumi na jamii barani Afrika, na kudhoofisha uwezo wao wa kustawisha uchumi. Kuna sababu nne zilizowafanya watu hao kuhamia ng'ambo, yaani umaskini na mgogoro wa kivita; mfumo mbaya; misharaha midogo; na hali duni ya kufanya utafiti wa kisayansi. Takwimu zinaonesha kuwa, fedha zilizotumiwa katika sekta ya sayansi na teknolojia barani Afrika zinachukua asilimia 0.3 tu ya jumla ya uzalishaji mali.

Suala la kuzuia watu wenye ujuzi wasiondoke Afrika kwa kweli ni suala la kuzingatia jinsi ya kulinda maslahi ya nchi dhaifu katika mchakato wa utandawazi. Utatuzi huo unahitaji juhudi za pamoja za jumuiya ya kimataifa, hasa nchi zilizoendelea. Serikali za nchi za Afrika pia zinatakiwa kuchukua hatua mwafaka kuweka hali ya kuwaheshimu watu wenye ujuzi, ili kuwashawishi watu wao waliosoma ng'ambo warudi nchini kwao na kutoa mchango wao ipasavyo.

Serikali ya China inafuatilia sana ushirikiano kati yake na Afrika katika sekta ya kuendeleza nguvukazi, ilianzisha mfuko wa maendeleo ya nguvukazi wa Afrika. Katika miaka ya karibuni, idara husika za China zimewaandaa wanataalamu elfu kadhaa wa nchi za Afrika katika sekta mbalimbali za diplomasia, usimamizi wa uchumi, kilimo, afya, elimu, sayansi na teknolojia, utamaduni na utoaji huduma, na kuwatuma wataalamu na walimu wa aina mbalimbali katika nchi za Afrika, ili kuzisaidia nchi za Afrika kuwaandaa wataalamu wa sekta za kilimo, elimu, mafunzo ya lugha ya Kichina, michezo ya sanaa, riadha na sarakasi, shughuli hizo zimesifiwa sana na serikali na watu wa Afrika.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-10