Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bw. Hamid Reza Asefi tarehe 28 alisema kuwa Iran haioni Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ni nchi pekee za kushiriki katika mazungumzo na Iran kuhusu suala la nyuklia, na pengine nchi hizo tatu zitasukumwa pembeni katika mazungumzo ya baadaye. Msemaji huyo alisema, Iran inataka zaidi kufanya mazungumzo na Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani. Hii imedhihirisha wazi msemo uliooneshwa na Iran siku chache zilizopita kwamba inataka nchi zitakazoshiriki kwenye mazungumzo ziongezeke, na kuvunja muundo wa mazungumzo yaliyoendelea kwa muda mrefu kati yake na nchi tatu za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.
Bw. Hamid Reza Asefi alisema, kama nchi hizo zitakuwa nje ya mazungumzo au la, ni uamuzi wa nchi hizo zenyewe. Katibu wa Kamati ya Usalama ya Iran ambaye pia ni mjumbe wa kwanza wa maazungumzo ya suala la nyuklia Bw. Ali Larijani alidokeza kuwa kuhusu suala la nyuklia, Iran imeanza kuzungumza na Japan, Malaysia na Afrika Kusini, na itazungumza na kundi la nchi zisizofungamana na upande wowote, China na Russia. Vyombo vya habari vya Ulaya vinaona kuwa msimamo huo uliooneshwa na Iran unalenga kumaliza nafasi ya uongozi ya nchi tatu hizo za Ulaya na kuboresha hali ya Iran katika mazungumzo.
Serikali mpya ya Iran inaona kuwa tumaini la serikali ya zamani la kutaka kutatua suala la nyuklia kwa kufanya mazungumzo na nchi hizo tati katika muda wa miaka miwili iliyopita ni la kitoto, na ni kosa kuendelea na mazungumzo hayo bila mwisho, kwa sababu lengo ambalo nchi hizo tatu ni sawa na la Marekani, na zinaweza tu kuruhusu Iran itumie nishati ya nyuklia kwa kiwango kidogo na kutaka kusimamisha kabisa mpango wa Iran kubadilisha uranium. Lakini hayo Iran kamwe haitakubali. Serikali mpya ya Iran inasema kuwa nchi tatu za Ulaya ziliwahi kukubali kuwa Iran ina haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa ajili ya amani kwenye "mkataba wa Paris". Kutokana na hayo, Iran inashutumu nchi hizo tatu kuwa zimevunja ahadi zao. Serikali mpya ya Iran inaona kuwa nchi tatu za Ulaya zina fikra potovu na kusababisha mazungumzo yasifanikiwe na kuyasukuma mazungumzo hayo kwenye kichochoro kisichopitika. Kama mazungumzo hayo yakiendelea, lengo la Iran la kuendeleza na kuitumia nishati ya nyuklia kwa kujitegemea litakuwa bure. Kwa hiyo ni kuvunja tu muundo wa sasa wa mazungumzo ni njia pekee ya kuweza kuleta uhai mpya wa mazungumzo.
Hivi sasa msimamo wa Iran ni mgumu, lakini je, ugumu huo utadumu? Inasemekana kuwa tarehe 3 Septemba ripoti ya Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani itabainisha kama kweli Iran inataka kuendeleza silaha za nyuklia. Nchi za Magharibi ziliwahi kutangaza sana kugundua alama ya Iran kusafisha uranium, lakini sasa imekuwa wazi kuwa alama hiyo ilikuwa ni zana zilizoagizwa kutoka nchi za nje, zaidi ya hayo, serikali mpya ya Iran inaona kuwa ina kitu kizito mikononi mwa Iran, kwamba Iran ina athari kubwa kwa madhehebu ya Shia ambayo ni muhimu katika serikali ya Iraq, kwa mtazamo wa mbali, utulivu wa Iraq hauwezi kutengana na ushirikiano wa Iran. Iran ni nchi inayozalisha mafuta kwa wingi na kusafirisha nje, katika hali ya sasa ambayo bei ya mafuta inapanda bila kushuka, nchi za Magharibi kuiwekea vikwazo Iran ni muhali.
Nchi tatu za Umoja wa Ulaya ziliwahi kuahidi kutoa msaada wa kiuchumi na teknolojia ili Iran iache kabisa mpango wake wa nyuklia, lakini sasa imekwua wazi kuwa lengo lao hilo haliwezi kufikiwa. Mbele ya Iran ambayo haiogopi "kiboko" wala "karoti", nchi tatu za Ulaya zinaonekana zimeishiwa na dawa, ila kutangaza kusimamisha mazungumzo kwa muda. Kutokana na habari za Ulaya, nchi hizo zimekuwa zikijadiliana mbinu ya kutumia kwa Iran. Je nchi hizo zitaendelea kuzungumza na Iran au zitaunga mkono Marekani na kuchukua msimamo mkali. Baada ya ripoti itakayotolewa na Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani tarehe 3 Septemba Umoja wa Ulaya utachukua msimamo gani? Tunasubiri.
Idhaa ya kiswahili 2005-08-29
|