Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-13 15:11:45    
Sera ya kimsingi na juhudi za serikali ya China ya kutatua suala la Taiwan

cri

       Wasikilizaji wapendwa karibuni katika kipindi hiki cha shindano la chemsha bongo kuhusu ujuzi wa "Taiwan-kisiwa cha hazina cha China". Katika kipindi kilichopita tuliwaletea makala ya kwanza kuhusu Kisiwa cha Taiwan ni sehemu moja ya ardhi ya China na sababu ya kutokea kwa suala la Taiwan. Leo tunawaletea makala ya pili ambayo itawajulisha sera ya kimsingi na juhudi za serikali ya China katika kutatua suala la Taiwan.

Wasikilizaji wapendwa, mlikuwa mkisikiliza rekodi ya hotuba aliyotoa rais Hu Jintao wa China mwezi Machi mwaka huu kuhusu utatuzi wa suala la Taiwan. Katika hotuba yake hiyo rais Hu alisema kuwa, China inamkaribisha mtu yeyote na chama chochote cha Taiwan juu ya juhudi zao za kuelekea kutatua kanuni ya kuwepo kwa China moja. Kama wanatambua kanuni ya kuwepo kwa China moja, bila kujali yeye ni mtu gani, chama gani, au zamani walisema nini na kufanya nini, tunapenda kuzungumza nao kuhusu kuendeleza uhusiano kati ya China bara na Taiwan na kuhimiza muungano wa amani.

Tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China mwaka 1949, serikali ya China siku zote haikuacha juhudi zake kutafuta muungano kamili wa taifa. Sera ya kimsingi ya serikali ya China katika kutatua suala la Taiwan ni "muungano wa amani, nchi moja mifumo miwili". Mambo muhimu ya sera hiyo ni kufanya juhudi kutimiza muungano wa pande mbili kwa kupitia mazungumzo ya amani, baada ya kutimiza muungano, uti wa mgongo wa taifa yaani China bara itashikilia mfumo wa ujamaa, na Taiwan itadumisha mfumo wake wa kibepari wa sasa, na kutoubadilisha kwa muda mrefu.

Katika miaka mingi iliyopita, serikali ya China imefanya juhudi za kusukuma mbele uhusiano kati ya China bara na Taiwan. Baada ya juhudi za pamoja za pande hizo mbili, katika kipindi cha mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, hali ya kutenganishwa kabisa karibu kwa miaka 40 kati ya pande hizo mbili ilivunjwa, ambapo mawasiliano ya kiuchumi, kiutamaduni na kati ya watu yamepata maendeleo makubwa. Takwimu zimeonesha kuwa, katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, thamani ya biashara kati ya China bara na Taiwan ilifikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 400, na urali wa biashara ya Taiwan ulifikia dola za kimarekani bilioni 300. China bara pia ilifanya juhudi kuweka hali mwafaka ya kuwawezesha ndugu wa Taiwan kuja China bara kukutana na jamaa zao, kufanya utalii na kufanya biashara. Hivi sasa kuna wakazi laki kadhaa wa Taiwan wanaofanya kazi, kusoma na kuishi China bara. Ili kuhakikisha haki na maslahi halali ya wakazi wa Taiwan walioko China bara, chombo cha utungaji wa sheria cha China na serikali kuu ya China pamoja na serikali za sehemu mbalimbali nchini China zimetunga sheria na kanuni kadha wa kadha na kuzitekeleza kihalisi. Wakati huo huo serikali ya China pia inafanya juhudi za kuhimiza pande mbili zianzishe mazungumzo ya kisiasa.

Lakini upande wa Taiwan uliweka vikwazo vingi vya kuwazuia wakazi wa China bara kwenda Taiwan kukutana na jamaa zao, kufanya utalii na kufanya biashara, vikwazo hivyo vimezuia mawasiliano zaidi kati ya ndugu wa China bara na Taiwan. Hasa katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na chama cha Guomintang cha China kupoteza nafasi ya utawala huko Taiwan, na shughuli za nguvu ya ufarakanishaji ya Taiwan kuchacha siku hadi siku, watawala wa huko walitembeza kijeuri sera ya kuifanya Taiwan ijitenge na China, na kutotambua ukweli wa mambo kuhusu Taiwan kuwa ni sehemu moja ya China, hii imesababisha hali ya wasiwasi ya uhusiano kati ya China bara na Taiwan.

Hata hivyo, serikali ya China bado inashikilia juhudi za kutafuta muungano wa amani wa China bara na Taiwan. Katika hotuba yake ya mwezi Machi kuhusu utatuzi wa suala la Taiwan, Rais Hu Jintao wa China alisema:

Upande wa China bara kamwe hautaacha juhudi za kutimiza muungano wa amani wa pande mbili. Upande wa China bara utafanya juhudi kubwa kadiri iwezekanavyo, mambo yoyote yanayowanufaisha ndugu wa Taiwan, mambo yoyote yanayosaidia kuhimiza mawasiliano kati ya pande mbili, na mambo yoyote yanayosaidia kulinda amani ya sehemu ya Mlango wa bahari wa Taiwan, China bara itayafanya mambo hayo na hakika itayafanya vizuri.

Na kuhusu vitendo vya utawala wa Taiwan vya kuzidisha siku hadi siku shughuli za kuifanya Taiwan kujitenga na China, pamoja na majaribio ya nguvu ya nchi nyingine fulani ya kuingilia kati muungano wa China, serikali ya China pia imetangaza rasmi mara kwa mara kuwa, ili kulinda muungano wa taifa, serikali ya China haiahidi kuacha uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi. Katika hotuba yake ya mwezi Machi mwaka huu kuhusu utatuzi wa suala la Taiwan, Rais Hu Jintao wa China alisisitiza tena msimamo huo imara. Akisema:

Kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ni maslahi makuu ya taifa. Mtu yeyote akitaka kuhataharisha mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, wananchi wa China wapatao bilioni 1.3 kamwe hawataweza kukubali. Kuhusu suala kubwa la kikanuni la kupinga kufarakanisha taifa, kamwe hatutaweza kusitasita, kutoonesha msimamo wazi au kurudi nyuma hata kidogo. China ni China ya wananchi wa China wapatao bilioni 1.3 pamoja na ndugu wa Taiwan wapatao milioni 23, suala lolote linalohusu mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya China, linapaswa kuamuliwa na wananchi wote wa China nzima.

Aidha, mwezi Machi mwaka huu, chombo chenye madaraja ya juu kabisa cha China pia kilitoa sheria moja inayoitwa "Sheria ya kupinga kufarahakisha taifa", ndiyo maana sera ya kimsingi ya serikali ya China katika kutatua suala la Taiwan na nia ya kupinga ufarakanishaji zimedumishwa kisheria.

Ili kutafuta amani na utulivu wa sehemu ya Mlango bahari wa Taiwan na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China bara na Taiwan, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, Chama cha kikomunisti cha China na katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China Bwana Hu Jintao alimwalika mwenyekiti wa chama cha Guomintang cha China ambacho ni chama kikuu kisichotawala cha Taiwan Bwana Lian Zhan afanye ziara China bara. Mwishoni mwa mwezi Aprili, viongozi wakuu wa vyama hivyo viwili walifanya mazungumzo kwa mara ya kwanza tokea China bara na Taiwan zikae katika hali ya uhasama katika miaka 56 iliyopita, ambapo pande hizo mbili zilifikia maoni mengi ya pamoja kuhusu kuzihimiza China bara na Taiwan zirudishe mapema iwezekanavyo mashauriano kwenye hali ya usawa juu ya msingi wa kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja. Baada ya mwenyekiti wa chama cha Guomintang kufanya ziara China bara, wenyeviti wa chama cha Qingmin na chama cha Xindang ambavyo ni vyama vingine visivyotawala vya Taiwan pia walifanya ziara China bara, na kufikia maoni ya pamoja na Bwana Hu Jintao kama yale yaliyofikiwa kati ya Bwana Hu Jintao na Bwana Lian Zhan.

Hivi sasa chama cha Guomintang na chama cha Qingmin na chama cha Xindang vimeundwa kuwa muungano ambavyo vina wingi zaidi wa viti kwenye "Baraza la utungaji wa sheria" la Taiwan. Ingawa vitendo vya kuoneshea moyo mwema kati ya China bara na vyama hivyo vitatu vya Taiwan vililaaniwa na utawala wa Taiwan unaoshikilia msimamo wa kuifanya Taiwan ijitenge na China, lakini vimesifiwa na kuungwa mkono zaidi na watu wa pande mbili za Mlango wa bahari wa Taiwan na jumuiya ya kimataifa, ambapo wameeleza matarajio yao mema juu ya mustakabali wa uhusiano kati ya China bara na Taiwan.

Wasikilizaji wapendwa, hadi hapo ndiyo tumemaliza kusoma makala ya pili ya shindano la chemsha bongo kuhusu ujuzi wa "Taiwan-kisiwa cha hazina cha China". Sasa tunatoa maswali mawili ili mjibu:

1. Sera ya kimsingi ya serikali ya China ya kutatua suala la Taiwan inasemaje?

2. Mwezi Machi mwaka huu, Bunge la umma la China ambalo ni chombo chenye madaraka ya juu kabisa cha China, lilipitisha sheria muhimu ikidumisha sera ya kimsingi ya serikali ya China ya kutatua suala la Taiwan na nia ya kupinga ufarakanishaji wa taifa, tafadhali eleza sheria hiyo inaitwaje?

Na wiki ijayo tutawaletea makala ya tatu ya chemsha bongo kuhusu serikali ya China yafanya juhudi za kusukuma mbele mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China bara na Taiwan ili kuwanufaisha wananchi wa pande hizo mbili. Msikose kutusikiliza. Na makala zote za chemsha bongo tutaziweka kwenye tovuti yetu. Msisahau anuani ya tovuti yetu ya www.cri.cn.

Idhaa ya kiswahili 2005-09-13