Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-23 17:59:26    
Xiamen yahimiza maingiliano ya uchumi na biashara ya kando mbili

cri

Katika miaka ya karibuni uhusiano wa mambo ya uchumi na biashara kati ya mkoa wa Taiwan na China bara umekuwa mkubwa mwaka hadi mwaka. Kampuni na viwanda vingi vya Taiwan vinaanzisha matawi yake katika China bara na bidhaa za Taiwan zilizosafirishwa kwa China bara pia zinaongezeka mwaka hadi mwaka. Mji wa Xiamen wa mkoa wa Fujian unaotazamana na Taiwan ukitumia ubora wake wa kijiografia unafanya kazi muhimu katika maingiliano ya uchumi na biashara ya kando mbili za mlango wa bahari wa Taiwan.

Mji wa Xiamen ni moja wa maeneo maalumu ya uchumi yaliyoanzishwa mapema nchini China, mji huo wenye eneo la kilomita za mraba zaidi ya 1,500 unatazamana na Jinmen ya Taiwan kwa kutengwa na bahari kwa umbali wa kilomita chache tu. Ubora wa kijiografia unauwezesha kuwa na ubora katika ukuzaji wa uhusiano wa uchumi na biashara pamoja na Taiwan. Mwezi Aprili mwaka 1997 kando mbili za mlango bahari zilianzisha kwa majaribio safari za uchukuzi za moja kwa moja. Hivi sasa kiasi cha 70% ya makontena kutoka Taiwan yanaingia au kutoka China bara kupitia mji wa Xiamen. Mwezi Januari mwaka 2001 usafarishaji wa abiria kati ya Xiamen na Jinmen, Taiwan ulifunguliwa ambazo ni njia muhimu kwa mawasiliano ya kando mbili. Takwimu zinaonesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu idadi ya abiria waliosafirishwa kwenye njia hiyo ilizidi laki 2.5. Mkurugenzi wa ofisi ya bandari ya Xiamen Bw. Zhou Qinghai alisema kuwa baada kufunguliwa kwa njia hiyo usafirishaji wa abiria kati ya kando hizo mbili umepata ufanisi mkubwa na kupongezwa na wafanyabiashara wa kando mbili, hususan wafanyabiashara waliowekeza katika China bara. Alisema,

"Kwa kawaida muda wa safari ni nusu saa hadi dakika 40 hivi, mtu akipanda meli kutoka Xiamen atafika Jinmen baada ya dakika 40, kisha anasafiri kutoka kiwanja cha ndege cha Jinmen hadi kisiwa kikuu cha Taiwan inamchukua pungufu ya saa mbili, endapo anasafiri kutoka Xiamen kurudi Taiwan kwa kupitia Macao au Hong Kong, kwa kawaida itamchukua saa 4 hadi 5. Kwa hiyo njia ya usafirishaji kati ya Xiamen na Jinmen inasifiwa kuwa ni 'njia ya dhahabu'."

Kuboreshwa kwa mazingira ya mawasiliano kunaleta ongezeko la biashara kati ya Xiamen na Taiwan. Bidhaa zinazosafirishwa na Xiamen kwa Taiwan ni pamoja na dawa za mitishamba, chakula na vitu vinavyohitajiwa na katika maisha ya watu, na vitu vinavyosafirishwa na Taiwan kwa Xiamen ni mazao ya kilimo yenye umaalumu wa Taiwan. Ili kuhimiza maendeleo ya biashara ya kando mbili, serikali ya China bara imejenga soko la bidhaa ndogo ndogo kwenye kisiwa cha Dadeng, Xiamen, hivi sasa thamani ya biashara ya soko hilo imefikia Yuan milioni 200 kwa mwaka.

Hivi karibuni aina 15 za matunda ya Taiwan yameruhusiwa kuingia kwenye soko la China bara bila ushuru wa forodha, aina nyingi za matunda hayo yanapatikana Taiwan peke yake. Ili kuhimiza maendeleo ya biashara kati ya kando mbili, serikali ya China bara ilifungua soko la bidhaa ndogo ndogo kwenye kisiwa cha Dadeng, Xiamen, ambalo thamani ya biashara imefikia Yuan za Renminbi milioni 200 kwa mwaka.

Hivi karibuni aina 15 za matunda yanayosafirishwa kutoka Taiwan kwenye soko la China bara zinasamehewa ushuru wa forodha, ambazo nyingi ni matunda yanayopatikana Taiwan tu. Xiamen ilitumia vizuri nafasi hiyo, ilirahisisha shughuli za karantini kuhusu matunda kutoka Taiwan na kutenga sehemu maalumu kwa matunda kutoka Taiwan katika soko la uuzaji wa jumla wa matunda la mji wa Xiamen. Hatua hizo zimeanzisha mazingira bora kwa matunda ya Taiwan kuingia kwenye soko la China bara kwa kupitia Xiamen. Naibu mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya biashara ya mji wa Xiamen Bw. Dai Bizhong alisema,

"Tokea tarehe 28 mwezi Mei, kampuni 6 za Xiamen ziliagiza shehena 17 za matunda ya Taiwan zenye uzito wa tani 86 na thamani ya dola za kimarekani elfu 84, ambayo mengi yaliuzwa Beijing, Shanghai na sehemu nyingine karibu na Xiamen."

Ubora wa kijiografia umeifanya Xiamen iwe sehemu ya kwanza inayochaguliwa na kampuni na viwanda vya Taiwan kwa uwekezaji katika China bara. Hadi mwezi Julai mwaka huu Xiamen iliwekezwa miradi zaidi ya 2,300 na wafanyabiashara kutoka Taiwan. Jumla ya thamani ya miradi iliyowekezwa imefikia dola za kimarekani bilioni 2.8. Miongoni mwa kampuni na viwanda vilivyowekezwa na wafanyabiashara kutoka Taiwan, kampuni za kilimo zinachukua nafasi kubwa zaidi katika Xiamen, ikilinganishwa na viwanda vingine vya uzalishaji uliozoeleka vya mitambo, nguo na elekitroniki, uwekezaji wa kilimo unahitaji kuchagua mahali. Hali ya hewa na udongo vya Xiamen vinalingana na vya Taiwan na vinafaa kwa uzalishaji wa kilimo.

Mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita mfanyabiashara kutoka Taiwan alikwenda Xiamen kuanzisha kampuni ya usindikaji wa chakula ya Xinchun. Hivi sasa kampuni hiyo ina wafanyakazi zaidi ya 700, na thamani ya uzalishaji wake inazidi dola za kimarekani milioni 12 kwa mwaka. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Lin Fufan alisema,

"Ninaishi Gaoxiong, hali ya hewa ya huko ni sawa na ya hapa, mazao ya kilimo yanakua vizuri katika hali ya hewa ya namna hiyo, tena mazingira ya uwekezaji pia ni mazuri, idadi ya wafanya-biashara walioko Xiamen imezidi elfu 20."

Xiamen iko karibu na Taiwan, utamaduni na matamshi ya maneno pia ni ya namna moja, hivyo Xiamen ina ubora ambao haupo katika sehemu nyingine katika ushirikiano wa kando mbili. Naibu meya wa Xiamen bibi Huang Ling alisema kuwa, maingiliano ya uchumi na biashara kati ya Xiamen na Taiwan yananufaisha watu wa kando zote mbili.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-23