Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-31 16:52:59    
Mapishi ya Supu ya Luosong

cri

Mahitaji:

Nyama ya ng'ombe gramu 500, mchuzi wa nyanya, viazi mviringo vitatu, kitunguu kimoja, kiasi kidogo cha tangawizi, unga wa pilipili manga na chumvi.

Njia:

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande vipande, halafu uviweke kwenye sufuria yenye maji, na pasha moto, baada ya kuchemka uvipakue vipande vya nyama ya ng'ombe.

2. tia mafuta kidogo kwenye sufuria, na pasha moto tena mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia vipande vya nyama ya ng'ombe na uvikoroge, tia vipande vya tangawizi na chumvi korogakoroga halafu mimina maji, kisha endelea kuchemsha.

3. baada ya maji kuchemka, tia vipande vya viazi mviringo, na upunguze moto, endelea kuchemsha kwa dakika 40, tia mchuzi wa nynya na vipande vya kitunguu, tia chumvi korogakoroga, na baada ya dakika 10, uipakue na tia unga wa pilipili manga. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-31