Kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ilitoa taarifa tarehe 18 mjini Geneva ilisema kuwa, chama cha Polisalio siku hiyo iliwaachia huru mateka 404 wa mwisho wa Morocco. Hadi hapo, suala la kuwachia huru mateka wa Morocco kwa chama cha Polisalio limekwisha, na kuleta matumaini kwa ufumbuzi wa suala la Sahara Magharibi lililodumu kwa miongo kadhaa.
Suala la Sahara Magharibi limekuwa kikwazo kikuu katika uhusiano kati ya Morocco na Algeria na kuufanya Umoja wa Maghreb wa nchi tano za Afrika Kaskazini uwe katika hali ya kutofanya kazi. Umoja wa Maghreb ulioundwa mwaka 1989 ulitafuta kutimiza umoja wa uchumi na muungano wa sehemu hiyo. Lakini tangu mwaka 1995, tofauti kubwa zilitokea kati ya Morocco na Algeria katika suala la Sahara Magharibi, Umoja wa Maghreb haukufanya kazi. Mkutano wa wakuu wa umoja huo uliopangwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu umeahirishwa kutokana na Algeria kusisitiza kukiunga mkono chama cha Polisalio na kusababisha malalamiko makubwa kutoka kwa Morocco.
Chama cha Polisalio kilichopigania uhuru wa Sahara Magharibi kimewateka Wamorocco wapatao elfu 2 katika vita vilivyodumu kwa miaka mingi. Kuanzia mwaka 1987, chama hicho kiliwaachia huru mateka hao kwa vipindi. Chama hicho kilieleza kuwa kuwaachia huru mateka wote wa Morocco kwa safari hii ni kueleza uungaji mkono kwa Umoja wa Mataifa kutatua suala la Sahara Magharibi. Msemaji wa chama hicho katika Umoja wa Ulaya Bw. Mohammed Sidati alieleza matumaini ya chama hicho kuwa, kitendo cha kuwaachia huru mateka kitasaidia kumaliza uchungu wa watu wa Sahara Magharibi na kutatua mgogoro wa sehemu hiyo kwa njia ya kudumu."
Taarifa ya kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu inasema kuwa chama cha Polisalio kiliamua kuwachia huru kikundi cha mwisho cha mateka wa Morocco kutokana na kusuluhishwa na Marekani. Mwenyekiti wa kamati ya uhusiano na nje ya baraza la juu la bunge la Marekani Bw. Richard Lugar alikutana na rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria kuhusu ushirikiano wa kupambana na ugaidi kati ya Marekani na Algeria na suala la mateka wa Morocco tarehe 18 nchini Algeria. Baada ya hapo, alikwenda kwenye makambi ya chama cha Polisalio walipokuwa wanashikiliwa mateka hao kusimamia kazi ya kuwaachia huru mateka hao. Tarehe 19 atakwenda nchini Morocco kukutana na mfalme Muhammad wa sita wa nchi hiyo.
Sasa serikali ya Morocco haijazungumzia lolote kutokana na kuachiwa kwa mateka wote wa Morocco. Lakini ofisa wa serikali ya Morocco ambaye hakudokeza jina lake aliilalamikia nchi yake jirani kuzuia kukamilisha kazi hiyo. Anaona kuwa chama cha Polisalio na Algeria inayokiunga mkono, kinataka kupata faida ya kisiasa kwa kuwachia huru mateka wa Morocco kwa vikundi na kwa vipindi.
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-19
|