Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-19 16:39:17    
Nchi mbalimbali za Jumuiya ya SADC zahimiza utandawazi wa kikanda

cri

Mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC ulifungwa tarehe 18 huko Gaborone, mji mkuu wa Botswana. Marais na wakuu wa serikali za nchi 14 wanachama wa SADC waliohudhuria mkutano huo wameona kwa kauli moja kuwa, nchi wanachama zinatakiwa kuchukua hatua halisi ili kutekeleza makubaliano mbalimbali yaliyosainiwa na mikakati ya maendeleo iliyowekwa ndani ya jumuiya ya SADC ili kuhimiza utandawazi wa sehemu hiyo.

Mwezi Agosti mwaka 2003, mkutano wa wakuu wa jumuiya ya SADC ulipitisha "Mpango wa uelekezaji wa mikakati ya maendeleo ya kikanda" nchini Tanzania. Mpango huo umeweka mipango mbalimbali wa kuondoa umaskini kwenye sehemu ya kusini mwa Afrika na kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa. Namna ya kutekeleza mpango huo ni changamoto kubwa inayozikabili nchi mbalimbali za jumuiya ya SADC, wakuu wengi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wamezitaka nchi wanachama ziondoe vikwazo ili kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo muhimu.

Ili kuharakisha mchakato wa utandawazi wa kikanda, mkutano huo wa wakuu umepitisha azimio moja la kuhimiza mawasiliano kati ya watu wa sehemu hiyo. Kutokana na makubaliano, katika mwaka mmoja, kama muda wa kukaa usiozidi siku 90 katika nchi nyingine mwanachama wa SADC kwa raia wa nchi moja mwanachama wa SADC, basi raia huyo hana haja ya kuomba visa tena ya kuingia nchi hiyo nyingine. Lakini makubaliano hayo yalisainiwa tu na viongozi wa nchi 4 tu, ambayo yanatakiwa kusainiwa na nchi 9 wanachama ndipo yatakapoweza kufanya kazi.

Katika miaka 25 iliyopita tangu kuanzishwa kwa jumuiya ya SADC, nchi wanachama wake zimesaini makubaliano 23, yakiwemo makubaliano 18 yaliyoidhinishwa na kufanya kazi kama vile makubaliano ya biashara, nishati, ushirikiano wa kwenye sekta za siasa, ulinzi na usalama. Lakini jumuiya hiyo inakabiliwa na tatizo ambalo makubaliano mengi ambayo yameanza kazi lakini yamewekwa kando na bado hayajatekelezwa kihalisi. Ndiyo maana, wakuu wa nchi nyingi waliohudhuria mkutano huo wamesisitiza umuhimu mkubwa wa kutekeleza makubaliano hayo kwa maendeleo ya sehemu hiyo.

Katika mwaka mmoja uliopita, nchi wanachama wa SADC zimedumisha kimsingi utulivu wa kisiasa. Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeonesha mwelekeo wa juhudi za maendeleo, na kupitisha katiba mpya, ambapo serikali mpya ya nchi hiyo itaundwa baada ya uchaguzi utakaofanyika kabla ya tarehe 30 mwezi Juni mwakani. Mkutano wa wakuu wa jumuiya ya SADC uliposifu juhudi za serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na wananchi wake katika kujipatia utulivu na maendeleo ya taifa, pia umefuatilia shughuli za vikosi vya kijeshi vya mashariki ya nchi hiyo ambazo zimekuwa changamoto kwa amani na utulivu wa kisiasa wa nchi hiyo. Mkutano huo umeamua kumkabidhi mwenyekiti wa Shirika la ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama la SADC ambaye pia ni rais wa Namibia Bwana Hifikepunye Pohamba jukumu la kufanya ushirikiano na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na pande nyingine mbalimbali husika, ili kuhakikisha uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unafanyika kwa wakati bila vikwazo.

Kwenye mkutano huo, rais Festus Mogae wa Botswana amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa SADIC badala ya waziri mkuu wa Mauritius Navinchandra Ramgoolam.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-19