Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-06 16:56:25    
Tangazo 0906

cri
Taiwan ni kisiwa kimoja cha China, lakini kutokana na sababu za vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyofanyika nchini China katika miaka ya 40 ya karne iliyopita, Taiwan na China bara zimekaa katika hali ya uhasama kwa kiasi fulani katika zaidi ya miaka 50 iliyopita, hivyo likatokea ati suala la Taiwan. Basi Taiwan ni kisiwa cha namna gani? Kwanini tunasema Taiwan ni sehemu moja ya ardhi ya China? Serikali ya China ina sera gani ya kimsingi katika kutatua suala la Taiwan? Serikali ya China imefanya juhudi gani katika kuhimiza muungano wa Taiwan na China bara? Hali ya biashara kati ya Taiwan na China bara ikoje? Kuna uhusiano gani kati ya watu wa Taiwan na wa China bara katika utamaduni wa jadi? Ili kuwawezesha wasikilizaji wa nchi mbalimbali waelewe kimsingi juu ya masuala hayo, Radio China kimataifa itatangaza vipindi vya chemsha bongo kuhusu "Taiwan?kisiwa cha hazina cha China". Tunawakaribisha wasikilizaji wetu mshiriki kwenye shindano hilo la chemsha bongo.

Kama tulivyofanya katika mashindano ya chemsha bongo yaliyopita, kila baada ya kusoma makala moja, tutaweza kutoa maswali mawili, ili wasikilizaji wetu wajibu, baada ya kupokea majibu, kamati ya uchaguzi ya Radio China kimataifa itachagua wasikilizaji watakaopewa tuzo ya nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu pamoja na washindi watakaopewa tuzo maalum watakaopata fursa ya kutembelea China bara kwa wiki moja mwakani.

Shindano la chemsha bongo kuhusu ujuzi wa "Taiwan-Kisiwa cha hazina cha China" limeanza na litakwisha tarehe 20 Desemba. Tunawataka wasikilizaji msikilize makala tutakazowasomea, mnapaswa kutuletea majibu kabla ya tarehe 20 Desemba mwaka huu. Tarehe 4 Septemba tutaanza kusoma makala ya kwanza ya shindano hilo la chemsha bongo, baadaye tutarudia matangazo yetu.

Tunawatakia wasikilizaji wetu mafanikio mema.

Idhaa ya kiswahili 2005-09-06