Chini ya shinikizo za nchi za Ufaransa na Italia ambazo ni nchi zinazozalisha bidhaa nyingi za nguo na mashirika ya nguo ya Umoja wa Ulaya, kamati ya Umoja wa Ulaya na idara za serikali ya China mwezi Juni zilifikia kumbukumbu ya maelewano kuhusu suala la bidhaa za nguo za China, na kurekebisha upya mgao wa uagizaji wa aina 10 za bidhaa za nguo za China katika miaka miwili ijayo.
Lakini miezi miwili baadaye, Kamati ya Umoja wa Ulaya inakabiliwa tena shinikizo la wafanyabiashara wa uagizaji bidhaa, wauzaji wa rejareja na wateja wa nchi za Umoja wa Ulaya ambao wanadai kulegeza vizuizi kwa uagizaji bidhaa za nguo za China. Katika muda mfupi namna hii, kwanini Umoja wa Ulaya unaweza kukabiliwa na mashinikizo tofauti namna hii?
Kutokana na kanuni zilizowekwa na shirika la biashara duniani, utaratibu wa mgao wa bidhaa za nguo duniani ulifutwa kwa pande zote kuanzia tarehe 1 Januari mwaka huu. Lakini nchi zinazozalisha bidhaa za nguo nyingi zaidi kama vile Ufaransa na Italia pamoja na mashirika ya bidhaa za nguo yalichukua kisingizio kwamba uagizaji wa bidhaa za nguo za China uliongezeka kwa kiasi kikubwa na kuvuruga soko la Umoja wa Ulaya, yakiitaka kamati ya Umoja wa Ulaya uweke vizuizi vya uagizaji wa bidhaa za nguo za China. Chini ya shinikizo hilo, Kamati ya Umoja wa Ulaya ilifanya mazungumzo mara kwa mara na kufikia makubaliano. Lakini kuanzia mwezi Julai, kamati ya Umoja wa Ulaya ilitangaza kwa mfululizo kwa uagizaji wa aina fulani fulani za bidhaa za nguo za China umezidi mgao wa mwaka huu, na mgao wa aina nyingine za uagizaji wa bidhaa za nguo pia utakwisha hivi karibuni. Hii si kama tu imesababisha kamati ya Umoja wa Ulaya kutoidhinisha tena maombi mapya ya uagizaji wa bidhaa za nguo za China, bali pia imesababisha bidhaa nyingi za nguo za China zilizoagizwa mwanzoni mwa mwaka huu kulundikana kwenye forodha za Umoja wa Ulaya, na kuleta hasara kwa wafanyabiashara wa uagizaji bidhaa na uuzaji bidhaa wa rejareja wa Umoja wa Ulaya. Ndiyo maana Kamati ya Umoja wa Ulaya ikakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wafanyabiashara hao na nchi wanachama wake za Ujerumani, Sweden na Denmark ya kuitaka kulegeza hata kufuta vizuizi vya uagizaji bidhaa za nguo za China.
Hali hiyo imeonesha dhahiri kuwa, kuweka vizuizi vya uagizaji bidhaa siyo dawa nzuri ya kutatua suala la bidhaa za nguo, bali ni hatua inayoweza kuhatarisha maslahi ya pande mbili.
Watu wengi wa sekta za bidhaa za nguo wanaona kuwa, sababu moja kubwa ya kutokea kwa suala la bidhaa za nguo la China na Umoja wa Ulaya ni kuwa, mashirika ya nguo hayakufanya maandalizi ya kutosha katika kipindi cha mpito kabla ya WTO kufuta utaratibu wa mgao. Mawaziri wanne wa Uholanzi, Sweden, Denmark na Finland hivi karibuni walitoa makala zao kwenye gazeti la Financial Times la Uingereza wakisema kuwa, hawaoni kuziwekea vizuizi vya uagizaji bidhaa za nguo za China kutaweza kuokoa viwanda vya nguo vya Umoja wa Ulaya.
Vyombo kadhaa vya habari vya Ulaya vinaona kuwa, uagizaji wa bidhaa za nguo za China si kama tu unaweza kusababisha kufilisika kwa viwanda kadhaa vya nguo vya Ulaya visivyo na uwezo wa ushindani na watu kadha wa kadha kupoteza ajira, bali pia unaweza kuleta nafasi za ajira kwa watu wengine wa shughuli za biashara ya rejareja. Na kuziwekea vizuizi bidhaa za China na kuzifanya zilundikane kwenye forodha, na kusababisha hali wasiwasi ya utoaji bidhaa kwenye soko, vilevile kunaweza kuyafanya mashirika kadha wa kadha ya uuzaji wa rejareja yafunge milango na watu wake wapoteze ajira, na kuleta madhara kwa wafanyabiashara na wateja, na kudhuru maendeleo mazuri ya uchumi wa Ulaya.
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-25
|