Mkutano wa mwaka wa wakuu wa Umoja wa maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC umefunguliwa tarehe 17 huko Gaborone, mji mkuu wa Botswana. Marais na wakuu wa serikali kutoka nchi wanachama wa SADC wamehudhuria mkutano huo wa siku mbili, ambapo wanajadili mikakati mikubwa ya maendeleo ya sehemu ya kusini mwa Afrika.
Huu ni mwaka wa 25 tangu kuanzishwa kwa SADC, mkutano huo wa wakuu umetiliwa maanani sana na nchi wanachama wa jumuiya hiyo. Kwenye mkutano huo, wakuu hao watathibitisha ripoti kuhusu hali ya siasa, uchumi na jamii ya sehemu ya jumuiya hiyo; kujadili masuala kuhusu usawa wa kijinsia, usalama wa chakula, mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi na kuipokea Madagascar kuwa nchi mwanachama rasmi wa jumuiya hiyo. Mkutano huo pia utatoa taarifa kuhusu matokeo ya mkutano huo.
Suala la usawa wa kijinsia siku zote ni mada kuu kwenye mkutano wa jumuiya ya SADIC. Mwaka 1997, nchi mbalimbali wanachama wa SADIC zilitoa taarifa kuhusu usawa wa kijinsia, ikiahidi kutimiza lengo la kuongeza idadi ya wanawake wenye madaraka kwa asilimia 30 ya idadi ya jumla ya watu wenye madaraka. Lakini hali halisi ya hivi sasa ni kuwa, idadi ya wanawake wenye madaraka ni ndogo sana. Kati ya nchi 13 wanachama wa SADC, hivi sasa katika nchi mbili tu za Afrika ya kusini na Msumbiji idadi ya wabunge wanawake imefikia asilimia 30 ya idadi ya jumla ya wabunge. Kutokana na hali hiyo, mkutano wa Baraza la mawaziri la SADC uliofungwa tarehe 16 umetoa pendekezo la kuongeza idadi hiyo kuwa ya asilimia 50 ili kulingana na lengo la usawa wa kijinsia lililothibitishwa na Umoja wa Afrika. Mkutano wa Baraza la mawaziri pia ulipendekeza mkutano wa wakuu uzingatie kuinua "Taarifa ya SADC kuhusu usawa wa kijinsia na maendeleo" kuwa "Makubaliano ya SADC kuhusu usawa wa kijinsia na maendeleo" yenye nguvu kubwa zaidi ya uzuizi kwa nchi wanachama, ili kuzihimiza nchi wanachama zitilie maanani suala la usawa wa kijinsia.
Mkutano huo wa wakuu pia utasaini "Makubaliano ya kurahisisha kuingia na kutoka kwa watu wa nchi wanachama wa SADC" makubaliano hayo ni muhimu. Kutimiza maendeleo endelevu ya uchumi wa sehemu hiyo, kuondoa umaskini na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi ni malengo ya SADC. Ili kutimiza malengo hayo, jumuiya ya SADIC inatakiwa kuondoa vikwazo vya kuzuia mzunguko wa fedha, watu na bidhaa katika sehemu hiyo. "Makubaliano ya kurahisisha kuingia na kutoka kwa watu wa nchi wanachama wa SADC" yana lengo la kuwapa raia wa nchi za sehemu hiyo urahisi wa kuingia na kutoka nchi za sehemu hiyo, ili kusukuma mbele kutimiza utandawazi wa sehemu hiyo.
Aidha mkutano huo wa wakuu utajadili kuipokea Madagascar kuwa nchi mwanachama wa 14 wa SADC. Na kwenye mkutano huo, Botswana imekuwa nchi mwenyekiti wa SADC badala ya Mauritius. Tarehe 17 mwenyekiti mpya wa jumuiya ya SADC ambaye pia ni rais wa Botswana Festus Mogae ataweka jiwe la msingi la makao makuu mapya ya SADC yanayotazamiwa kujengwa huko Gaborone.
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-17
|