Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-31 18:40:54    
Wanasayansi watafuta viumbe nje ya dunia

cri

Wakati wanasayansi wengi wanapojaribu kutafuta viumbe visivyo vya dunia kwenye sayari ya Mars, baadhi ya wanasayansi wanatupia macho yao kwenye sayari inayojulikana kwa jina la "Europe" ambayo ni sayari inayoizunguka Jupiter na iko mbali sana na dunia.

Profesa wa chuo kikuu cha Cambridge Bw. Simon Kanvi Moros alisema "kuna uwezekano mdogo sana kuona viumbe vilivyoko nje ya dunia katika jamii ya sayari ya Jua, lakini kama kuna uwezekano huo havikosi kuwepo kwenye sayari ya 'Europe' na wala siyo kwenye Mars."

Idara ya safari za anga ya juu ya Marekani tarehe 12 mwezi Agosti ilirusha chombo cha uchunguzi cha aina mpya cha Mars, kinacholenga kuchunguza raslimali ya maji na dalili za viumbe kwenye sayari ya Mars.

Mwanasayansi huyo mashuhuri wa elimu ya viumbe vya kale amesema kuwa, hata kama kuna viumbe kwenye sayari ya Mars, viumbe hivyo ni vile vilivyoangamia. Wana elimu wa viumbe vya kale wanaofanya utafiti kuhusu viumbe vilivyoangamia wanaweza kufanya kazi muhimu sana katika kutafuta viumbe vilivyoko nje ya dunia.

Msomi wa elimu ya viumbe vya kale kutoka chuo cha Pomorner Bw. Robert Gance anaona kuwa, sayari za "Europe" na Mars zina baridi sana, mazingira hayo hayafai kwa viumbe kuishi. Hivi sasa watu bado hawafahamu muundo wa wake wa kijiolojia. Kwa hiyo itawastaajabisha watu sana kama vitagunduliwa viumbe katika sayari ya "Europe", lakini si kulikuwa na mambo mengi ya kustaajabisha watu yaliyokuwa ya kweli.

Data zilizogunduliwa na Satellite zinaonesha kuwa, ukubwa wa sayari hiyo unalingana na wa mwezi, sehemu yake ya juu kabisa inafunikwa na barafu nyembamba, wanasayansi wanaona kuwa kuna bahari chini ya barafu hiyo ya nje.

Wanaona kuwa sayari ya "Europe" iko kati ya Jupiter na sayari nyingine, ambazo zinabadilishana nishati, hivyo huenda kuna maji chini ya barafu. Lakini majaribio maarufu yaliyojulikana kwa "Mille" yanaonesha kuwa maji, hewa, joto na mazingira ya kikemikali vitaweza kuzalisha viumbe, na sayari ya "Europe" imekuwa na maji na joto.

Lakini tukitaka kujua kama kuna viumbe kwenye sayari ya "Europe", hatuna budi kutegemea vituo vilivyochukuliwa na chombo cha anga kutoka kwenye sayari hiyo. Wanasayansi wanaona kuwa kutokana na umbali mkubwa ni vigumu kwa chombo cha anga kutua kwenye "Europe".

Hivi sasa idara ya safari za anga ya juu ya Marekani inanuia kurusha chombo kinachoizunguka "Europe" ndani ya miaka mitatu ijayo ikiwa na lengo la kugundua unene wa barafu pamoja na kina cha maji ya bahari yanayoweza kuweko chini ya barafu hiyo.

Bw. Simon alisema kuwa wanasayansi wa Ulaya na Marekani pia wanajadili uwezekano wa kutua kwenye "Europe", lakini ni nishati ya nyuklia peke yake inayoweza kufikisha chombo cha anga kwenye sayari hiyo ya mbali. Mambo yanayowatia wasiwasi ni kuwa endapo urushaji wa chombo hicho ukishindwa, chombo hicho kitachafua mazingira ya dunia baada ya kuanguka duniani.

Wataalamu 12 wa elimu ya viumbe vya kale vya nchini na wa nchi za nje wakiwemo Bw. Simon na Bw. Gance pamoja na wataalamu zaidi ya 10 wa China, hivi sasa wanafanya utafiti kuhusu dalili za viumbe vilivyokuweko zaidi ya miaka milioni 600 iliyopita kwenye milima ya mkoani Guizhou. Wataalamu hao watashiriki mkutano wa kijiolojia wa kipindi cha Cambrian ambao ungefanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mjini Nanjing.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-31