Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-11 18:48:57    
Makundi mbalimbali ya Iraq yafanya mazungumzo ya "marathon" juu ya mswada wa katiba

cri

Kuanzia tarehe 7, viongozi wa madhehebu ya Shia na ya Suni pamoja na kundi la vyama vya wakurd waliendelea na mkutano kujadili suala la katiba ya kudumu ili kuondoa migongano na kujitahidi kupata maoni ya pamoja juu ya mswada wa katiba. Lakini baada ya majadiliano ya "kimarathon" ya siku kadhaa, makundi hayo bado hayajaweza kuondoa migongano husika.

Usiku wa tarehe 9, viongozi wa makundi mbalimbali walijadili tena mswada wa katiba. Kwenye mkutano uliofanyika kwa saa 4, viongozi wa makundi mbalimbali walijadili hasa migongano mikubwa 18 kuhusu mfumo wa shirikisho, hadhi ya dini nchini humo, Iraq ya kiislamu au la, jina la nchi, lugha ya kiserikali, ugawaji wa mafuta na umiliki wa Kirkuk.

Hivi sasa mgongano mkubwa kati ya makundi mbalimbali bado ni kuhusu Iraq itafuata mfumo wa shirikisho au la katika siku za usoni. Wakurd wameshikilia kuandika kwenye katiba kuhusu mfumo wa shirikisho ili kuhakikisha wakurd wa kaskazini wanaendelea kupewa haki ya kujiendesha. Kiongozi wa chama cha demokrasia cha Kurdistan Bwana Mesud Barzani amesistiza mara kwa mara kuwa, suala kuhusu haki na maslahi ya kimsingi ya wakurd haliruhusiwi kujadiliwa tena na tena. Lakini balozi wa Marekani nchini Iraq tarehe 9 alidokeza kuwa, Bwana Barzani ameamua kuwa hataomba kuandika kifungu kwenye katiba kuhusu kuhakikisha haki ya kujiendesha ya kabila la wakurd.

Lakini watu wa madhehebu ya Suni siku zote wanapinga kutekeleza mfumo wa shirikisho, na wana wasiwasi kuwa wakurd watatumia fursa hiyo kufarakanisha Iraq. Mjumbe wa madhehebu ya Suni katika kamati ya utungaji wa mswada ya Iraq Bwana Saleh Mutlaq tarehe 9 alionya kuwa, katika mazingira ya hivi sasa, madhehebu ya Suni hayawezi kupokea mfumo wa shirikisho, kama ombi la wakurd litakidhiwa, Iraq itakabiliwa na matokeo mengi mabaya katika siku za usoni. Na ameshauri kuliacha bunge litakalochaguliwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Desemba liamue kama Iraq itafuata mfumo wa shirikisho au la.

Kuhusu suala la hadhi ya dini ya kiislamu, kuna migongano ya bila kusita kati ya makundi mbalimbali kuhusu sheria ya dini ya kiislamu kuwa chanzo kikuu au chanzo kimoja cha utungaji wa katiba. Wakati huo huo jumuiya moja inayotetea haki za wanawake ya Iraq tarehe 9 ilitoa taarifa ikidai katiba mpya ihakikishe watu wote wa jamii ya Iraq wanakuwa na haki za binadamu bila kujaili tofauti za kijinsia, makabila, madhehebu, na dini.

Rais Jalal Talabani wa Iraq alisema kuwa, baada ya mkutano wa 9 wa viongozi wa makundi mbalimbali, hautafanyika tena mkutano rasmi, bali viongozi wa makundi mbalimbali watakutana faraghani. Tarehe 10 viongozi wa makundi mbalimbali ya Iraq wameanza kufanya mawasiliano faraghani, ili kutatua mapema iwezekanavyo masuala ambayo ni vigumu kutatuliwa.

Aidha, ili kuzuia mchakato wa utungaji wa katiba ya Iraq, vikosi vinavyoipinga Marekani na serikali vya Iraq hivi karibuni vimeanzisha mashambulizi makali zaidi dhidi ya jeshi la Marekani na shabaha ya jeshi la Iraq.

Hivi sasa bado kuna muda wa chini ya wiki moja hadi kutolewa kwa mswada wa katiba kwa mpango uliowekwa, lakini kuna matumaini madogo sana kwa kufikia makubaliano kati ya makundi mbalimbali. Hii imeifanya Marekani iwe na wasiwasi mkubwa. Naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bwana Adam Ereli tarehe 10 alisema kuwa, mchakato wa utungaji wa katiba ya Iraq unaendelea kufanyika kwa mpango uliowekwa, na balozi wa Marekani nchini Iraq Zalmay Khalilzad siku zote anajitahidi kujadiliana na makundi mbalimbali na kutoa maoni ya Marekani juu ya mchakato huo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-11