Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-30 21:13:15    
Uzalishaji wa televisheni za kitarakimu wapamba moto

cri

Ofisa wa idara ya utangazaji na sinema ya China hivi karibuni hapa Beijing alitangaza kuwa ifikapo mwaka 2015 sekta ya uzalishaji wa televisheni hapa nchini itakuwa imamaliza kipindi cha mpito cha kutoka uzalishaji wa televisheni za analog kwa televisheni za kitarakimu. Hatua hiyo inamaanisha kuwa televisheni zaidi ya milioni 400 zilizopo hivi sasa karibu zote zitabadilishwa kwa televisheni za kitarakimu. Habari zinasema kuwa pamoja na mchakato wa utangazaji wa vipindi vya televisheni wa kitarakimu, sekta mpya kabisa ya uzalishaji wa televisheni za kitarakimu inastawi kimya kimya.

Bw. Sun Zhi ambaye anaishi katika mji wa Hangzhou, sehemu ya mashariki ya China, baada ya kutoka kazini kitu kinachomvutia zaidi ni kuangalia televisheni. Lakini tofauti na televisheni za watu wengi ni kuwa televisheni ya Bw. Sun ni ya kitarakimu. Alisema kuwa televisheni anayotumia ina uwezo mwingi mbali na kuanzalia vipindi vya televisheni.

"Baada ya kuwa na televisheni ya kitarakimu, ninaweza kuchagua vipindi ninavyopenda, nikitaka kuangalia habari basi ninaweza kuona mara moja, nikitaka kuangali sinema pia ninaweza kuona mara moja. Mbali na hayo ninaweza kununua vitu kwa kupitia televisheni ya kitarakimu au kufahamu habari katika tovuti ya serikali, kwa jumla mambo yamekuwa rahisi."

Televisheni ya kitarakimu ni ya kizazi cha tatu baada ya televisheni za kawaida na za rangi, ambayo upigaji picha, uhariri, utengenezaji vipindi, utangazaji na unasaji vipindi vyote vinatumia tekinolojia ya kitarakimu. Hivi sasa mchakato wa maandalizi ya vipindi katika stesheni za televisheni umetumia tekinolojia ya kitarakimu ila tu televisheni za nyumbani kwa watu ni za analog.

Tokea mwaka 2003 miji 49 ya China ikiwemo ya Qingdao, Hangzhou na Fuoshan inahimiza wakazi wa huko kuangalia televisheni za kitarakimu badala ya kuangalia televisheni analog. Wakazi wengi kama Bw. Zun Zhi wanaweza kuonapicha safi kama za DVD katika televisheni za kawaida na kusikia sauti nzuri iliyofanana na ya ile katika majumba ya sinema. Aidha, wakazi wa miji hiyo licha ya kuweza kuona vipindi mbalimbali vya televisheni, bali pia wanaweza kupata habari na huduma za shughuli za kiserikali, biashara ya televisheni na hali ya mawasiliano ya sasa hivi.

Ili kuhimiza maendeleo ya sekta ya uzalishaji wa televisheni za kitarakimu nchini China, serikali pia imeweka ratiba ya kipindi cha mpito cha kuelekea matumizi ya televisheni za kitarakimu. Naibu kiongozi wa idara ya tekinolojia ya idara ya utangazaji ya taifa Bw. Wang Lian alisema kuwa China inanuia kusimamisha utangazaji wa vipindi vya televisheni anlog mnamo mwaka 2015 na kutumia televisheni za kitarakimu nchini kote.

"Katika mchakato wa cable TV kuelekea za kitarakimu, tumebuni mpango wa maendeleo wa utekelezaji wa vipindi vinne katika maeneo matatu ya mashariki, kati na magharibi na kujitahidi kuufanikisha katika mwaka 2005."

Habari zinasema kuwa hivi sasa idadi ya televisheni zilizoko nchini China imezidi milioni 400, katika hali ya kutosheka kwa televisheni za analog, matumizi ya televisheni za kiutarakimu bila shaka ni nafasi nazuri kwa viwanda vya televisheni. Ili kushindania soko la televisheni za kitarakimu la siku za mbele, viwanda vingi vya China hivi sasa vinajitahidi kufanya utafiti kuhusu televisheni za kitarakimu. Naibu meneja mkuu wa kampuni ya TCL Bw. Luo Qiulin alisema kuwa kampuni yao inafuatilia sana hali ya maendeleo ya uzalishaji wa televisheni za kitarakimu na kubuni mkakati wa uwekezaji na maendeleo.

"TCL itajitahidi kufanya utafigi kuhusu televisheni za kitarakimu kwenye msingi wa kutosheleza manufaa ya wateja. Itashirikiana na wafanya biashara wa mtandao na wa uendeshaji wa shughuli kuhusu televisheni za kitarakimu ili kuweka kigezo cha namna moja kuhusu televisheni za kitarakimu na kuanzisha muundo mpya unaonufaisha pande mbalimbali."

Habari zinasema kuwa hadi mwaka 2008 kampuni ya TCL itawekeza Yuan bilioni 1 kwa utafiti, uzalishaji na uuzaji wa televisheni za kitarakimu.

Siyo tu kwamba viwanda mbalimbali vya televisheni za rangi vimechukulia maendeleo ya sekta ya televisheni za kitarakimu kuwa ni nafasi moja kubwa ya biashara, baadhi ya serikali za mitaa zimeorodhesha maendeleo ya sekta ya uzalishaji wa televisheni za kitarakimu kuwa ni miradi muhimu inayoweza kukuza maendeleo yao ya uchumi. Kwa mfano, mji wa Baotou ulioko sehemu ya kaskazini ya China ambao ni kituo cha zamani cha viwanda nchini China, hivi sasa sekta za kuzoeleka za chuma na chuma cha pua, alyuminium, thulium, umeme na mitambo za mji huo zimezuiliwa na uwezo wa mazingira ya huko. Hivyo serikali ya mji wa Baotou imeamua kurekebisha muundo wa uzalishai mali wa huko kwa kupitia kukuza sekta ya uzalishaji wa televisheni za kitarakimu ili kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii ya huko.

Naibu meya wa mji wa Baotou Bw. Zhag Jiping alisema kuwa tokea mwaka jana wakitumia nafasi ya kuendeleza televisheni ya kitarakimu walianzisha kampuni, kujenga mfumo, kubuni sera husika na kuingiza miradi kadhaa ikiwa ni pamoja na mistari ya uzalishaji wa kisanduku kinachowekwa juu ya televisheni analog cha kunasa mawimbi ya vipindi vya televisheni za kitarakimu, uzalishaji wa televisheni za mkononi, uzalishaji wa LCD screen na televisheni za plasm, ambayo imewekezwa dola za kimarekani bilioni 1.3. miradi hiyo baada ya kukailishwa ujenzi wake italeta pato la Yuan zaidi ya bilioni 50 kwa mwaka.

Mara tu baada ya sekta ya uzalishaji wa televisheni za kitarakimu kuibuka nchini China, sekta hiyo ikafuatiliwa na wawekezaji wengi wa nchi za nje, baadhi ya kampuni za uwekezaji zimeanza kuwekeza katika baadhi ya maeneo ya sekta ya televisheni za kitarakimu nchini. Meneja wa uwekezaji wa kampuni ya ushirikiano wa uchumi wa Marekani na China Bw. Xiong Yuzhu alisema kuwa ushindani katika eneo la uzalishaji wa zana na televisheni za kitarakimu ni mkali kutokana na wingi wa uwekezaji, hivyo sekta hiyo haitawekwa katika eneo la uwekezaji wa kampuni yao hivi karibuni. Lakini wanayo shauku kubwa kuhusu mambo yaliyomo katika televisheni za kitarakimu za China. Alisema kuwa wanaona televisheni za kitarakimu ni kama medium ambayo mambo yaliyomo ndani yake ni muhimu sana yakiwa ni pamoja na ununuzi wa vitu katika televisheni, hususan frequency channe ambayo ina mambo mengi.

Wataalamu wa sekta hiyo walichambua kuwa kwa kulinganishwa na televisheni za analog, televisheni za kitarakimu ni mfumo mpya kabisa wa utoaji huduma katika televisheni na inahusika na panda nyingi zikiwa ni pamoja na wafanya-biashara wa mambo yaliyomo katika televisheni za kitarakimu, wafanya-biashara wa mtandao, wafanya-biashara wa hardware na software pamoja na wafanya-biashara wa uzalishaji wa televisheni za kitarakimu. Ingawa hivi sasa sekta ya televisheni za kitarakimu imeibuka siku chache zilizopita, idadi ya wateja bado ni ndogo na vigezo husika bado havija kamilika, lakini viwanda mbalimbali vilivyoko katika mnyororo wa sekta hiyo vinaona sekta hiyo ni nafasi nzuri sana na yenye maendeleo makubwa katika siku za mbele.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-30