Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-14 16:48:49    
Sherehe ya kwanza ya kupewa cheo cha juu cha masomo ya elimu ya dini ya kibudhaa ya kitivo cha lugha ya kitibet yafanyika

cri

Tarehe 12 Septemba, katika Hekalu la Tal la Qinghai, Chuo cha elimu ya ngazi ya juu ya dini ya kibudhaa cha kitivo cha lugha ya kitibet cha China, kilifanya mahafali ya kwanza ya kuhitimu masomo kwa wanafunzi wa darasa la kupewa cheo cha juu cha elimu, ambapo wanafunzi 11 walioshiriki kwenye mtihani wa kujibu maswali ya misahafu walifanikiwa kupita mtihani na kupewa kitambulisho cha kuhitimu masomo, tena wamepata haki ya kuja Beijing katikati ya mwezi Oktoba kushiriki mtihani wa kujibu maswali juu ya makala ya taaluma na misahafu.

Katika mtihani wa kuhitimu masomo uliofanyika kwa siku 8, watawa 11 walioshiriki mtihani wakifuata mambo yaliyomo kwenye kitabu cha "Elimu ya dini ya kibudhaa ya kitibet ya juzuu tano" ambacho ni kitabu maarufu cha dini ya kibudhaa ya kitibet walijibu maswali kwa kufuata desturi za jadi za dini ya kibudhaa ya kitibet za kutetea misahafu. Baada ya kukabiliana na watu 15 wenye ujuzi wa misahafu kutoka mahekalu makubwa ya dini ya kibudhaa ya kitibet, na kupitia kamati ya ukaguzi iliyoundwa na masufii wa ngazi ya juu wenye ujuzi mkubwa wa elimu walioalikwa kutoka mikoa ya Qinghai, Tibet, Sichuan na Gansu, wanafunzi hao 11 walikamilisha vizuri mtihani wa kuhitimu masomo.

Wanafunzi hao 11 walioshiriki mtihani huo ni wanafunzi wa darasa la kwanza la kupewa cheo cha juu cha elimu walioandikishwa mwaka 2004 kutokana na utaratibu mpya wa kutoa cheo cha juu cha elimu, wanafunzi hao walichaguliwa kutoka sehemu za kabila la watibet za mikoa ya Tibet, Qinghai, Gansu na Sichuan nchini China.

Naibu mkuu wa chuo cha elimu ya dini ya kibudhaa ya ngazi ya juu ya kitivo cha lugha ya kitibet cha China Bwana Li Guoqing alisema kuwa, kufanikiwa kwa mtihani wa kuhitimu masomo kwa wanafunzi wa darasa la kupewa cheo cha juu cha elimu, kumeonesha kuwa utekelezaji wa utaratibu wa kutoa cheo cha juu cha elimu ya dini ya kibudha ya kitibet umepiga hatua moja yenye umuhimu. Mwezi Oktoba wanafunzi hao watashiriki tena kwenye mtihani mjini Beijing, ambapo watajibu maswali kuhusu makala za taaluma na misahafu, watakaopita mtihani watapewa cheo cha juu cha elimu kwa mara ya kwanza, na kazi ya kutoa cheo cha juu cha elimu ya dini ya kibudhaa ya kitibet itakamilishwa kwa mara ya kwanza nchini China.

Mwanafunzi kutoka hekalu la Tal la Qinghai aliyepita mtihani Bwana Jianchangongbao alimwambia mwandishi wa habari kuwa, kushiriki masomo kwenye darasa la kupewa cheo cha juu cha elimu ya dini ya kibudha ya kitibet si kama tu kumepanua upeo wake, bali pia kumemfanya apate nafasi ya kubadilishana maoni na watawa wengine kutoka sehemu za kabila la watibet. Kufanya mtihani wa kujibu maswali juu ya elimu ya dini ya kibudha ya kitibet ni kwa ajili ya kujadili elimu ya dini na misaafu, kupima matokeo ya masomo ya watawa, hii imeonesha sera ya chama na serikali ya China kuhusu dini, ambayo ina umuhimu mkubwa kwa kuenzi utamaduni wa kidini wa sehemu za kabila la watibet.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-14