Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-17 21:13:54    
China yazingatia kufanya utafiti kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini

cri
China ilianza kufanya utafiti wa kisayansi kwenye sehemu ya ncha za dunia, hasa sehemu ya ncha ya kusini tokea miaka ya 80 ya karne iliyopita Lakini katika miaka ya hivi karibuni, utafiti kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini pia umeanza kuzingatiwa. Kabla ya miaka ya 90 karne ya 20, kutokana na kuwepo kwa vita baridi, ilikuwa ni vigumu kwa China ambayo ni nchi isiyopakana na ncha ya kaskazini kuingia kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini kufanya utafiti wa kisayansi. China ilianza kufanya utafiti kwenye ncha za dunia baada ya kukomeshwa kwa vita baridi. Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti kwenye sehemu ya ncha za dunia katika idara ya bahari ya taifa ya China Bw. Qu Tanzhou alieleza:

"Sehemu ya ncha ya kaskazini ikiwa ni ncha yenye baridi, mchakato wa mabadiliko kwenye sehemu hiyo utaathiri vipi shughuli za jamii ya binadamu, na vipi shughuli za binadamu zitaathiri sehemu hiyo, ni masuala yanayofuatiliwa sana kote duniani. China ikiwa ni nchi kubwa katika kisio cha kaskazini, inaathiriwa moja kwa moja na mabadiliko ya hali ya hewa kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini. Kwa hivyo, tunazingatia zaidi mchakato wa mabadiliko ya hali ya hewa kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini. Hivi sasa hilo ni eneo la utafiti linalofuatiliwa na kuzingatiwa zaidi duniani."

Mwaka 1999 na mwaka 2003, China ilifanya utafiti wa kisayansi mara mbili kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini. meli ya utafiti wa kisanyasi "Xue Long" ikiwa ilikuwa ni chombo muhimu katika utafiti huo, ilifanya utafiti wa jumla wa taaluma nyingi kwenye maeneo mbalimbali ya bahari ya Arctic na kupata data na sampuli nyingi muhimu, zikiwemo sampuli ya masalio ya kimaumbile kwenye sehemu ya chini ya bahari hiyo yenye kina cha mita 3000 na data za utafiti wa anga yenye urefu wa mita 3100. aidha, wanasayansi wa China pia waligundua kuwa kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini tabaka la chini la anga (troposphere) kwenye sehemu hiyo liko juu zaidi kuliko sehemu nyingine duniani, na ugunduzi huo una umuhimu mkubwa kwa utafiti wa mabadiliko ya majira na hali ya hewa nchini China.

Kutokana na kutumia meli, China haikuweza kuendelea na utafiti kama huo kwa muda mrefu. Hivyo ili kuimarisha utafiti wa ncha ya kaskazini ya dunia, China ilijenga kituo cha utafiti kwenye sehemu hiyo mwaka 2004. Bw. Li Chunxian aliyeshiriki kwenye ujenzi wa kituo hicho alisema,

"China ilijenga kituo cha utafiti wa kisayansi wa ncha ya kaskazini huko Ny-Alesund kwenye visiwa vya Spitsbergen nchini Norway, na kuanza utafiti wa jumla wa taalamu nyingi za fizikia ya dunia, elimu ya hewa, maelezo ya hali ya ardhi, jiografia na elimu ya bahari, na kupata data na sampuli nyingi. Kazi hiyo imeweka msingi imara kwa utafiti wa muda mrefu wa ncha ya kaskazini."

Kituo hicho kinawawezesha wanasayansi wa China wafanye utafiti kwa muda mrefu kwenye sehemu hiyo. Katika muda wa mwaka mmoja tu baada ya kujengwa kwa kituo hicho, wanasayansi 10 hodari wa China walifanya utafiti mara 10 kwenye kituo hicho, na mafanikio yamepatikana katika baadhi ya miradi hiyo. Mwanasayansi mkuu wa kituo hicho Prof. Yang Huigen alieleza kuwa wanasayansi wa China wamegundua athari zinazotolewa na shughuli za binadamu kwenye baadhi ya sehemu za ncha ya kaskazini. Alisema:

"mahali kilipo kituo hicho palikuwa ni kampuni moja ya uchimbaji wa makaa ya mawe, na kampuni hiyo iliendelea na shughuli ya uchimbaji hadi kwenye miaka ya 60 karne iliyopita. Wanasayansi wetu walichunguza athari zilizotolewa na shughuli ya uchimbaji kwa mabadiliko ya kiikolojia ya dunia kwa njia ya kibiolojia na kikemikali na fikizia ya dunia. Matokea yanaonesha kuwa, katika karne moja iliyopita, kutokana na uchimbaji na shughuli nyingine za binadamu kwenye sehemu hiyo, idadi ya ndege wa baharini ilipungua kwa kiasi kikubwa."

Aidha, wanasayansi wa China pia walichunguza hali ya mazingira ya hewa kwenye anga ya juu katika sehemu ya ncha ya kaskazini kwa kutumia zana za mwangaza wa Laser, na kupata data za utafiti huo kwa zaidi ya saa 1000. hiyo imepanua kabisa eneo la utafiti wa elimu ya fizikia ya hewa ya juu kwenye sehemu hiyo.

Wataalamu walieleza kuwa, katika siku za baadaye, China ina malengo mawili ya utafiti kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini katika siku za baadaye, kwanza ni kufahamu utaratibu wa athiri za sehemu hiyo kutokana na mabadiliko duniani, na kuanzisha kwa hatua ya mwanzo mfumo wa utafiti wa bahari na hali ya hewa kwenye sehemu ya bahari ya Arctic; pili ni kufahamu athari za mabadiliko kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini kwa mazingira ya hali ya hewa ya China.

Ili kuimarisha zaidi shughuli za utafiti kwenye sehemu hiyo, China itaweka mkazo katika kuboresha hali ya kituo cha utafiti, kupeleka zana nyingi zaidi, zikiwemo magari ya Jeep, pikipiki maalum za kusafiri juu ya barafu na mashua ya raba, na kuboresha zaidi hali ya maisha, ofisi na mawasiliano kwenye kituo hicho.

Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa ncha za dunia katika idara ya bahari ya China Bw. Qu Tangzhou alisema kuwa, kutokana na kukamilika kwa hali ya utafiti kwenye kituo hicho, China itaanza kufanya utafiti wa muda mrefu kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia. Alisema kuwa,

"Hivi sasa kwa kutegemea meli ya utafiti ya "Xue Long" na kituo cha utafiti cha Mto Manjaro, utafiti wa kisayansi kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia umeendelea hatua kwa hatua, na kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wetu wa uchungzi kwenye sehemu hiyo. Katika siku za baadaye, mbali na utafiti kwenye kituo, China itaendelea kupeleka meli kufanya utafiti kwenye sehemu ya bahari ya Arctic, na pia kuweka mkazo katika ushirikiano wa kimataifa, na kuinua kiwango cha utafiti wetu."

Alisema kuwa, kuanzia mwaka huo, China itapeleka meli ya utafiti wa Xue Long kwenye sehemu hiyo kila mwaka. Hivi karibuni, shughuli za utafiti wa kisayansi kwenye sehemu ya ncha ya kaskazini za mwaka 2005 zimeanza hivi karibuni, wanasayansi 21 watafanya utafiti kuhusu bahari, barafu baharini, mabadiliko ya mzunguko wa mawimbi baharini, mazingira ya anga na mstakabali na matumizi ya raslimali za sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-17