Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-13 16:57:39    
Mkutano utakaoamua mustakbali wa Umoja wa Mataifa

cri

Mkutano wa wakuu wa kuadhimisha miaka 60 ya Umoja wa Mataifa utafanyika huko New York, makao makuu ya umoja huo kuanzia tarehe 14 hadi 16 mwezi huu. Mpaka sasa wakuu wa nchi au wa serikali wapatao zaidi ya 180 wamejiandikisha kuhudhuria mkutano huo. Rais Hu Jintao wa China pia atahudhuria mkutano huo. Huu utakuwa ni mkutano mkubwa zaidi na wa ngazi ya juu zaidi katika historia ya Umoja wa Mataifa. Matokeo ya mkutano huo yataleta athari kubwa na muhimu kwa maendeleo ya siku za baadaye za Umoja wa Mataifa na hali ya kimataifa.

Umoja wa Mataifa ulianzishwa baada ya vita vya pili vya dunia. Katika mchakato wa maendeleo yake ya miaka 60 iliyopita, Umoja wa Mataifa ikiwa jumuiya ya kimataifa inayowakilisha nchi nyingi zaidi na wenye heshima kubwa zaidi, umetoa mchango mkubwa kwa ajili ya kulinda amani na usalama wa dunia, kuhimiza usawazishaji na ushirikiano wa kimataifa na kusukuma mbele ustawi na maendeleo ya dunia nzima. Baada ya kuingia karne mpya, Umoja wa Mataifa umekabiliwa na mabadiliko makubwa ya hali ya kimataifa, muundo wa nchi wanachama na jukumu la kihistoria. Vitendo vya upande mmoja au vya kibabe vya nchi fulani vimeufanya Umoja wa Mataifa uwekwe ukingoni siku hadi siku, pamoja na hali ya kuwepo kwa mashirika mengi kupita kiasi ya Umoja wa Mataifa, yote hayo yameufanya Umoja wa Mataifa ufike kwenye njia panda.

Ingawa heshima ya maamuzi ya Umoja wa Mataifa imekabiliwa na changamoto, lakini hadhi na umuhimu wa Umoja wa Mataifa hauruhusu mtu yeyote kuutisika. Umoja wa Mataifa unahitaji kufanyiwa mageuzi ili kupata nguvu mpya ya uhai. Jumuiya ya kimataifa inatarajia kuimarisha umuhimu wa Umoja wa Mataifa baada ya kufanya mageuzi kwake, ili kuongeza heshima yake ya maamuzi. Lakini kuhusu mambo halisi ya mageuzi hayo, kuna migongano mikubwa kati ya nchi mbalimbali. Nchi nyingi zinazoendelea zinafuatilia zaidi utekelezaji wa "malengo ya maendeleo ya milenia", na kutarajia kwa dharura kuondoa umaskini kwa kupitia maendeleo; lakini nchi fulani nyingine zinasisitiza zaidi upanuzi wa baraza la usalama, na kuyachukulia mageuzi ya Umoja wa Mataifa kama fursa kwao ya kuziwezesha kuwa wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama.

Jambo linalohitajiwa kudhihirishwa ni kuwa, mageuzi ya Umoja wa Mataifa ni mradi wenye matata utakaofanyika kwa pande zote, upanuzi wa baraza la usalama ni sehemu moja tu kati ya kazi hizo. Umoja wa Mataifa unapaswa kuzingatia ipasavyo maslahi ya nchi nyingi zinazoendelea, na kuzingatia kwanza suala la maendeleo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Kofi Annan hivi karibuni ameeleza kuwa, "malengo ya maendeleo ya milenia" ya Umoja wa Mataifa ni jukumu la pamoja la nchi zilizoendelea na zinazoendelea, malengo hayo yanaihimiza jumuiya ya kimataifa ianzishe ushirikiano mkubwa ambao haukufanyika hapo awali, na yatazinufaisha pande mbili.

Jumuiya ya kimataifa inatilia maanani sana kuwa na matumaini makubwa juu ya mkutano wa wakuu wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika hivi karibuni. Viongozi wa nchi zaidi ya 180 wakikusanyika pamoja na kujadili kwa kina kuhusu namna ya kuimarisha umuhimu wa Umoja wa Mataifa, kuhimiza mageuzi ya Umoja wa Mataifa, na kutatua suala la maendeleo. Wakati huo huo mazungumzo kwenye kikundi cha kazi cha kiini cha Umoja wa Mataifa pia yameingia katika kipindi chake cha mwisho, na kinatazamiwa kufikia maoni ya pamoja kabla ya kufanyika kwa mkutano wa wakuu wa Umoja wa Mataifa, hii itahakikisha mkutano huo utaweza unafanikiwa.

China siku zote inaunga mkono Umoja wa Mataifa uoneshe umuhimu wake katika kulinda amani ya dunia na kusukuma mbele maendeleo ya pamoja. China inapenda kushirikiana pamoja na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kuhimiza mkutano wa wakuu upate matokeo yenye juhudi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-13