Inspekta mkuu wa polisi wa London Bw. Ian Blair, alijitetea katika toleo la tarehe 21 la gazeti la "News of the World" kuwa, alijua kuwa kijana wa Brazil Bw. Jean Charles de Menezes hakuwa na makosa hadi siku ya pili baada ya yeye kuuawa kwa kushukiwa kuwa ni gaidi. Tamko hilo alilolitoa linafuatia lawama walilotoa jamaa za kijana huyo la kumtaka awajibike kuhusu kifo cha Menezes. Lakini vyombo vya habari vya huko vinaona kuwa tamko hilo la kujitoa katika lawama haliwezi kuepusha kuhojiwa na umma kuhusu kifo cha Menezes.
Tarehe 22 mwezi Julai yaani siku ya pili baada ya kutokea kwa mlipuko wa pili mjini London, Menezes mwenye umri wa miaka 27 alifuatwa na polisi wa kupambana na magaidi kutokana na kijana huyu mwenye sura ya kiasia na kuvaa koti kubwa katika majira hayo. Polisi walisema kuwa walitekeleza amri ya kumwua walipokuwa wakitaka kumkamata. Lakini baada ya hapo waliona kuwa kijana yule aliyeshukiwa mwenye mabomu ya kujilipua hakuwa na makosa yoyote. Lakini Bw. Ian Blair katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika siku ile aliendelea kusema kuwa Menezes alikuwa mtuhumiwa. Jamaa za Menezes na wakili walisema kuwa ni vigumu kuamini kuwa Ian Blair alitangaza hivyo katika hali ya kutofahamu ukweli wa mambo, kwa upande mmoja waliwalaani polisi kuwa hawakusahihisha makosa yao. Kwa upande mwingine walisema kuwa Ian Blair anapaswa kuwajibika kuhusu kifo cha Menezes na kumtaka ajiuzulu. Ni dhahiri kuwa nia ya Ian Blair ya kutoa maelezo katika gazeti ni kutaka kueleza kuwa wakati ule hakufahamu mambo yaliyotokea.
Ukweli ni kuwa Menezes aliuawa kwa makosa, ni suala ambalo watu wana maoni ya tofauti. Pamoja na kuwa uchunguzi unaendelea, baadhi ya habari zilizodokezwa zinaonesha kuwa watu walioshuhudia na picha zilizopigwa na Kamera ya video vinathibitisha kuwa Menezes aliingia kwenye subway akitembea, na hata alisimama kuchukua gazeti linalotolewa bila malipo, kisha alitembea na kupita kwenye sehemu ya kukagua tikiti, na alianza kukimbia alipoona subway ikikaribia kituoni, wakati alipouawa alikuwa ameketi ndani ya behewa. Lakini hapo awali polisi walisema kuwa Menezes aliruka kwenye sehemu ya kukagua tiketi, tena nguo aliyovaa Menezes siku ile haikuwa koti kubwa lililojaa vitu ndani, bali lilikuwa ni jaketi lililotengenezwa kwa kitambaa cha pamba. Baadhi ya maofisa walioshiriki katika uchunguzi kuhusu tukio hilo wanaona kuwa, kutokana na data zilizoko hivi sasa ni vigumu kuona kama Menezes wakati ule alitenda vitendo vinavyofanya watu kumshuku kuwa ni wa hatari. Maneno hayo yanafanya Ian Blair akabiliwe na shinikizo kubwa.
Baada ya habari hizo kudokezwa, serikali ya Brazil ilighadhabishwa na kuamua kutuma maofisa wawili wa sheria wa ngazi ya juu kwenda London wiki ijayo kuonana na wajumbe wa kamati ya rufani ya polisi iliyokabidhiwa jukumu la kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo. Kamati hiyo ya rufani ya polisi ililalamika kuwa ilipata shinikizo kutoka polisi ya Uingereza hapo mwanzoni. Lakini imefanya vyombo vya habari vidai ufanywe uchunguzi kuhusu tukio la kifo cha Menezes. Lakini Ian Blair anashikilia kuwa, baada ya kutokea tukio hilo polisi inafanya kila iwezacho kufanya ushirikiano katika uchunguzi huo wala hakukuwa na mtu aliyejaribu kuficha ukweli wa mambo. Alisema kuwa hivi sasa jukumu kubwa zaidi la polisi ni kupambana na ugaidi. Kisha waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Bw. Charles Clarke alieleza uungaji mkono kwa Ian Blair, anaona kuwa mambo iliyofanya polisi katika uchunguzi kuhusu kifo cha Menezes ni ya kuridhisha.
Wachambuzi wanaona kuwa polisi ya Uingereza bado haijatoa maelezo ipasavyo kwa umma.
Idhaa ya Kiswahili
|