Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-08 21:17:18    
Mamlaka ya Bahari na Visiwa

cri

Mwambao wa nchi kavu ya China unaanzia mlango wa Mto Yalu wa Mkoa wa Liaoning wa kaskazini hadi Mlango wa Mto Beilun wa Mkoa wa Guangxi wa kusini, urefu wake ni kilomita 1,800. Hali ya kijiografia ya pwani za bahari ni tambarare, ambapo kuna bandari na ghuba nyingi zenye hali bora, na nyingi ni bandari ambazo maji yake hayawezi kuganda kwa mwaka mzima. Kuna bahari kubwa 5 za karibu nchini China kama vile Bahari ya Bo, Bahari ya Huang, Bahari ya Mashariki, Bahari ya Kusini pamoja na Sehemu ya Bahari ya Pasifiki ya mashariki ya Taiwan. Miongoni mwa hizo, Bahari ya Bo ni bahari ya ndani ya China. Sehemu ya Bahari ya Pasifiki ya mashariki ya Taiwan inaanzia Visiwa vya Xiandao vya kaskazini vilivyoko kusini magharibi ya Visiwa vya Ryukyu vya Japan, mpaka kwenye Mlango wa Bahari ya Bashi wa kusini.

Eneo la bahari la China ni pamoja na maji ya ndani na mamlaka ya bahari ya China, eneo lake la jumla ni zaidi ya kilomita 380,000. Maji ya ndani ya China ni eneo la bahari la Jamhuri ya watu wa China toka mstari wa mamlaka ya bahari unaoelekea upande wa nchi kavu hadi mwambao wa bahari. Upana wa mamlaka ya bahari ya China ni nautical maili 12 kuanzia mstari wa bahari.

Kwenye eneo la bahari ya China kuna visiwa zaidi ya 5000, eneo lake la jumla ni kilomita za mraba 80,000, mwambao wa visiwa ni kilomita za mraba 14,000. Miongoni mwao Kisiwa cha Taiwan ni kikubwa zaidi kuliko vingine vyote, eneo lake ni kilomita za mraba 36,000; Kisiwa cha Hainan ni cha pili kwa ukubwa wake, eneo lake ni kilomita za mraba 34,000. Visiwa vya Diaoyu na Visiwa vya Chiwei vilivyoko kwenye bahari ya kaskazini mashariki ya Kisiwa cha Taiwan ni visiwa vilivyoko kwenye sehemu ya mashariki kabisa ya China. Visiwa vya Dongsha, Visiwa vya Xisha, Visiwa vya Zhongshan na Visiwa vya Nasha vilivyoko kusini kabisa ya China vinaitwa kuwa ni visiwa mbalimbali vya Bahari ya Kusini.

Hali ya Jiografia

China ni nchi yenye milima mingi, eneo la sehemu za milimani linachukua theluthi mbili ya eneo la jumla la nchi nzima. Sehemu hizo za milimani ni pamoja na ardhi milimani, vilima na nyanda za juu. Katika eneo lote la China ardhi ya milima inachukua 33 %, nyanda za juu 26 %, mabonde 19 %, tambarare 12 % na vilima 10 %.

Katika mamilioni ya miaka kadhaa iliyopita, Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet ulikuwa kama nundu kwenye ardhi duniani, maumbo ya ardhi ya China yakatokana na uwanda huo. Ukiiangalia ardhi ya China kutoka angani, hali ya kijiografia ya China ni kama ngazi inayoelekea mashariki kutoka magharibi, inatelemka hatua kwa hatua. Kutokana na kugongana kati ya ardhi ya India na ardhi ya Ulaya na Asia, Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet ulijitokeza siku hadi siku, mwinuko wake kwenye usawa wa bahari ni zaidi ya mita 4000, hivyo uwanda huo unaitwa kuwa ni "Paa la dunia", na kuwa ngazi ya kwanza kwenye ardhi ya China. Kilele kikuu cha Jomolangma cha Mlima Himalaya kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet kina urefu wa mita 8848.13, ambacho ni kilele cha juu cha kwanza duniani. Ngazi ya pili inaundwa na Uwanda wa Juu wa Mongolia ya ndani, Uwanda wa juu wa Huangtu, Uwanda wa Juu wa Yungui pamoja na Bonde la Talimu, Bonde la Zhungeer na Bonde la Sichuan, wastani wa mwinuko wake kutoka usawa wa bahari ni mita 1000-2000. Ukipita ukingo wa mashariki wa ngazi ya pili ni ngazi ya tatu inayoundwa na Milima Daxinganling, Milima Taihan, Mlima Wu na Mlima Xuefeng inayoelekea pwani ya mashariki ya bahari ya Pasifiki. Katika sehemu ya mwinuko unaotelemka chini ya mita 500 hadi 1000, kuna Tambarare ya Kaskazini ya mashariki, Tambarare ya Kaskazini, na Tambarare ya eneo la katikati na chini ya mtitiriko wa Mto Changjiang, na katika sehemu ya ukingoni mwa tambarare hizo kuna milima mifupi na vilima. Mashariki ya sehemu hiyo ni sehemu inayoelekea kwenye bahari ya China yaani ngazi ya nne, ambapo kimo cha maji ya sehemu kubwa ni chini ya mita 200.

Milima mingi mikubwa na mirefu imekuwa kama "mifupa" ya ardhi ya China, na kuundwa kuwa mifumo mingi tofauti ya milima. Milima mikubwa maarufu ya China ni: Milima Himalaya, Milima Kunlun, Milima Tiansha, Milima Tanggula, Milima Qinling, Milima Daxinganling, Milima Taihang, Milima Qilian, na Milima Hengduan.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-08