Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-12 21:34:09    
Dar es Salaam-Matatizo ya kinywa na meno huambatana na ugonjwa Ukimwi- TDA

cri

Utafiti uliofanyika mkoani Dar es Salaam umebaini kuwa matatizo ya kinywa na meno ni miongoni mwa dalili za kwanza za Ukimwi, hivyo watu wenye matatizo ya mara kwa mara ya aina hiyo hawana budi wapatiwe ushauri wa wataalam.

Matokeo ya utafiti huo yametolewa jijini Dar es Salaam jana na chama cha madaktari wa taaluma ya afya ya kinywa na meno Tanzania- TDA, wakati wa mkutano wa wadau wanaoshughulikia mapambano dhidi ya Ukimwi, uliofadhiliwa na tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi- TACAIDS.