Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-07 16:37:54    
Jumuiya ya kimataifa yaweza kukabiliana na mfumko wa bei ya mafuta

cri

Tangu shirika la nishati duniani liamue kutuliza bei ya soko la mafuta kwa kutumia mafuta ya akiba ya kimkakati, bei ya mafuta sokoni ilipungua kwa siku tatu mfululizo. Ukweli wa mambo umeonesha kuwa, kama jumuiya ya kimataifa ikiweza kuratibu vitendo vyao na kushirikiana vizuri, bei ya mafuta kwenye soko la kimataifa iliyokuwa inapanda mara kwa mara katika miaka miwili iliyopita inaweza kupungua na kurudi katika kiwango cha kawaida.

Tangu kimbunga ya Katrina kiikumbe sehemu ya Ghuba ya Mexico kusini mwa Marekani inayozalisha mafuta kwa wingi kuanzia mwishoni mwa mwezi Agosti, bei ya mafuta ghafi kwenye soko la kimataifa ilipanda juu na kuweka rekodi ya kihistoria mara kwa mara, hasa bei ya mafuta ya nchini Marekani iliwahi kuongezeka maradufu.

Ili kuisaidia Marekani kukabiliana na tatizo hilo la dharura, jumuiya ya kimataifa imetoa misaada mingi. Tarehe 2 mwezi huu, nchi wanachama 26 wa shirika la nishati duniani walikubali kwa kauli moja kutumia mafuta ya akiba ya kimkakati, yaani litatoa mapipa milioni 60 ya mafuta kwenye soko la kimataifa katika siku 30 zijazo. Kabla ya kimbunga ya Katrina kuikumba Marekani, nchi wanachama wa OPEC zikiwemo Saudi Arabia, Kuwait na Venezuela ziliamua kuongeza uzalishaji wa mafuta ya asili ili kupunguza ukosefu wa mafuta ulioongezeka siku hadi siku nchini Marekani. Baada ya kimbunga kuikumba Ghuba ya Mexico, serikali ya Canada iliahidi kuongeza mapipa elfu 91 ya mafuta kwa Marekani kwa siku. Isitoshe, Korea ya Kusini, Japan na nchi nyingine pia zimeamua kutumia mafuta ya akiba ya kimkakati.

Jambo hilo limeonesha wazi kuwa, jumuiya ya kimataifa inaweza kukabiliana na matatizo yoyote, likiwemo la mfumko wa bei ya mafuta duniani ikishirikiana pamoja.

Pili, Marekani inatakiwa kufanya kazi kubwa zaidi katika kutuliza bei za mafuta ghafi duniani. Marekani ni nchi kubwa ya kwanza duniani katika matumizi ya mafuta na uagizaji wa mafuta kutoka nje, pia ina akiba kubwa kabisa duniani ya mafuta ya kimkakati, hivyo kitendo chochote cha Marekani kitaathiri soko la mafuta ghafi duniani. Lakini kabla ya hapo kwa sababu kupanda kwa bei ya mafuta haikuleta pigo kubwa kwa Marekani, hivyo serikali ya Bush haikutekeleza wajibu wake ipasavyo kutokana na kuzingatia maslahi yake. Vyombo vya habari vimeeleza matumaini kuwa, Marekani itapata mafunzo kutokana na jambo hilo, kujishughulisha katika ushirikiano wa kimataifa pamoja na suala la nishati, katika zama tulizonazo ambazo nchi mbalimbali zinategemeana sana.

Tatu, mfumko wa bei ya mafuta ghafi wa hivi sasa umeleta athari kubwa kwa uchumi wa duniani na maisha ya binadamu, na mafuta yaliyoko ardhini yatamalizika hatimaye, hivyo namna ya kuokoa nishati ikiwemo mafuta, na kutafuta nishati nyingine zinazoweza kubadilisha mafuta limekuwa suala kubwa linaloikabili jumuiya ya kimataifa. Watu wanaamini kuwa, kama jumuiya ya kimataifa ikiweza kuimarisha ushirikiano kati yao, si ndoto kupata nishati mpya yenye usafi zaidi na ufanisi mkubwa zaidi.

Mwenyekiti wa OPEC, ambaye pia ni waziri wa nishati wa Kuwait Sheikh Ahmad alisema kuwa, bei ya mafuta ya hivi sasa sokoni imezidi kwa kiasi kikubwa kiwango chake halisi, kuna sababu nyingi zinazoathiri bei ya mafuta ghafi duniani, kwa hivyo, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kushirikiana vizuri ili kupata ufumbuzi wa muda mrefu na wenye ufanisi wa kuondoa upungufu wa mafuta duniani.

Idhaa ya kiswahili 2005-09-07