Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-05 15:45:27    
Palestina yatumai kuanzisha mchakato wa amani haraka iwezekanavyo

cri

Mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina Bw. Mahmoud Abbas hivi karibuni alieleza kuwa Palestina inatumai kurejesha mara moja mazungumzo kati yake na Israel baada ya kukamilisha mpango wa upande mmoja kwa Israel, kuhusu masuala mengi ambayo bado hayajatatuliwa, ili kuanzisha nchi ya Palestina mwaka kesho. Maneno hayo ya Abbas yameonesha moyo wa kuanzisha haraka mchakato wa amani. Lakini wachambuzi wameainisha kuwa, hivi sasa kuna matatizo kadhaa kuhusu kuanzisha mchakato wa amani.

Kadiri mpango wa upande mmoja wa Israel unavyokaribia kukamilika, ndivyo mamlaka ya Palestina inaweka mkazo wake katika kurejesha upya mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel wakati wa kupewa mamlaka ya Gaza. Palestina inatumai kuwa Israel itaendelea kuondoka kutoka katika ardhi za Palestina inazozikalia.

Moyo wa matarajio wa Palestina unaeleweka. Kuondoka kutoka Gaza ni kuondoka kwa hiari na kwa mara ya kwanza kwa Israel kuondoka kutoka kwenye ardhi ya Palestina inayoikalia, na ni maendeleo makubwa ya juhudi za ukombozi wa taifa wa Palestina, jambo ambalo ni hatua muhimu katika kujenga nchi ya Palestina. Lakini Palestina bado ina wasiwasi kwa nia halisi ya Israel kutekeleza mpango wa upande mmoja. Wasiwasi huo ni kuwa nia ya Israel kuacha Gaza ni kwa ajili ya kuimarisha utawala wake katika sehemu ya kando ya magharibi ya mto Jordan iliyo yenye mkakati na Jerusalem na kuweka eneo la ardhi za nchi ya Palestina kutokana na mahitaji ya Israel. Sasa Israel inaharakisha kujenga ukuta wa utenganishaji katika kando ya magharibi ya mto Jordan na kuweka mpaka wa siku za usoni kati ya Palestina Israel, hatua ambayo imeongeza wasiwasi wa Palestina. Palestina inaona kuwa kurejesha upya mazungumzo ya amani haraka iwezekanavyo na kutatua masuala mengi ambayo bado hayajatatuliwa kabla ya masuala hayo kuwa bayana na kutatua masuala hayo kwa kunaambatana na maslahi ya msingi ya Palestina, na haifai kuahirisha zaidi mazungumzo hayo.

Vyombo vya habari vinaona kuwa hali ya maendeleo ya hivi karibuni inaonesha kuwa mustakbali wa kuanzisha upya mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel hauwafurahishi watu.

Kwanza, Israel bado inashikilia msimamo wake baada ya kuondoka kutoka katika Gaza, yaani Palestina ikitaka kurejesha upya mazungumzo ya amani, lazima ichukue hatua imara za kunyang'anya silaha kutoka kwa makundi yenye msimamo mkali na kusimamisha mashambulizi dhidi ya Israel.

Pili, jambo la dharura kwa waziri mkuu wa Israel Sharon ni kushinda njama ya wapinzani wa chama cha Likud ya kumwondoa madarakani mwenyekiti wa chama cha Likud na waziri mkuu. Msimamo wa Sharon utadhibitiwa na hali ya kisiasa ya Israel ambao ni kikwazo kikubwa cha kuzuia mchakato wa amani.

Tatu, Marekani iliyosuluhisha mgogoro kati ya Palestina na Israel imebadili msimamo wake, haitaji mpango wa amani wa Mashariki ya Kati na kuweka shinikizo kwa Palestina katika suala la usalama.

Hivi sasa, Israel na Marekani bado ni upande wa kuongoza mchakato wa amani wa Palestina na Israel. Misimamo yao inaonesha kuwa mustakbali wa kurejesha mazungumzo ya amani hivi karibuni sio mzuri.

Idhaa ya kiswahili 2005-09-05