Mahitaji:
Samaki gramu 750, chumvi gramu 6, mchuzi wa soya gramu 25, mvinyo wa kupikia gramu 15, M.S.G gramu 3, unga wa pilipili manga gramu 2, vipande vya tangawizi gramu 15, vipande vya vitunguu maji gramu 15, ufute wa mafuta gramu 50.
Njia:
1. Mwoshe samaki, ondoa utumbo, na umweke mistari kwa kisu kwenye mgongo wake.
2. Washa moto mimina maji kwenye sufuria, na tia samaki, vitunguu maji na tangawizi na uchemshe kwa dakika 15, kisha pakua.
3. Tia chumvi, M.S.G, unga wa pilipili manga, mvinyo wa kupikia, vitunguu maji na tangawizi kwenye samaki, halafu mimina mchuzi wa soya.
4. Pasha moto tena, mimina mafuta ya ufuta kwenye sufuria, baada ya kuchemka, pakua na umimine kwenye samaki. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-24
|