Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-29 19:14:23    
China itahimiza maendeleo ya harakati za wanawake duniani

cri

  

    Mkutano wa maadhimisho ya miaka 10 tangu ufanyike mkutano wa nne wa wanawake wa Umoja wa Mataifa umefunguliwa tarehe 29 hapa Beijing, rais Hu Jintao katika ufunguzi wa mkutano huo alisema kuwa tangu ufanyike mkutano wa nne wa wanawake wa Umoja wa Mataifa, harakati za wanawake wa nchi mbalimbali zimepata maendeleo makubwa. China itajitahidi pamoja na watu wa nchi mbalimbali kuhimiza usawa wa kijinsia, kulinda haki za wanawake na maendeleo ya harakati za wanawake duniani.

    Mwaka 1995, mkutano wa nne wa wanawake wa Umoja wa Mataifa ulifanyika hapa Beijing ambao ulihudhuriwa na wanawake zaidi ya elfu 40 na ni mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhudhuriwa na washiriki wengi. Mkutano ule ulipitisha "Azimio la Beijing" na "mpango wa utekelezaji", kuthibitisha usawa kati ya wanaume na wanawake na kusema kuwapa haki wanawake ni kitu muhimu sana katika kuleta maendeleo na amani. Katika muda huo wa zaidi ya miaka 10, umuhimu wa mkutano ule umedhihirishwa na maendeleo na uzoefu wa harakati za wanawake duniani.

    Mkutano wa maadhimisho ya miaka 10 tangu ufanyike mkutano wa nne wa wanawake wa Umoja wa Mataifa umefunguliwa tarehe 29 hapa Beijing, rais Hu Jintao alipotoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano alisisitiza umuhimu wa kufanyika kwa mkutano huo, alisema, "Siku ya leo baada ya kupita miaka 10, China inafanya mkutano wa kuadhimisha miaka kumi tangu ifanyike mkutano wa nne wa wanawake wa Umoja wa Mataifa, ili kuhimiza usawa wa kijinsia na kuleta maendeleo kwa pamoja, kukuza moyo wa mkutano wa nne wa wanawake wa Umoja wa Mataifa, kuangalia jinsi serikali za nchi mbalimbali zilivyotekeleza ahadi zilizotoa kuhusu kuhimiza amani na maendeleo ya dunia, kutathimini mafanikio ya maendeleo ya harakati za wanawake duniani, kutafuta njia ya kuhimiza maendeleo ya harakati za wanawake duniani."

    Rais Hu Jintao alisema kuwa katika miaka zaidi ya 10 iliyopita, moyo wa mkutano wa nne wa wanawake wa Umoja wa Mataifa umekuzwa katika mipango na vitendo vya serikali za nchi mbalimbali, wazo la kuhimiza usawa wa kijinsia limetekelezwa katika sera za serikali za nchi mbalimbali, vitengo vinavyohimiza maendeleo ya harakati za wanawake vimeanzishwa, mazingira ya kuishi, haki za maendeleo na hadhi ya jamii vya wanawake wa nchi mbalimbali vimeboreshwa kwa viwango tofauti.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan alituma salamu za pongezi kwa mkutano wa maadhimisho zikisifu umuhimu wa mkutano wa nne wa wanawake duniani na kusema kuwa tangu ufanyike mkutano wa Beijing baadhi ya masuala yaliyochukuliwa kuwa ni masuala ya wanawake, sasa yanachukuliwa kuwa ni masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa. Mifumo na shirikisho la wanawake linalovyovuka mipaka ya nchi vimeundwa. Bw. Annan anatarajia nchi mbalimbali duniani zitaendelea kutekeleza "Azimio la Beijing" na "mpango wa utekelezaji" na kutoa mchango mpya katika kuhimiza maendeleo ya harakati za wanawake.

    Harakati za wanawake wa China pia zilipata maendeleo makubwa tangu ufanyike mkutano wa nne wa wanawake wa Umoja wa Mataifa. Rais Hu Jintao alisema kuwa China itabuni sera zenye ufanisi mkubwa kutatua matatizo yaliyopo hivi sasa na kuhimiza maingiliano ya kimataifa ili kuhimiza maendeleo ya harakati za wanawake duniani, alisema, "China itanyanyua juu bendera za amani, maendeleo na ushirikiano, kushikilia njia ya amani na maendeleo, kukuza ushirikiano na maingiliano na jumuiya ya kimataifa, kuendeleza harakati za wanawake duniani na kunufaisha wanawake wa nchi mbalimbali na watu duniani.

 

Idhaa ya Kiswahili