Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-09 15:38:21    
Rais wa zamani wa Marekani asifu kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi nchini China

cri

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton tarehe 8 alifanya ziara katika mji wa Kunming mkoani Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China, ili kukagua kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi nchini China. Bw. Clinton alisifu kazi hiyo ya China.

Bw. Clinton alisema kuwa, China imeanzisha miradi mingi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi, ambayo inapaswa kuenezwa na kuwahudumia watu wengi zaidi.

Hali ya ugonjwa wa ukimwi mkoani Yunnan ni mbaya nchini China. Tangu mwaka 2004, mfuko wa Clinton ulianza kuiunga mkono kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi mkoani Yunnan. Mwezi Juni mwaka huu, mkoa wa Yunnan na mfuko wa Clinton walisaini mkataba wa ushirikiano, pande mbili zilianzisha mradi mmoja wa ushirikiano wa miaka mitatu ili kutoa huduma na matibabu bora kwa wagonjwa wa ukimwi wa sehemu ya Dali na sehemu nyingine za Yunnan, katika miaka kadhaa ijayo, miradi hiyo ya ushirikiano itaongezwa zaidi.

picha husika>>

1  2