Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-25 21:46:18    
Mji wa Hohhot

cri

Mji wa Hohhot ni mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, pia ni kituo cha kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni cha mkoa huo.

Mji wa Hohhot ni mji muhimu kwenye mikakati ya uendelezaji mkubwa wa sehemu ya magharibi ya China. Na pia ni daraja linalounganisha sehemu ya ndani ya China na Mongolia, Russia na nchi za Ulaya ya Mashariki.

Mji wa Hohhot uko kwenye tambare ya Tumch iliyoko katikati ya mkoa huo, na uko kusini ya Mlima Yin na kaskazini ya Mto Manjano. Mwinuko kutoka usawa wa bahari wa mji huo ni mita 1050. Joto la wastani kwa mwaka mzima ni nyuzi 8 sentigredi, na kiasi cha mvua inayonyesha kwa mwaka ni milimita 300 hadi 500. Mjini humo kuna mandhari nzuri, na mazao na bidhaa nyingi zinazalishwa huko. Mji huo pia ni sehemu yenye maliasili nyingi ambayo ni sehemu muhimu ya ujenzi.

Mjini Hohhot kuna watu wa makabila 36 wakiwemo Wamongolia, Wahan, Waman na Wahui. Eneo la mji huo ni kilomita za mraba elfu 17. Idadi ya watu ni milioni 2.147. Watu laki 2.68 ni wa makabila madogo madogo, na miongoni mwa watu hao, watu laki 2 ni wa kabila la Mongolia.

Hohhot ni mji maarufu wenye historia ndefu na utamaduni mkubwa, na ni moja ya chimbuko la utamaduni wa China. Zaidi ya miaka laki 5 iliyopita, utamaduni wa binadamu ulianza kutokea kwenye mji huo. Masalio mengi yameonesha historia ndefu ya mji huo.

 

Mji wa Hohhot ni mji unaofungua mlango kwa nje. Katika Enzi za Han na Tang, mji huo ulikuwa ni njia muhimu kwa China kufanya mawasiliano na nchi za nje, na ni kituo muhimu kwenye njia ya hariri mbugani. Katika Enzi za Ming na Qing, mji huo ulikuwa ni sehemu waliyojikusanya wafanyabiashara wengi. Hivi sasa Mji wa Hohhot umeanzisha uhusiano wa kiuchumi, ushirikiano wa kiteknolojia na maingiliano ya kiutamaduni na nchi na sehemu 26.

Kutokana na fursa nzuri iliyoletwa na mikakati ya uendelezaji mkubwa wa sehemu ya magharibi ya China, mji huo unachukua maendeleo kuwa kazi yake ya kwanza, na kushikilia kwenda na wakati. Umeharakisha mchakato wa maendeleo ya viwanda, miji na mambo ya upashanaji habari, kufanya juhudi kusukuma mbele maendeleo makubwa ya uchumi na maendeleo ya pande zote ya jamii. Kwenye msingi wa uchumi unaostawi, kiwango cha juu cha sayansi na teknolojia, hali nzuri ya mawasiliano, upashanaji habari na huduma za jamii, mji wa Hohhot unashikilia mageuzi na kusukuma mbele maendeleo. Uchumi na shughuli za jamii mjini humo zimekuwa na mwelekeo mzuri wa kupata maendeleo ya kasi. Mji huo umekuwa sehemu nzuri ya kuwekeza vitega uchumi kwa wafanyabiashara wa China na wa nchi za nje.

picha husika>>

1  2