Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-06 17:01:45    
Makala ya kwanza ya Shindano la chemsha bongo kuhusu "Taiwan-kisiwa cha hazina cha China"

cri

       Kwa nini tunasema Taiwan ni ardhi ya China

Wasikilizaji wapendwa, tunawakaribisha washiriki shindano la chemsha bongo kuhusu ujuzi wa "Taiwan, kisiwa cha hazina cha China". Katika kipindi hiki cha leo tunawaletea makala ya kwanza kuhusu historia na hali ya ujumla ya Taiwan, tutawafahamisha chanzo cha suala la Taiwan, na kuwaambia kwa nini tunasema Taiwan ni ardhi ya China.

Kisiwa cha Taiwan kiko kwenye eneo la bahari la kusini mashariki ya China bara, hiki ni kisiwa cha kwanza cha China kwa ukubwa, eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya elfu 30. Kisiwa hicho kinatazamana na China bara, katikati kuna mlango bahari, na sehemu iliyo karibu zaidi kati ya pande hizo mbili ni kilomita 130. Katika zama za kale sana, ardhi ya kisiwa cha Taiwan kilifungamana na China bara, baadaye kutokana na shughuli za sehemu ya juu ya uso wa dunia, sehemu iliyoungana ilizama chini ya bahari, na ukatokea mlango bahari, na kuundwa kuwa Kisiwa cha Taiwan cha hivi sasa.

Hivi sasa Taiwan ina idadi ya watu milioni 23, hii ni 1.8 % ya ile ya jumla ya China bara. Kisiwa cha Taiwan siyo kikubwa sana, lakini sura yake ya kijiografia ni ya aina mbalimbali, ambapo kuna milima, vilima, tambarare, mabonde, maziwa na maporomoko. Taiwan ni sehemu maarufu yenye vivutio vingi vya utalii, watu huisifu Taiwan kwa mandhari yake kuwa ni yenye "milima ya kupendeza, misitu minene, maporomoko mengi na pwani za ajabu". Kisiwa cha Taiwan kinazalisha mazao mengi ya mpunga, miwa ya sukari, chai, matunda, na maua ya orchid. Na shughuli za utengenezaji, upashanaji habari na biashara na nje ziliendelea zaidi kisiwani Taiwan, shughuli hizo zimekuwa nguzo za uchumi wa Taiwan.

Utafiti wa mambo ya kale umeonesha kuwa, wakazi wa Taiwan wa mwanzoni wengi wao walikuwa wakazi wa China bara waliohamia huko, na kumbukumbu nyingi za maandishi zimeandikwa kuhusu hali ya wachina waanzilishi walivyoendeleza Taiwan. Kuhusu mahusiano kati ya Kisiwa cha Taiwan na China bara katika historia, Mkuu wa Taasisi ya Taiwan katika Chuo kikuu cha muungano cha Beijing Bwana Xu Bodong akifahamisha alisema:

Kuhusu Taiwan, historia yenye kumbukumbu ya maandishi ilianzia mwaka 230 kabla ya Kristo. Wakati huo mfalme wa dola la Wu Sun Quan aliwahi kuwatuma maofisa na askari elfu 10 kuvuka bahari na kufika Taiwan. Ilipofika mwishoni mwa karne ya 6 na mwanzoni mwa karne ya 7 wakati wa Enzi ya Sui, Mfalme Suiyangdi aliwatuma watu kwenda Taiwan mara tatu, kufanya ukaguzi, kufahamishwa desturi na mila tofauti na kuwapa pole wakazi wa huko. Wakati huo huo wakazi wa pwani ya China bara, walianza kuhamia kwenye visiwa vya Penghu vya Taiwan na ufundi wao wa kimaendeleo wa uzalishaji mazao. Mwanzoni mwa karne ya 17, waholanzi walichukua fursa ambayo enzi ya Ming ya China ya kale ya wakati huo ilikuwa dhaifu, wakavamia na kuikalia Taiwan, Taiwan ikawa sehemu ya kikoloni ya Uholanzi kwa muda. Katika miaka ya 60 ya karne ya 17, shujaa wa taifa la China jenerali Zheng Chenggong aliliongoza jeshi kuwafukuza wakoloni wa Uholanzi, na Taiwan ikarudi kwa China.

Lakini mwishoni mwa karne ya 19 Taiwan ilikuwa mikononi mwa wavamizi tena. Mwaka 1894, Japan ilianzisha vita vya kuivamia China, Serikali ya Enzi ya Qing iliyoshindwa katika vita hivyo ililazimishwa kusaini "Mkataba wa Maguan", ilitenga Taiwan na kuikabidhi kwa Japan,

Mwaka 1945, Japan ilishindwa katika vita vikuu vya pili vya dunia, China ikarudisha tena Taiwan iliyotawaliwa na Japan kwa miaka 50.

Profesa Xu Bodong alifahamisha mchakato wa China wa kurudisha Taiwan akisema:

Mwaka 1937, Japan ilianzisha vita vya kuivamia China kutoka pande zote, China ikaanzisha mapambano dhidi ya uvamizi kwa miaka minane. Mwaka 1941, serikali ya China iliziambia nchi mbalimbali katika "Tangazo la China la kuanzisha vita dhidi ya uvamizi wa Japan" kuwa, China imefuta mikataba yote iliyohusika na uhusiano kati ya China na Japan ukiwemo "Mkataba wa Maguan", tena itarudisha Taiwan. Mwaka 1943, "Taarifa ya Cairo" iliyosainiwa kati ya China, Marekani na Uingereza ilieleza kuwa, "Ardhi ya China iliyoibwa na Japan kama vile sehemu ya kaskazini mashariki, Taiwan na visiwa vya Penghu zote zirudishwe kwa China". Mwaka 1945, "Taarifa ya Potsdam" iliyosainiwa na nchi nne za China, Marekani na Uingereza pamoja na Urusi ya zamani ilisisitiza kuwa "masharti yaliyothibitishwa kwenye Taarifa ya Cairo yapaswa kutekelezwa". Mwezi Agosti mwaka huo, Japan ilitangaza kusalimu amri, na iliahidi katika "Vifungu vya Japan kusalimu amri" kuwa "itatekeleza kwa utii majukumu mbalimbali yaliyowekwa kwenye Taarifa ya Potsdam". Mwezi Oktoba mwaka huo, serikali ya China ilirudisha Taiwan iliyokaliwa kwa nguvu na Japan kwa miaka 50, na kufufua mamlaka yake huko Taiwan.

Profesa Xu Bodong alidhihirisha kuwa, "Taarifa ya Cairo" ilithibitisha suala la umiliki wa Taiwan kwa njia ya sheria ya kimataifa. Baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, Taiwan ilirudishwa China kisheria na kihalisi.

Wasikilizaji wapendwa, kutokana na ujulisho wetu, huenda mtakuwa mmeelewa hali ya ujumla ya ukweli wa mambo kuhusu Taiwan ni ardhi ya China tangu enzi na dahari. Lakini huenda mtakuwa na mashaka kuwa, kwa nini baadaye Taiwan na China bara zilikuwa katika hali ya uhasama? Je, kwa nini Taiwan na China bara hazijaungana mpaka sasa? Sasa tunaanza kuzungunmzia suala hilo.

Kwa ufupi, kuwepo tena kwa suala la Taiwan ni kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanzishwa na Chama cha Guomintang cha China katika miaka ya 40 ya karne iliyopita. Katika mwaka wa pili baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, Chama cha Guomintang cha China kilichowahi kushirikiana na Chama cha kikomunisti cha China katika mapambano dhidi ya uvamizi wa Japan, kilianzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe, sababu ya vita hivyo ni kuwa Chama cha Guomintang kilikataa kuanzisha serikali ya muungano na Chama cha Kikomunisti, kikaanzisha vita kujaribu kukiangamiza Chama cha kikomunisti cha China na kutaka kuanzisha utawala wake wa udikteta wa chama kimoja. Baada ya kufanya vita hivyo kwa miaka mitatu, Chama cha kikomunisti cha China ambacho kilikuwa na nguvu dhaifu ya kijeshi lakini kiliungwa mkono na wananchi wa China na kukishinda Chama cha Guomintang. Mwaka 1949, Chama cha kikomunisti cha China kilichopata ushindi kilianzisha Jamhuri ya Watu wa China, na nguvu ya Chama cha Guomintang iliyoshindwa ilirudi nyuma kufika kisiwa cha Taiwan na kukikalia kisiwa hicho ambacho eneo lake ni moja kwa mia tatu ya eneo la jumla la China. Chini ya msaada wa Marekani, nguvu hiyo ya chama cha Guomintang haitaimbui hadhi ya Jamhuri ya watu wa China ambayo ni mwakilishi halali wa China nzima. Mpaka hivi sasa, ingawa mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China bara na Taiwan yanaongezeka siku hadi siku, lakini hali ya uhasama kati ya pande hizo mbili bado haijakomeshwa rasmi.

Kuhusu ukweli wa mambo kuwa Taiwan ni sehemu moja ya China, msimamo wa jumuiya ya kimataifa ni wazi. Katika zaidi ya miaka 50 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, nchi zaidi ya 160 zimewekeana uhusiano wa kibalozi na China. Msingi wa kuanzisha uhusiano huo wa kibalozi kati ya China na nchi hizo ni kuwa nchi hizo zinapaswa kutambua serikali ya Jamhuri ya watu wa China ni serikali pekee halali inayowakilisha China nzima, na Taiwan ni sehemu moja ya China. Nchi hizo zilizowekeana uhusiano wa kibalozi na China, zote zilitoa ahadi zao hizo. Ingawa hivi sasa bado kuna nchi chache sana ambazo zimedumisha ati uhusiano wa kibalozi na utawala wa Taiwan, nchi hizo zote ni nchi ndogo zenye taabu za kiuchumi, utawala wa Taiwan ulichukua fursa hii kutumia pesa kuzishawishi na kuzivutia kudumisha ati uhusiano wa kibalozi na nchi hizo.

Mpaka sasa tumemaliza kuwasomea makala ya kwanza ya shindano la chemsha bongo kuhusu ujuzi wa "Taiwan-kisiwa cha hazina cha China". Katika kipindi kijacho tunawaletea makala ya pili ambayo itayowafahamisha sera ya kimsingi na juhudi za serikali ya China katika kutatua suala la Taiwan.

Haya basi sasa tunatoa maswali mawili ili mjibu:

1. Kisiwa cha Taiwan kiko kwenye eneo gani la China bara? Kati ya China bara na Kisiwa cha Taiwan kuna mlango bahari. Je, sehemu yenye umbali mfupi kabisa kati ya pande hizo mbili ni kilomita ngapi?

2. Mwaka 1943, nchi tatu za China, Marekani na Uingereza zilisaini taarifa moja ikithibitisha kisheria kuwa Taiwan ni sehemu moja ya ardhi ya China. Je, taarifa hiyo inaitwaje?

Na wiki ijayo tutawaletea makala ya pili ya chemsha bongo kuhusu Sera ya kimsingi na juhudi za serikali ya China ya kutatua suala la Taiwan, msikose kutusikiliza. Na makala hizo zitawekwa kwenye tovuti yetu ya mtandao wa internet moja baada ya nyingine, msisahau anuani ya tovuti yetu hiyo ya www.cri.cn, chagua kiswahili mtasoma makala zote na vipindi mbalimbali.

Idhaa ya kiswahili 2005-09-06