Mabadiliko yametokea hivi karibuni katika kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama cha Likud kati ya waziri mkuu wa Israel Bw. Ariel Sharon na waziri wa fedha wa zamani Bw. Benjamin Netanyahu. Upimaji wa maoni ya raia uliotolewa tarehe 6 kwenye gazeti la Haaretz la Israel unaonesha kuwa, kiasi cha uungaji mkono wa Netanyahu katika chama cha Likud kilipungua kwa asilimia 11 katika siku 11 zilizopita. Ingawa Netanyahu anamzidi Sharon kwa hivi sasa, lakini hali hiyo inaanza kubadilika kwa mwelekeo wa kumnufaisha Sharon. Mbinu za kujibu mashambulizi zilizofanywa na Sharon katika siku kadhaa zilizopita zimepata mafanikio kwa hatua ya mwanzo.
Mwezi uliopita, Netanyahu alitoa changamoto hadharani kwa Sharon ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Likud na kutangaza kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama cha Likud na waziri mkuu wa Israel wa awamu ijayo. Netanyahu aliungana na watu wenye msimamo mkali wa chama hicho, kujaribu kuhimiza kufanya haraka uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho na kumpindua Sharon.
Ili kukabiliana na changamoto za Netanyahu, Sharon alianzisha ulinzi wa maisha ya kisiasa. Tarehe 6 alikutana na maofisa wa manispaa wa mikoa wapatao zaidi ya 70 katika makazi yake mjini Jerusalem akiwataka wazuie juhudi za Bw. Netanyahu za kutaka uchaguzi wa mwenyekiti wa chama cha Likud ufanyike mapema. Bw. Sharon alishutumu kitendo alichofanya Netanyahu kwa ajili ya kuridhisha nia yake ya kisiasa. Bw. Sharon alisema kuwa Netanyahu anaweza kuendelea na madaraka katika chama cha Likud kwa zaidi ya mwaka mmoja, lakini anajitahidi kutanguliza uchaguzi wa chama hicho, Sharon alieleza kuwa anashindwa kuelewa na kitendo hicho cha uwazimu na hatarudi nyuma katika kukabiliana na kitendo hicho. Sharon anashikilia msimamo wake kuwa chama cha Likud kingefanya uchaguzi ndani ya chama mwezi Aprili mwakani kutokana na mpango uliowekwa na kuamini kuwa wanachama wa Likud wanaweza kufanya uchaguzi wao wa busara.
Malalamiko hayo ya Bw. Sharon pia ni wasiwasi wa wanachama wengi wa Likud. Kufanya uchaguzi mapema ndani ya chama cha Likud, kutasababisha kufanyika mapema kwa uchaguzi mkuu na kumalizika kwa hadhi ya utawala wa Likud. Sio tu madaraka ya mawaziri, wabunge na maofisa wa manispaa wa mikoa wa Likud hayataendelea, na mtu yeyote hawezi kuhakikisha kuwa chama cha Likud kitapata ushindi kwenye uchaguzi mkuu na kuwekwa kwa chama hicho kando ya mambo ya kisiasa.
Uchunguzi unaonesha kuwa ingawa kiasi cha uungaji mkono wa Netanyahu ndani ya chama cha Likud unazidi ule wa Sharon, lakini watu wanaomwunga mkono Netanyahu wameanza kubadilisha misimamo yao. Kwa Sharon na Netanyahu, nani atapata ushindi katika uchaguzi huo, watu watangoja matokeo ya mwisho.
Idhaa ya kiswahili 2005-09-07
|