Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-08 15:11:34    
Misri yafanya uchaguzi wa urais wa moja kwa moja kwa mara ya kwanza

cri

Tarehe 7 Misri ilifanya uchaguzi wa rais wa moja kwa moja kwa mara ya kwanza unaowashirikisha wagombea kumi akiwemo Hosni Mubarak, ambaye ni rais wa sasa ambaye pia ni mgombea wa chama tawala cha demokrasia cha taifa, Ayman Nour ambaye ni mgombea wa chama cha Al-Ghad ambacho ni chama kikubwa cha upinzani na Numan Gumaa, mgombea wa chama cha New Wafd.

Kutokana na takwimu zilizotolewa na tume kuu ya uchaguzi ya Misri, wapiga kura halali wenye umri wa miaka 18 wapatao milioni 32 kati ya watu wote milioni 74.9 wa nchi hiyo wamejiandikisha kushiriki kwenye uchaguzi huo. Matokeo ya uchaguzi huo yatatangazwa tarehe 9 au tarehe 10.

Asubuhi ya siku hiyo, kwenye kituo cha upigaji kura ndani ya shule moja iliyoko katika wilaya ya Mhandiseen mjini Cairo, kwa kuwa siku hiyo sio siku ya mapumziko, wapiga kura waliingia mmoja mmoja au vikundi vikundi kwenye kituo hicho. Baada ya kupiga kura, baadhi waliwaonesha waandishi wa habari kidole chenye rangi nyekundu. Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu na mzee mmoja anayefanya kazi katika kampuni ya umeme walisema kuwa wanamwunga mkono rais wa sasa Mubarak.

Ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika bila matatizo, serikali ya Misri imeimarisha ulinzi kwenye vituo mbalimbali vya upigaji kura. Polisi walikuwa wamesimama kwenye vituo hivyo. Zaidi ya hayo, majaji, wafanyakazi wa idara za sheria na wajumbe wa vyama mbalimbali walipelekwa katika vituo hivyo kusimamia upigaji kura, ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki.

Vyombo vya habari vya Misri vinaona kuwa kati ya wagombea kumi wa urais, rais Mubarak aliyetawala Misri kwa miaka 24 anaweza kuchaguliwa kuwa rais kwa mara tano mfululizo. Vyombo vya habari vinaona kuwa Mubarak aliposhika madaraka ya urais nchini Misri, alitoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya Misri na kufanya kazi kubwa kwa ajili ya kuinua hadhi ya Misri duniani na katika Mashariki ya Kati. Rais Mubarak mwenyewe pia amepata heshima kubwa nchini Misri na katika nchi za nje. Ikilinganishwa na Mubarak, wagombea wengine tisa wako nyuma sana. Hivi sasa, mgombea wa chama cha Al-Ghad, wakili mwenye umri wa miaka 40 Ayman Nour anaweza kuwa mpinzani mkubwa wa Mubarak. Kwa kuwa chama cha Al-Ghad kinachoongozwa na Ayman Nour kilianzishwa mwezi Oktoba mwaka jana, kwa hiyo hakina athari kubwa katika jamii na baraza la kisiasa nchini Misri. Kwa hiyo Ayman Nour anashindwa kupambana na Mubarak. Mgombea mwingine wa chama cha New Wafd Numan Gumaa mwenye umri wa miaka 71 alieleza faraghani kuwa alilazimishwa kugombea nafasi hiyo na chama hicho. Wagombea wengine saba, hawajulikani kwa wapiga kura. Kwa hiyo inawezekana kusema kuwa hakuna taabu kwa Bwana Mubarak kuchaguliwa kuwa rais.

Vyombo vya habari vinaona kuwa uchaguzi wenye wagombea wengi unatokana na Marekani kutoa mpango mkuu wa demokrasia ya Mashariki ya Kati, ni matokeo ya kusujudu kwa shinikizo la magharibi. Lakini uchaguzi huo wa rais wa moja kwa moja unafanywa kutokana na uamuzi wa Misri yenyewekwa mujibu wa hali halisi ya nchi hiyo. Jambo hilo linaonesha kuwa Misri imepiga hatua muhimu kwa ajili ya kuhimiza mchakato wa mageuzi ya kisiasa.

Idhaa ya kiswahili 2005-09-08