Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-24 21:24:35    
Guangxi yazalisha mboga bora

cri

Mwaka huu mkoa wa Guangxi umeandaa mashamba hekta 8,000 kupanda mboga zisizona vitu vyenye madhara kwa afya za watu katika majira ya kupukutika majani na baridi.

Vituo vya uzalishaji mboga ni dhamana muhimu kwa mboga bora, mkoa wa Guangxi unahakiksha ubora wa mboga kwa kufanya udhibiti wa hatua tatu za uzalishaji mboga katika vituo, pembejeo za kilimo na ukaguzi kwa mboga zinazoingia sokoni. Hivi sasa vituo vya uzalishaji wa mboga katika majira ya kupukutika majani na baridi vimejengwa katika miji ya Nanning, Liuzhou, Beise na Guilin. Katika mji wa Liuzhou vimejngwa vituo vinne vya uzalishaji mboga vyenye hekta 64.3; vituo hivyo vilivyoko katika mji wa Gulin mwaka 2004 vilikuwa na mashamba hekta 406.6, na unanuia kupanda mboga kiasi cha hekta 666.6 mwaka 2005; wilaya ya Hepu ya mji wa Beihai imejenga vituo 6 vya majaribio vya uzalishaji mboga zisizona vitu vyenye madhara kwa afya za watu. Vituo vya uzalishaji mboga vya mkoa wa Guangxi vinazingatia kuchagua mbegu bora na ya kutoa mavuno mazuri.

Kuhusu pembejeo za kilimo mkoa wa Guangxi umetunga maagizo kadhaa kuhusu matumizi ya dawa za kilimo na mbolea za madawa, udhibiti wa dawa za kilimo ambazo vitu vingi vyenye madhara kwa afya za watu kubaki katika mboga na kueneza matumizi ya dawa za kilimo zenye madhara kidogo kwa afya za watu na mbolea ya samadi. Wilaya ya Tianyang ya mji wa Beise imebuni sera husika za kutoa mafunzo maalumu kwa wakulima wa mboga, kufuata utaratibu wa teknolojia ya uzalishaji mboga zisizona vitu vya madhara na kuimarisha usimamizi kuhusu matumizi ya dawa za kilimo na mbolea za madawa.

 

Aidha, mkoa wa Guangxi umeimarisha utekelezaji wa ukaguzi wa ubora na usalama wa mboga zinazoingia soko la mboga na kujenga vituo vya kukagua vitu vyenye madhara vilivyobaki katika mboga kwenye vituo vya uzalishaji mboga na masoko ya mboga ili kufanya upimaji kuhusu mboga zinazoingia sokoni. Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2005, idara za kilimo katika ngazi mbalimbali za mji wa Nanning zilifanya upimaji mara elfu 470 ambazo 99.4% kati ya mboga hizo zililingana na vigezo vilivyowekwa na kuchukua nafasi ya kwanza miongoni miji 37 mikubwa na wastani nchini. Mji wa Liuzhou umekuwa na mfumo wa ukaguzi wa ubora na usalama kuhusu mazao ya kilimo katika ngazi tano za mji, wilaya, taarafa, vituo na masoko ili kuhakikisha usimamizi wa usalama kuhusu uzalishaji na uuzaji wa mboga za mji wa Liuzhou.

Kutokana na utekelezaji wa udhibiti wa hatua tatu za vituo vya uzalisjaii, pembejeo za kilimo na ukaguzi wa kuingia sokoni, ubora wa mboga za Guanzxi umechukua nafasi ya kwanza katika nchi nzima. Mwaka 2004 katika ukaguzi wa ubora na usalama uliofanywa na wizara ya kilimo kuhusu ubora na usalama wa mboga, mboga bora za mkoa wa Guangxi ulizidi 90%. Mwezi Januari mwaka 2005 katika ukaguzi uliofanywa na wiara ya kilimo mboga bora za mji wa Nanning zilifikia 89.4%, na kufikia 98.4% katika mwezi Aprili zikichukua nafasi ya kwanza nchini.

Habari zinasema kuwa uzalishaji wa mboga katika majira ya kupukutika majani na siku baridi ni sekta ya kuzoeleka yenye ubora mkoani Guangxi, tokea Guangxi kuanza kurekebisha muundo wa kilimo na kuchukulia uzalishaji mboga katika majira ya kupukutika majani na baridi kuwa hatua muhimu ya kuongeza pato la wakulima, eneo la kupanda mboga mkoani Guangxi mwaka 2004 lilifikia hekta 7467 zikichukua nafasi ya 7 nchini.

 

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-24