Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-11 21:17:56    
Tiba ya kichina-Uvumbuzi mkubwa wa tano katika China ya kale

cri

Mavumbuzi manne makubwa katika China ya kale yanajulikana kwa watu wengi. Ufundi wa kutengeneza karatasi ulivyovumbuliwa katika Enzi ya Han, baruti, dira na uchapaji wa mpangilio huru wa maneno vilivyovumbuliwa katika Enzi za Song na Yuan, vyote viliwahi kutoa mchango mkubwa kwa utamaduni wa binadamu na maendeleo ya jamii. Baada ya mavumbuzi matatu ya mwisho kuingizwa huko Ulaya katika karne ya 13 hadi karne ya 14, yalikuwa nguvu kubwa iliyosukuma mbele ustawi wa Ubepari.  Wataalamu wafilosofia, historia na siasa walio maarufu duniani waliwahi kutoa hoja wazi juu ya mchango huo.

Lakini mavumbuzi makubwa katika China ya kale si hayo manne tu. Tiba ya kichina ni uvumbuzi mkubwa zaidi kuliko mavumbuzi hayo, ambayo inaweza kuhesabika kuwa ni uvumbuzi mkubwa wa tano wa China.

Kwanza, tiba ya kichina iliyovumbuliwa na Wachina, ni mafanikio makubwa ya kisayansi katika China ya Kale, na mfano mzuri wa sayansi na teknolojia ya China ya kale

Pili, tiba ya kichina ilisambazwa duniani na kutumiwa na watu wengi. Thamani yake ya kisayansi na mchango wake mkubwa vimethibitishwa na madaktari duniani.

Tatu, tiba ya kichina imesukuma mbele utamaduni wa binadamu na maendeleo ya jamii, na imethibitishwa duniani kote kuwa utibabu wa kichina ni uvumbuzi mkubwa na una thamani mkubwa.

Tiba ya kichina ni tofauti na tiba ya nchi za magharibi katika mawazo, nadharia na njia ya kutibu, hivyo ina nguvu yake ya kipekee. Na imesukuma mbele maendeleo na mageuzi ya utibabu, na kutoa mchango wa kipekee kwa afya ya binadamu.

Na katika sekta ya maendeleo ya sayansi na utamaduni, nadharia ya tiba ya kichina kuhusu maisha ya binadamu yamesukuma mbele utafiti wa sayansi ya maisha, na utatoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya utamaduni wa binadamu. Madaktari na wanasayansi mashuhuri duniani walisema mara kwa mara kuwa, tiba ya kichina ina uwezekano mkubwa zaidi wa kuipatia China tuzo ya Nobel.

Mwanasayansi mashuhuri wa China Bw. Qian Xueseng aliwahi kusema kuwa, mambo ya kisasa ya tiba ya kichina yatasukuma mbele maendeleo ya sayansi ya binadamu, na kuleta mapinduzi ya sayansi na teknolojia, na ufufuaji wa utamaduni katika nchi za mashariki.

Tiba ya kichina ni pamoja na uvumbuzi wa kiteknolojia na ugunduzi wa kisayansi. Utengenezaji karatasi, baruti, dira na uchapaji wa mpangilio huru vyote ni ufundi tu, lakini tofauti na mavumbuzi hayo, Tiba ya kichina ni mfumo wa mavumbuzi kadhaa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-11