Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-31 20:27:17    
Elimu ya lugha mbili za Kitibet na Kichina mkoani Tibet

cri

Wasikilizaji, mnasikiliza wanafunzi wa shule ya msingi ya wilaya ya Zedang kwenye sehemu ya Shannan mkoani Tibet wakiimba wimbo mmoja wa kitibet. Mkoa unaojiendesha wa Tibet ulioko kwenye sehemu ya "Paa la dunia" ni moja kati ya mikoa mitano inayojiendesha ya makabila madogomadogo nchini China. Idadi kubwa ya wakazi wa mkoa huo ni wa-Tibet, na wanatumia lugha ya kitibet.

Kutokana na mazingira maalum ya kijiografia na ya kiutamaduni, kabla ya mwaka 1959, Tibet bado ilikuwapo kwenye jamii ya mfumo wa kimwinyi wa wakulima watumwa, asilimia 95 ya wa-Tibet walikuwa ni wakulima watumwa wasiokuwa na uhuru wa kibinafsi, licha mbali elimu. Mwaka 1959, kutokana na China kutekeleza mageuzi ya demokrasia huko Tibet, mamilioni ya wakulima watumwa wa Tibet walipata uhuru wa kibinafsi na raslimali ya kujikima na kufanya shughuli za kiuchumi, zikiwemo mashamba na mifugo, pia wakaanza kupewa elimu bure na serikali.

Baada ya kuasisiwa kwa mkoa unaojiendesha wa Tibet mwaka 1965, kwa mujibu wa sera ya kuendeleza elimu ya lugha za kikabila, mkoa huo ulianza kueneza elimu ya lugha mbili za Kitibet na Kichina, na kuinua kadri iwezekanavyo kiwango cha elimu ya watoto wa wakulimu na wafugaji wa Tibet.

Ofisa mkuu wa elimu wa mkoa huo Bw. Ma Erqiong anaona kuwa, katika miaka 40 iliyopita, idara za elimu za ngazi mbalimbali mkoani humo zilikuwa zimezingatia sana elimu ya lugha ya kitibet. Alisema:

"lugha ya kitibet ni utamaduni wa kimaendeleo uliovumbuliwa na wa-Tibet, na ni lazima turithi na kuendeleza utamaduni huo katika vizazi vya baadaye. Kwa ajili ya lengo hilo, serikali ya mkoa huo ilianzisha kamati ya kazi ya kueneza elimu ya lugha ya kitibet na kikundi cha uongozi wa kuelekeza elimu ya lugha hiyo."

Kwa mujibu wa Bw. Ma Erqiong, kila mwanafunzi wa Tibet hujifunza lugha ya kitibet kuanzia shule ya msingi hadi shule ya sekondari ya juu, na kuanza kujifunza lugha ya kichina kuanzia darasa la tatu tu la shule ya msingi. Lengo la mpango huo ni kuwawezesha wanafunzi hao kuishi kwa urahisi mkoani Tibet na kote nchini China.

Hii ni hali halisi ya kipindi cha lugha ya kitibet katika shule ya sekondari ya wilaya ya Naidong kwenye sehemu ya Shannang mkoani Tibet. Wanafunzi wote wa shule hiyo wanatoka familia za wakulima au wafugaji wa huko, na vipindi vya lugha za kitibet na kichina vimewekwa katika kila darasa. Ili kuwasaidia wanafunzi kuongeza uwezo wa matumizi ya lugha hizo mbili, shule hizo pia zinaandaa mara kwa mara maonesho ya michezo, mashindano ya kutoa hutuba, uandishi wa makala na maandiko ya lugha hizo mbili. Mwanafunzi Pingcuo Wangdui alisema,

"Lugha ya kitibet ni lugha ya kabila letu. Kwenye vipindi vya lugha hiyo, tutaweza kusoma historia, mashairi ya kabila la Tibet na riwaya nyingi za kigeni zilizotafsiriwa kwa kitibet, navipenda sana vipindi hivyo. Baada ya kumaliza masomo ya shule ya sekondari, nitaendelea kusoma katika shule za sekondari ya juu. Nataka kuwa mwalimu katika siku za baadaye."

Naibu ofisa mkuu wa idara ya elimu ya michezo ya sehemu ya Shannan Bw. Zhaxi Jiacuo alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, shule zote za kimsingi na za sekondari za huko zimetimiza lengo la kuwawezesha wanafunzi kutumia lugha zote mbili. Shule nyingi za kimsingi za huko zimeweka vipindi vya lugha ya kichina kuanzia darasa la kwanza, mpango huo unakubaliwa na kuungwa mkono na wazazi wa wanafunzi na jamii. Kutokana na kutekeleza mfumo wa elimu kwa lugha mbili, wanafunzi wa Tibet wanaweza kuelewa vizuri masomo mbalimbali yanayofundishwa kwa kichina baada ya kujifunza lugha ya kichina kwa miaka 6 katika shule ya kimsingi.

Wakati wa kuimarisha mfumo wa elimu kwa lugha mbili, baadhi ya shule za kimsingi za huko pia zimeweka vipindi vya lugha ya kiingereza kuanzia darasa la tatu. Mlikuwa mnasikiliza kipindi kimoja cha kiingereza katika shule ya kimsingi ya wilaya ya Zedang. Bw. Danzeng Qunpei ambaye mtoto wake anasoma katika shule ya kimsingi alisema kuwa, anaunga mkono sana shule nyingi zaidi za kimsingi mkoani Tibet kuanzisha elimu ya lugha nyingi. alieleza,

"kuna wa-Han na wageni wengi kwenye sehemu nyingi mkoani Tibet, kama hatuwezi kuongea kichina na kiingereza, basi ni vigumu kwetu kuelewana. Shule kufundisha lugha mbili au tatu za kiingereza, kichina na kitibet, kunasaidia sana."

Kuhusu hali hiyo, ofisa mkuu wa elimu wa Tibet Bw. Ma Erqiong anaona kuwa, mkoa wa Tibet ukitaka kuendelea na kuwa wa kisasa, elimu ya Tibet lazima ikabili dunia na kukabili siku za baadaye. Lugha za kichina na kiingereza zimekuwa vyombo muhimu kwa wa-Tibet kupata maendeleo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-31