Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-14 19:23:18    
Mapishi ya kupika nyama ya ng'ombe pamoja na giligilani

cri

Mahitaji

Giligilani gramu 300, nyama ya ng'ombe gramu 150, vipande vya

vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi kila kimoja kijiko 1/3,

chumvi kijiko 1/2, mafuta ya ufuta kijiko 1, mvinyo wa kupikia kijiko 1,

mchuzi wa soya kijiko 1, wanga kijiko 1/2

Njia

1. osha giligilani na uikata iwe vipande. Kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, na uiweke kwenye bakuli moja, tia mvinyo wa kupikia, mchuzi wa soya, wanga na korogakoroga.

2. tia mafuta kwenye sufuria, pasha moto mpaka yawe nyuzi ya 60, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi korogakoroga kwa haraka, tia chumvi kisha koroga koroga. Punguza moto tia vipande vya giligilani na mafuta ya ufuta, korogakoroga halafu uipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.