Ujumbe wa ngazi wa mawaziri uliotumwa na Umoja wa Afrika tarehe 9 ulifika Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania kufanya mazungumzo na utawala wa kijeshi ulioshika hatamu za kiserikali baada ya uasi kuhusu kufufua utaratibu wa katiba wa Mauritania. Hii ni mara ya kwanza kwa ujumbe wa Umoja wa Afrika kuwasiliana na utawala huo.
Dalili mbalimbali zimeonesha kuwa misimamo ya watu nchini Mauritania na wa nje ya nchi hiyo juu ya utawala wa kijeshi wa Mauritania imeanza kubadilika.
Tarehe 3 mwezi huu wanajeshi wengi wa kikosi cha ulinzi wa rais wa Mauritania na idara ya usalama wa nchi wakichukua fursa ya kutokuwepo nchini humo kwa rais Taya, walifanya mapinduzi ya kijeshi kuupindua utawala wa Taya. Wakati huo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na jumuiya nyingine za kimataifa zililaani mapinduzi hayo ya kijeshi na kutaka katiba na utaratibu wa Mauritania urudishwe mara moja. Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika tarehe 4 lilitoa uamuzi maalum juu ya hatua hiyo, na kuisimamisha Mauritania uanachama kwa muda. Lakini siku 6 zilizopita baada ya mapinduzi hayo, Umoja wa Afrika umetuma ujumbe wake wa ngazi ya mawaziri huko Nouakchott kufanya mazungumzo na viongozi wa utawala wa kijeshi wa Mauritania. Tarehe 9 waziri wa mambo ya nje wa Libya Mohammed Abdel Shalgam pia alikuwa na mazungumzo na viongozi wa utawala wa kijeshi wa Mauritania. Habari zinasema kuwa, ujumbe mmoja wa Umoja wa nchi za kiarabu pia utafika Nouakchott hivi karibuni. Balozi wa Afrika ya kusini nchini Mauritania Bwana William Mokou tarehe 9 huko Nouakchott alipohojiwa na waandishi wa habari alisema kuwa, Umoja wa Afrika unapinga mapinduzi ya kijeshi, lakini msimamo huo si lazima unafaa kwa hali halisi ya kila nchi mwanachama wa Umoja wa Afrika.
Aidha, mazungumzo ya safari hii kati ya ujumbe wa ngazi ya mawaziri wa Umoja wa Afrika na viongozi wa utawala wa kijeshi wa Mauritania kwa kweli yameungwa mkono na kuitikiwa na Marekani na Umoja wa Afrika.
Baada ya kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini Mauritania, kaimu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani George Casey alieleza wazi kuwa, Marekani itafanya juhudi pamoja na Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na jumuiya nyingine za kikanda na kimataifa, ili kufufua mapema iwezekanavyo utaratibu wa katiba wa Mauritania na kufufua hadhi ya utawala ya rais Taya. Lakini baada ya kujulikana kwa habari kuhusu Umoja wa Ulaya kuamua kutuma ujumbe wa ngazi wa mawaziri kufanya mazungumzo na viongozi wa utawala wa kijeshi, wizara ya mambo ya nje ya Marekani tarehe 8 ilieleza bayana kuunga mkono ziara hiyo, na haitaji tena kufufua utawala wa Taya. Maofisa wa kidiplomasia wa Umoja wa Afrika walioko Nouakchott tarehe 9 pia walisema kuwa kama utawala wa kijeshi wa Mauritania utatimiza ahadi yake ya kufanya tena uchaguzi wa kidemokrasia ndani ya miaka miwili, basi jumuiya ya kimataifa huenda itaupokea utawala wa kijeshi wa Mauritania.
Zaidi ya hayo, hali ya nchini Mauritania pia inaendelea kwa mwelekeo wa kuusaidia utawala wa kijeshi. Kwa kuwa baada ya mapinduzi, utawala wa kijeshi ulidhibiti kwa haraka hali ya Nouakchott, na kuchukua hatua kadha wa kadha kuharakisha kuunda serikali ya mpito, na kutoa ahadi ya kufanya tena uchaguzi mkuu ndani ya miaka miwili na viongozi wa utawala wa kijeshi na waziri mkuu wa serikali ya mpito kutoruhusiwa kugombea kiti cha rais, wananchi wengi wa Mauritania wameunga mkono na kufurahia hayo. Na mabalozi wa nchi kadha wa kadha nchini Mauritania wameeleza kuwa, jumuiya ya kimataifa ingeheshimu nia na chaguo la wananchi wa Mauritania.
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-10
|