Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-18 15:53:46    
Mchakato wa kisiasa wa Iraq wazuiliwa na mashambulizi makali

cri

Mashambulizi makali yameongezeka hivi karibuni nchini Iraq. Tarehe 17, Matukio ya kuwashambulia raia yalitokea mjini Baghdad, Iraq. Jambo hilo linaonesha kuwa mchakato wa kisiasa na hali ya usalama vinaathiriana na hali ya huko bado ni ya hatari.

Habari zinasema kuwa matukio ya milipuko mitatu ya kujiua yalitokea siku hiyo mjini Baghdad. Milipuko miwili ilitokea kwenye kituo cha basi, katikati ya Baghdad. Baada ya dakika 30, mlipuko wa tatu ulitokea kwenye hospitali iliyo karibu na kituo hicho. Milipuko hiyo ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 43.

Kituo cha televisheni cha serikali ya Iraq kilitangaza kuwa serikali hiyo iliwakamata watuhumiwa wanne waliohusika na milipuko hiyo. Msemaji wa serikali ya mpito ya Iraq Bw. Laith Kuba alitangaza kuwa milipuko hiyo ilifanywa na watu wa utawala wa zamani, madhumuni yao ni kutikisa imani ya Wairaq kwa mchakato wa kisiasa na kujaribu kuzusha machafuko na kuipindua serikali ya sasa.

Tarehe 17, milipuko mingine pia ilitokea kwenye sehemu mbalimbali nchini humo. Jeshi la Marekani lililoko nchini Iraq siku hiyo lilitoa taarifa likithibitisha kuwa askari wake watano waliuawa katika saa 48 zilizopita.

Ni dhahiri kuwa mashambulizi hayo makali yaliyotokea hivi karibuni nchini Iraq yanahusiana na mchakato wa kutunga mswada wa katiba ya Iraq. Tarehe 15, tarehe ya mwisho ya kutolewa kwa mswada wa katiba rasmi ilipofika, makundi mbalimbali ya kisiasa ya Iraq bado yalikuwa na mgongano kwenye baadhi ya vifungu vya mswada huo na kulazimisha bunge la umma la mpito liongeze muda wa siku ya kutokewa kwa mswada wa katiba hiyo.

Shirika la habari la AP lilieleza kuwa chama cha kiislam cha Iraq cha madhehebu ya Suni, ambacho ni chama kikubwa kabisa nchini Iraq, tarehe 17 kilitoa taarifa kikiikosoa tume ya utungaji wa mswada wa katiba ya Iraq na kusema kuwa tume hiyo ina mambo inayopendelea. Taarifa hiyo inasema kuwa chama cha kiislam cha Iraq kina maoni tofauti kuhusu vifungu vingi vya mswada huo. Chama hicho kinaona kuwa mfumo wa shirikisho la Iraq unafaa tu kwenye sehemu ya utawala wa Kurd, kaskazini mwa Iraq na haufai kwenye sehemu nyingine nchini humo. Zaidi ya hayo, katiba mpya ingethibitisha Iraq iwe nchi ya kiarabu na kiislam. Taarifa hiyo pia inasema kuwa raslimali za Iraq zingemilikiwa na umma.

Wachambuzi walianisha kuwa kwa kukabiliwa na kuathiriana vibaya kati ya mchakato wa ukarabati wa kisiasa wa Iraq na hali ya usalama, kukamilisha kazi ya utungaji wa mswada wa katiba mapema iwezekanavyo ni jambo muhimu sana kwa kutuliza hali ya Iraq na kukamilisha ukarabati wa kisiasa. Kwa hiyo, makundi mbalimbali ya Iraq yanapaswa kuweka kando maoni tofauti na kufikia makubaliano kwenye mswada wa katiba.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-18