Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-02 21:27:39    
Kikundi cha nyimbo na ngoma cha China chafanya maonesho katika nchi nne barani Afrika.

cri

Kuanzia tarehe 2 hadi 23?mwezi Agosti?wachezaji 25 wa Ujumbe wa kikundi cha jeshi cha nyimbo na ngoma (China Flag Song and Dance Ensemble) wa Idara ya siasa ya sehemu ya kijeshi ya Chengdu, China, walitembelea nchi nne za Afrika Ethiopia, Kenya, Msumbiji na Tanzania, na kufanya maonesho mazuri katika nchi hizo, ambapo walisifiwa sana na waafrika.

Mkuu wa ujumbe huo anasema:

"Safari hii, ujumbe wetu umefanya maonesho kumi kadhaa katika nchi nne za Afrika, na kukaribishwa na waafrika. Baada ya kutembelea nchi hizo, tumeona kuwa waafrika ni wakarimu sana, na wanapenda sanaa ya kichina. Tunafurahi kuona kuwa tumepata mafanyikio mazuri katika safari yetu barani Afrika."

Kikundi cha Kijeshi cha Nyimbo na ngoma kinajulikana sana nchini China. Kikundi hicho kilianzishwa mwezi Septemba mwaka 1952, na kuiwakilisha nchi na jeshi kufanya maonesho katika nchi kumi kadhaa duniani zikiwemo Uingereza, Canada, Russia, Poland, Ujerumani, Ufaransa, Romania, Korea ya Kaskazini, Laos na Viet Nam. Hii ni mara yake ya kwanza kufanya maonesho barani Afrika tangu kianzishwe katika miaka 53 iliyopita.

Tarehe 4, Agosti, ujumbe huo ulifanya maonesho ya kwanza barani Afrika kwenye Jumba la maonesho la taifa huko Addis Ababa nchini Ethiopia. Usiku huo, watu wapatao 3000 kutoka nyanja mbalimbali za Ethiopia, maofisa wa ubalozi wa China nchini humo, wafanyakazi wa mashirika ya China na watu wenye asili ya kichina nchini humo walitazama maonesho hayo. Maonesho hayo yaliyokusudia kuadhimisha miaka 35 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Ethiopia, yalisifiwa sana na waziri wa utamaduni wa Ethiopia Bw. Shome Toga. Ofisa huyo pia anatumai kuwa nchi hizo mbili zitaimarisha mawasiliano ya utamaduni ili kuongeza maelewano kati ya nchi hizo mbili.

Kenya ilikuwa ni kituo cha pili kwa ujumbe huo barani Afrika. Mada muhimu ya maonesho ya ujumbe huo ni kuadhimisha miaka 600 tangu Msafiri mkuu wa China Zheng He afunge safari ya mbali baharini. Tarehe 8, mwezi Agosti, tamasha hilo lilifanyika kwenye Jumba la taifa huko Nairobi, nchini Kenya. Balozi wa China nchini humo Bw Guo Chongli alitoa hotuba kabla ya tamasha hilo kufanyika akisema:

"Usiku huu, tunaburudishwa kwa maonesho mazuri ya kikundi maarufu cha sanaa kutoka China. Maonesho yake mazuri si kama tu yanakaribishwa nchini China, bali pia nchi nyingine duniani kama vile Uingereza, Marekani na Ujerumani. Natumai kuwa maonesho hayo yataongeza maelewano kati ya China na Kenya, na kuimarisha urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili."

Katika maonesho hayo, wachezaji wa China walicheza ngoma na kupiga ala za muziki za makabila mbalimbali ya China, zikiwemo za makabila ya waMeng, waXian, waZang, waDai, waYi, na kuimba nyimbo za makabila hayo pamoja na dansi za kisasa. Wakati mwimbaji alipoimba wimbo maarufu wa Kenya Jambo, watazamaji wote walifuata sauti ya mwimbaji na kuimba kwa pamoja, na jumba la maonesho lilikuwa kama ni bahari ya furaha.

Baada ya maonesho kumalizika, mtazamaji mkenya anasema:

Tarehe 14 hadi 23, ujumbe huo ulitembelea Msumbiji na Tanzania, na kufanya maonesho kwa ajili ya wenyeji wa nchi hizo. Tunaamini kuwa, mawasiliano hayo ya utamaduni yatakuwa mengi zaidi katika siku za baadaye, na kujenga daraja imara la urafiki kati ya China na Afrika.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-02