Chombo cha safari za anga ya cha Marekani kinachojulikana kwa jina la "Discovery", baada ya kumaliza safari yake kwenye anga ya juu kilirejea kwenye kituo cha jeshi la anga cha Edwards huko California mnamo saa 2 na dakika 11 kwa saa za sehemu ya mashariki ya Marekani. Vyombo vya habari vinaona kuwa kurejea salama kwa "Discovery" si kama tu kumepunguza wasiwasi wa shirika la safari za anga ya juu la Marekani (NASA) bali pia kumetia moyo utekelezaji wa mpango wa kurusha vyombo vya anga ya juu ambao watu wengi wamekuwa hawana imani nao.
Kutua salama kwa chombo cha "Discovery" kulikuwa na matatizo mengi kama ilivyo rushwa angani. Nafasi mbili za alfajiri na mapema ya tarehe 8 kurejea duniani zilizopangwa hapo awali hazikuweza kutumika kutokana na hali mbaya ya hewa. Alfajiri ya tarehe 9 "Discovery" iliyokuwa na mpango wa kutua kwenye kituo cha safari za anga ya juu cha Kennedy mnamo saa 11 na dakika 7 ilitua kwenye kituo cha jeshi la anga cha Edwards kwenye jimbo la California kutokana hali mbaya ya hewa. Habari zilisema kuwa chombo cha "Discovery" kiliruka kwa kiasi cha saa 1 katika hewa ya anga la dunia hatimaye ilitua kwa usalama. Katika mkutano uliofanyika wakati huo shirika la safari za anga ya juu la Marekani lilisema kuwa safari ya siku 14 ya "Discovery" imefanikiwa. Hiyo ni safari ya kwanza chombo cha anga ya juu kinachobeba binaadamu baada ya ile ya "Columbia" kuteketea kwenye ajali mwaka 2003.
Ni kama shirika la safari za anga ya juu ya Marekani lilivyosema "Discovery" imefanikiwa katika kutimiza majukumu yake yakiwa ni pamoja na kupeleka tani 2 za vitu vya mahitaji na zana za kazi, kuchukua tani kadhaa za takataka zilizotoka kwenye kituo cha angani, wana-anga walifanya shughuli mara tatu nje ya chombo na kukifanyia ukarabati chombo cha "Discovery". Wachambuzi wanasema kuwa mafanikio ya "Discovery" yametia moyo utakelezaji wa mpango wa kurusha vyombo vya anga ya juu.
Kwanza kabisa, kwa kiwango fulani imeimarisha imani ya watu kuhusu safari za anga ya juu. Tokea muda mrefu uliopita watu wa Marekani walikuwa na mashaka kuhusu usalama wa vyombo vya safari za anga ya juu, baadhi ya jumuiya na makundi ya watu vinakosoa mpango wa safari za vyombo vya kupeleka vyombo vya anga ya juu, kuwa ni kupoteza fedha za walipa kodi na nguvu-kazi na kutaka kudhibiti utekelezaji wa mpango huo. Mwaka 2003 chombo cha "Columbia" kilikumbwa na ajali, watu walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa kurejea kwa usalama kwa ndege za aina hiyo, baadhi ya wazazi nchini Marekani hawakuwaruhusu watoto wao kuangalia picha za televisheni kuhusu kurejea kwa chombo cha "Discovery", ili wasije wakapatwa tena na kutokana na ajali za ndege za aina hiyo. Hivyo kurejea kwa usalama kwa "Discovery" kumeonesha nguvu halisi ya Marekani katika mradi wa ndege za kubebea vyombo vya anga ya juu.
Pili kumeongeza sifa kwa shirika la safari za anga ya juu la Marekani na kuimarisha imani ya kuendeleza mpango wa safari za anga ya juu kwa binadamu. Marekani ilikuwa na wazo la kusimamisha utekelezaji wa mradi wa safari za anga ya juu kutokana na kuwa vyombo vya safari za anga ya juu vimechakaa vibaya na gharama ya ukarabati wake ni kubwa sana. Kwa kufuata mpango wa utafiti wa anga ya juu ya serikali ya Bush, vyombo vyote safari za anga ya juu vitaacha kutumika kabla ya mwaka 2010, badala yake vitatumika vyombo vya aina mpya. Lakini baadhi ya wataalamu wamelalamika kuwa vituo vya angani vya kimataifa vinahitaji vyombo vya aina hiyo, hususan katika muda wa kabla ya kutumika kwa vyombo vya aina mpya. Hivyo kurejea kwa usalama kwa "Discovery" huenda kutaanzisha kipindi kipya cha utafiti wa mambo ya anga ya juu.
Idhaa ya Kiswahili
|