Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-18 20:34:31    
Milipuko mfululizo yatokea nchini Bangladesh

cri

Milipuko mfululizo ya mabomu zaidi ya 300 ya mabomu ilitokea ndani ya saa moja tarehe 17 huko Dacca na wilaya 58 katika wilaya zote 64 nchini Bangladesh, na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 130 kujeruhiwa. Waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Khaleda Zia ambaye yuko ziarani nchini China alilaani vikali kuwa waliozusha milipuko hiyo ni 'maadui wa nchi nzima, taifa zima na amani, ubinadamu na demokrasia'.

Habari kutoka nchini humo zinasema kuwa, milipuko hiyo ilitokea kati ya saa 4 na nusu na saa 5 na nusu kwa saa za huko. Katika mji wa Dacca, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zia, klabu ya waandishi wa habari wa nchi hiyo, mahakama kuu, chuo kikuu cha Dacca na sehemu nyingine nyingi zilishambuliwa kwa mabomu. Milipuko mingine 15 iliripotiwa huko Chittagong sehemu ya kusini magharibi ya nchi hiyo. Kwa ujumla mabomu 350 ya kutegewa kwa wakati yalilipuka mfululizo kote nchini Bangladesh na kikosi cha usalama pia kiligundua mabomu mengi ambayo hayakulipuka. Tukio hilo adimu la milipuko lilisababisha vifo vya watu wawili, mmoja kati ya hao ni mtoto wa kiume wenye umri wa miaka 10 hivi na mwengine ni mwanamume mzima. Hivi sasa polisi wa Bangladesh wamewakamata watuhumiwa 45, wakiwemo mwanamume mmoja amabaye mkono wake ulijeruhiwa katika mlipuko, na wa-Bangladesh watatu walioshukiwa kuwa na vitu vya baruti.

Polisi wa nchi hiyo pia waligundua vipeperushi vyenye maneno ya "Jamayetul Mujahideen" kwenye sehemu ilipotokea milipuko. "Jamayetul Mujahideen" ni kundi la kiislam lenye msimamo mkali nchini Bangladesh. Mwezi Februari mwaka huu, kundi hilo lilipigwa marufuku na serikali ya nchi hiyo kutokana na kushukiwa kuwa lilishiriki mara nyingi kwenye mashambulizi ya milipuko dhidi ya jumuiya zisizo za kiserikali na sehemu takatifu za kidini. Ingawa hivi sasa bado hakuna ushahidi dhahiri wa kuthibitisha kuwa kundi hilo linahusika na milipuko hiyo, lakini taarifa moja iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imesema kuwa, kundi hilo linatiliwa mashaka makubwa kabisa, na polisi wameanza kulichunguza kundi hilo.

Bangladesh ni nchi ya tatu ya kiislam kwa ukubwa duniani, asilimia 90 ya wananchi wa nchi hiyo wanaamini dini ya kiislam. Ingawa hivyo, nchi hiyo imeendelea kutekeleza sera ya kutengenisha siasa na dini tangu ijipatie uhuru, na kundi la Jamayetul Mujahideen lilikuwa limeendelea kupinga sera hiyo. vipeperushi vilivyogunduliwa vinataka nchi hiyo ikomeshe siasa ya kawaida, na kutekeleza kanuni kali za kiislam, ambazo zinaagiza kuwa wanawake lazima wavae barakoa usoni na wanaume lazima wafuge ndevu.

Waziri wa mambo ya ndani ya Bangladesh Bw. Lutfozzaman Babor alisema kuwa, "milipuko hiyo ilipangwa kwa makini, na wala si tukio la upweke." Habari kutoka polisi wa nchi hiyo zinasema kuwa, mabomu ya milipuko hiyo yote ni zana rahisi za baruti zenye nguvu ndogo zilizotengenezwa nyumbani. Lengo la milipuko hiyo ni kufanya vurugu na ghasia nchini humo. Bw. Babor alisema kuwa, nchi hiyo imeinua kiwango cha tahadhari mara baada ya kutokea kwa milipuko hiyo, na serikali imesambaza vikosi vya usalama kote nchini, na kuweka vituo vingi vya ukaguzi kwenye sehemu mbalimbali.

Baada ya kutokea kwa milipuko hiyo, jumuiya ya kimataifa imelaani tukio hilo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan siku hiyo alitoa taarifa, akionesha kukasirishwa na tukio hilo la kimabavu lililosababisha vifo na majeruhi wengi wa raia wa kawaida, na kusema kuwa, hiki na kitendo cha woga na cha kuaibisha na kutaka nchi hiyo iwkamate na kuwaadhibu kisheria wahusika wa tukio hilo haraka iwezekanavyo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-18