Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-09 20:02:19    
Mpango wa mawasiliano kati ya wanafunzi wa China na Kenya kujenga daraja la urafiki kati ya nchi hizo mbili.

cri

Tarehe 4 mwezi Septemba, wanafunzi 12 kutoka Kenya waliopata msaada wa kulipiwa gharama za masomo na serikali ya China, walipanda ndege kutoka Nairobi kuelekea China kuanza masomo yao katika nchi ya kigeni. Tarehe 26, mwezi Agosti, Ubalozi wa China nchini Kenya ulifanya sherehe kubwa ya kuwasindikiza wanafunzi hao. Balozi wa China nchini Kenya Bw. Guo Chongli aliwapa wanafunzi hao taarifa ya vyuo vikuu vya China vitakavyowapokea, na tiketi za ndege. Kwenye sherehe hiyo, Bw. Guo alitoa hotuba akisema:

"Kwanza, kwa niaba ya serikali ya China, nawapa mkono wa pongezi wanafunzi 12 wa Kenya mliopata fursa ya kusoma nchini China. Natumai kuwa, mtafanikiwa kumaliza masomo yenu na kurudi kutoa mchango kwa maendeleo ya nchi yenu. Wakati huo huo, Natumai kuwa mtafanya juhudi kuongeza mawasiliano kati ya China na Kenya, na kukuza urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili."

Kwenye hotuba hiyo, Bw. Guo alieleza kuwa, tangu serikali za China na Kenya zilipoanza kutekeleza mpango wa kuwasomesha wanafunzi mnamo mwaka 1982, mpaka sasa wanafunzi wapatao 200 kutoka nchi hizo mbili wamesema na kumaliza masomo yao katika nchi hizo. Mpango huo unahimiza maelewano kati ya nchi hizo mbili zilizo tenganishwa kwa umbali mkubwa, na kujenga daraja linalokuza urafiki kati yao.

Habari zinasema kuwa, wanafunzi hao 12 wa Kenya watasoma kwa miaka 4 hadi 6 katika vyuo vikuu kumi vya China kikiwemo Chuo Kikuu cha Wuhan na Chuo Kikuu cha Udaktari cha China.

Kizazi wa Msafiri mkuu wa China Zhenghe Mwamaka Sharif atasomea kozi ya udaktari nchini China. Akiwa mwakilishi wa wanafunzi hao, alitoa shukrani kwa serikali ya China kwa kuwapa wanafunzi wa Kenya fursa hiyo ya kusoma nchini China, akisema:

Bw. Kinyagia Benson Mburu alikuwa mtumishi wa serikali ya Kenya, alipata fursa hiyo ya kusoma nchini China baada ya ushindani mkali. Alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, atasomea shahada ya udaktari ya somo la viumbe katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Kusini mwa China. Bw. Mburu anasema:

Bw. Mburu alieleza kuwa, baada ya kumaliza masomo yake nchini China, atarudi Kenya na kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya taifa lake kwa kutumia ujuzi wake unaopatikana nchini China. Anasema:

Alipozungumzia Mpango wa kusomesha wanafunzi kati ya China na Kenya, Bw. Mburu anasema:

Mwaka 2003, wanafunzi wa Kenya waliosoma nchini China walianzisha chama chao maalum. Bw. Ondiaka ni mwanzilishi muhimu wa Chama cha Wanafunzi Wakenya waliosoma Nchini China, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho. Aliwahi kusoma nchini China kwa miaka 9, na anaweza kuzungumza kichina sanifu. Kutokana na kuishi kwa muda mrefu nchini China, Bw. Ondiaka anafahamu nchi hiyo katika maeneo mbalimbali. Bw. Ondiaka alianza kusoma nchini China mwaka 1986. Kukaa nchini China kwa muda mrefu kulimfanya aipende sana China na watu wa China, na alioa msichana mchina ambaye pia ni daktari, na walianzisha kliniki huko Nairobi nchini Kenya. Hivi sasa wana watoto wawili. Alipozungumzia Chama cha wanafunzi wakenya waliosoma nchini China, Bw. Ondiaka alisema, madhumuni ya kuanzisha chama hicho ni kuzidisha maelewano kati ya watu wa Kenya na China, na kukuza urafiki kati ya nchi hizi mbili.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-09