Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-12 21:06:53    
Utamaduni na sanaa nchini China 2

cri

Katika miaka 20 iliyopita tangu yafanywe mageuzi na ufunguaji mlango wazi kwa nje, sanaa ya sarakasi ya China ilipata mafanikio katika mashindano makubwa ya kimataifa, ustadi wa kijadi wa michezo mingi imepata kuinuliwa zaidi na kuwavuta sana watu macho.

Watangulizi wa China walivumbua mafanikio ya miziki iliyowashangaza watu katika zama za kale sana. Katika miaka 20 iliyopita, wanamuziki walifanya kazi nyingi katika kukusanya na kutengeneza upya miziki ya kale ya kichina na kuifanya iwaburudishe wasikilizaji.

Baada ya kujifunza umaalum wa upigaji muziki wa nchi za magharibi, aina mbalimbali za upigaji wa muziki zimeiongezea miziki mingi maarufu ya kichina mvuto wa kuwaburudisha watu.

Sanaa ya uchoraji ya China pia ilianzia tangu enzi na dahari. Mapema ya miaka 2,200 iliyopita, michoro iliyochorwa kwa kutumia kalamu ya burashi, karatasi maarufu ya Xiuan , wino nyeusi na rangi nyingine iliendelezwa kuwa uchoraji wa kitaifa wa China siku hadi siku, uchoraji huo ambao ni kama vielelezo vya mafanikio makubwa kabisa ya sanaa ya uchoraji wa kijadi ya China. Michoro fulani ilionyesha jinsi wachoraji walivyotumia wino nzito au nyepesi kwa kueleza tafsiri zao juu ya milima na mito au biinadamu, michoro mingine ilichorwa kwa makini sana, hata nywele za watu, manyoya ya ndege, kila kitu kilichorwa vilivyo kwa utaratibu kamili. Tangu China mpya ianzishwe, wachoraji wengi walijitahidi kupatanisha uchoraji wa kichina na uchoraji wa nchi za magharibi ili kuvumbua michora mbalimbali ya aina mpya.

Fasihi ya China ya hivi leo imeingia katika zama mpya kabisa, usitawi usiotokea hapo kabla umeonekana katika utungaji wa fasihi na utoaji wa tuzo mbalimali umehimiza utungaji wa fasihi nzuri.

Hadithi ndefu kama vile "Li Zichen", "Umbo wa kibinadamu unaobadilikabadilika", "Meli ya kale", "Mbuga wa paa mweupe", "Vita na binadamu" zilisifiwa na kupendwa na wasomaji wengi.

Utamaduni na sanaa za China ziliposhikilia mtindo wa kichina huku zikijitahidi kupokea matunda yote ya utamaduni yenye manufaa, ikawa aina za utamaduni na sanaa za China zimeongezeka.

Mchezo wa kuigiza uliletwa China kutoka nchi za nje mwanzoni mwa karne hii, wasanii wa mchezo huo walitafuta njia ya kuufanya uambatane na jamii ya kichina . Michezo iitwao "Mkahawa wa chai", "Bonde la ndevu la dragon" ndiyo vielelezo ambavyo vilifuatilia hatua za zama tulizo nazo na kuonyesha hali halisi ya maisha ya wachina, tena vilijitoa kutoka aina ile ile ya mchezo wa kuigiza wa nchi za magharibi na kufuatilia hatua kwa hatua desturi na tabia za wachina.

Katika miaka kadha ililyopita michezo mizuri ya kuigiza kama vile 'Mzee Gou ", "Jumba la kwanza duniani", "Cai Wenji", "Wang Zhaojun", "Mjumba wa Beijing" yote ilionyesha umaalum dhahiri wa kienyeji na kuvuta sana watu macho .

Filamu ya "Mwangaza wa ncha" ikitumia mbinu ya sayansi na teknolojia ya kisasa iliwafanya watazamaji wajione kama wako ncha ya kusini yenye hali pekee ya kijiografia.

Filamu za China zilianza kutengenezwa mwanzoni mwa karne hii, katika miaka 50 hivi ililyopita, filamu nyingi nzuri zilitolewa , sanaa hiyo imeenea nchini kote China.

Hivi sasa kila mwaka filamu 200 hivi za aina mbalimbali hutolewa nchini China, nchini humo kuna idara laki 1.2 za kuonyesha filamu , na filamu nyingi za kichina zilipewa tuzo au kusifiwa ulimwenguni.

Kuanzia zama za miaka ya 80, filamu za "Hadithi za zamani za kusini mwa mji", "Mtama mwekundu", "Qiuju amshitaki mkuu wa kijiji", "Dada Xianghun", na kadhalika zilipewa tuzo katika tamasha kubwa za filamu za kimataifa, ambapo waongozi na wachezaji maarufu wa China wakaanza kufahamishwa na watazamaji wa nchi za nje.

Zaidi ya hayo, wanafilamu wa China wanafanya majaribio yasiyolegea ili kufuatilia ukuaji wa sayansi na teknolojia za hali ya juu katika utengenezaji wa filamu..

Michezo kadha maarufu ya opera ya nchi za magharibi huonyeshwa mara kwa mara nchini China.

Wasanii wa China walipopokea opera hiyo, walitafuta njia ya kuunganisha opera hiyo na michezo ya kichina, wakatunga michezo ya opera mpya ya kichina kama vile "Kikosi cha ulinzi cha ziwa Hunghu", "Matumbawe mekundu" "Msichana mwenye nywele nyeupe", "Dada Jiang" na mingineyo .

Tokea zama za miaka ya 90, michezo mizuri zaidi ya opera ya kichina kama vile: "Zhang Qian", "Makopolo", Mbuga mkubwa" imesifiwa zaidi na watu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-12