Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-16 15:41:55    
Tangazo 0816

cri

Leo kwanza tunapenda kuwaarifu kuwa, shindano la chemsha bongo linaloandaliwa kila mwaka na Radio China kimataifa litaanzishwa hivi karibuni, shindano hilo la chemsha bongo mwaka huu ni kuhusu ujuzi wa "Taiwan?kisiwa cha hazina cha China", Idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa itatangaza makala 4 za shindano hilo la chemsha bongo kuanzia Tarehe 4 Septemba.

Taiwan ni kisiwa kimoja cha China, lakini kutokana na sababu za vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyofanyika nchini China katika miaka ya 40 ya karne iliyopita, Taiwan na China bara zimekaa katika hali ya uadui kwa kiasi fulani katika zaidi ya miaka 50 iliyopita, hivyo likatokea ati suala la Taiwan. Basi Taiwan ni kisiwa cha namna gani? Kwa nini tunasema Taiwan ni sehemu moja ya ardhi ya China? Serikali ya China ina sera gani ya kimsingi katika kutatua suala la Taiwan? Serikali ya China imefanya juhudi gani kwa kuhimiza muungano wa Taiwan na China bara? Hali ya biashara kati ya Taiwan na China bara ikoje? Kuna uhusiano gani kati ya watu wa Taiwan na wa China bara katika utamaduni wa jadi? Ili kuwawezesha wasikilizaji wa nchi mbalimbali waelewe kimsingi juu ya masuala hayo, Radio China kimataifa itatangaza makala za chemsha bongo kuhusu "Taiwan?kisiwa cha hazina cha China". Tunawakaribisha wasikilizaji wetu washiriki katika shindano hilo la chemsha bongo.

Kama tulivyofanya katika mashindano ya chemsha bongo yaliyopita, kila baada ya kusoma makala moja, tutaweza kutoa maswali mawili, ili wasikilizaji wetu wajibu, baada ya kupokea majibu, kamati ya uchaguzi ya Radio China kimataifa itachagua wasikilizaji watakaopewa tuzo ya nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu pamoja na washindi watakaopewa tuzo maalum watapata fursa ya kutembelea China bara kwa wiki moja mwakani.

Tunatumai kuwa wasikilizaji wetu watashiriki kwenye shindano hilo la chemsha bongo, tutaanza kuwatumia barua hivi karibuni.

Na kuanzia tarehe 1 Septemba mwaka huu, muda wa matangazo yetu ya kupitia Shirika la utangazaji la KBC utaongezewa kuwa saa moja badala ya nusu saa ya siku zilizopita, na saa za matangazo hayo yatabadilika kuanza saa 9 hadi saa 10 jioni kwa saa za Kenya. Wakati huo huo, matangazo yetu kwenye masafa mafupi pia yataongezwa muda kuwa saa moja badala ya nusu saa. Matangazo kwenye masafa mafupi yataanzia saa moja hadi saa mbili na marudio yake yataanzia saa mbili hadi saa tatu kwa saa za Afrika mashariki. Kutokana na muda utakaoongezwa, kutakuwa na baadhi ya mabadiliko katika vipindi vyetu, vipindi vinavyopendwa na wasikilizaji wetu vitaongezwa muda, kama vile kipindi cha salamu zenu na vinginevyo. Na kutokana na maandalizi yasiyo ya kutosha, huenda mwanzoni hakutakuwa na mabadiliko makubwa, lakini kadiri siku zinavyokwenda tutapanga vizuri zaidi na kuvifanya vipindi vipendeze zaidi. Tunawakaribisha wasikilizaji wetu mtoe maoni na mapendekezo yenu.

 

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-16