Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-30 13:46:17    
Mkutano wa Kupunguza Silaha Haukupiga Hatua kwa Muda Mrefu

cri

Mkutano wa kupunguza silaha mwaka 2005 hivi sasa unafanyika mjini Geneva. Ukiwa mkutano pekee wa kupunguza silaha duniani umekwama bila mafanikio yoyote katika muda wa miaka sita iliyopita.

Mkutano huo ulianzia mwishoni mwa miaka ya 50 wakati kamati ya nchi kumi ya kupunguza silaha ilipoanzishwa, lengo lake lilikuwa ni kupunguza silaha chini ya usimamizi wa kamati hiyo. Ili kuambatana na mabadiliko duniani, kamati hiyo iliyokuwa yenye nchi kumi za Magharibi tu hapo awali, ilipanua mpaka kwenye nchi zisizofungamana na upande wowote na nchi kubwa kiasi na ndogo. Mkutano wa kupunguza silaha uliwahi kutoa mchango wake kutokana na mikataba mfululizo iliyopatikana kama mikataba ya "Marufuku kwa Majaribio ya Silaha za Nyuklia kwa Kiwango", "Mkataba wa Matumizi ya Anga ya Juu", "Marufuku ya Keneza Silaha za Nyuklia", "Mafuruku ya Silaha za Viumbe", "Marufuku ya Silaha za Kimemikali" na "Marufuku ya Majaribio ya Silaha za Nyuklia".

Ingawa mkutano huo umepata mafanikio mengi, lakini tokea karne mpya ianze, mkutano huo haukupiga hatua yoyote nyingine. Hii inamaanisha kuwa pande hizo zina misimamo tofauti.

Kwa ufupi, shinikizo la usalama linalotoka kutoka pande mbalimbali ni sababu muhimu ya kuufanya mkutano huo usiweze kufikia maafikiano. Hivi sasa, migogoro iliyosababishwa na ugomvi wa kugombea ardhi, dini, ukabila inatokea mara kwa mara, na matumizi ya nguvu ya kijeshi yanatumika zaidi kwa lengo la utatuzi wa migogoro hiyo. Jambo linalokuwa baya zaidi ni kuwa ugaidi umeshamiri, na tatizo la vikundi visivyo vya kiserikali kupata silaha, ni tatizo jipya la kimataifa. Hali mbaya ya usalama duniani imesababisha mkutano wa kupunguza silaha usifanikiwe. Pili, Marekani ambayo ni nchi yenye nguvu kubwa ya kijeshi duniani imekuwa sababu nyingine ya kuzuia upunguzaji wa silaha.

Wachambuzi wanaona kuwa kuzingatia maslahi ya pande mbelimbali, ni sharti la lazima kwa mkutano huo kupata mafanikio. Kushiriki kwa China katika mkutano huo kumeleta juhudi nyingi za kufanikisha mkutano huo.

Mwaka 1980 China ilianza kushiriki rasmi kwenye mkutano huo, mwaka 1983 ilipeleka balozi wake wa kudumu kwenye makao makuu ya mkutano huo huko Geneva. China iliwahi kutoa mapendekezo mengi kuhusu kuzuia mashindano ya silaha, kupunguza silaha na kuzuia vita vya nyuklia. Ni jambo linalostahili kutajwa kwamba katika miaka mingi iliyopita China imefanya juhudi nyingi kwa ajili ya kuzuia mashindano ya silaha katika anga ya juu. Mwezi Machi mwaka huu China, Russia na Taasisi ya Upunguzaji wa Silaha katika Umoja wa Mataifa zilifanya kongamano kuhusu "Kuhakikishwa kwa Usalama wa Anga ya Juu: Kuzuia Mashindano ya Silaha katika Anga ya Juu". China inaona kuwa kupatikana kwa mkataba mapema kuhusu matumizi ya anga ya juu kunanufaisha matumizi ya amani na kuleta manufaa kwa binadamu na kuimarisha uslama kwa nchi zote.

Idhaa ya kiswahili 2005-08-30